Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Upepo wa mapambano kati ya majenerali wawili nchini Sudan unaonekana kubadilika ghafla dhidi ya Hemedti.
Jeshi linaloongozwa na generali Burhani limesema kwa sasa wananchi wate waliobaki mjini Khartoum wabaki ndani na wasichungulie madirishani kwani wameanza kutumia vifaru kushambulia kutoka pembe zote ili kuwang'oa askari wa genrel Hemedti.
Hii ni baada ya kampeni ya takriban wiki tatu ya kushambulia kutoka angani kupiga karibu na ikulu,makao makuu ya jeshi na uwanja wa ndege ambako RSF walifanikiwa kuyashikilia.
Hali inaonekana ni mbaya kwa RSF kwani wameishia kushikilia maeneo muhimu ya Khartoum tu na kubakisha maeneo yote mpaka Port Sudan chini ya udhibiti ya jeshi.Hilo limetoa fursa kwa jeshi kujitengenezea nguvu kubwa ya kuukomboa mji mkuu wa Khartoum.