sijui kwanini watu wanapinga sana hizi harakati za kuwawajibisha wasiolipa kodi wakati ndo kilikua kilioMbona sapna ilivyopigwa pin watu mlishangilia? Mbona Bakhresa mlishangilia? Eti uzi utokee, uende wapi? Kama si sahihi kilichorushwa kiteteeni na si mods wakitoe. Ukiona mwenzako ananyolewa......
wewe dada vitu vyako unauza ghali kuliko kawaida kwa kigezo unalipa kodi? kodi ipi
lakini pia juzi ulipost kwamba watu wajiandae kwa upotevu wa makontena kama walipitisha bila kulipia kumbe na wewe ni mmoja wa mapapa naam ni mmoja maana ushampost sana "yule jamaa anaesafirisha bidhaa kwa miujiza kufika kwako bila kodi" ukisifia sana kuhusu ubora wa huduma zake duh wewe kumbe haulipi kodi
Ingawa simjui huyu mdada unayemshambulia, post yako imekaa kimajungu, otherwise tupe evidence.
Evidence gani tena, na kwa nini udhani ni majungu? Mbona kwa SSB na ICD yake hukudhani ni majungu?Ingawa simjui huyu mdada unayemshambulia, post yako imekaa kimajungu, otherwise tupe evidence.
Jamani siwote tunaomfahamu huyo Dada mwenye maelezo yakutosha atusaidie Jina peke yake halitoshi....
Queen ukijua kinachoendelea kuhusu huyu unaemtetea ungekaa kimya.
Asante
Funguka basi.
Mi simtetei mtu asiyelipa kodi sema kinachokera ni jinsi watu wanashangilia,fikiria eti mtu anasema afilisiwe,mradi hajaua mtu mi nadhani ingekua vizuri akaachiwa aendelee ma boashara zake halafu apewe muda wa kulipa hiyo kodi waliyokwepa.
Pia kufungiwa duka sio ushahidi kuwa hawalipi kodi,inaweza kuwa limefungwa kwa kutuhumiwa kutolipa kodi,then mahakama ndio itaamua kama mtuhumiwa ni mkwepa kodi au la.
Hata kama kweli walikwepa kodi,tusemw tu ukweli jamani ni nani mjanja hapa mjini hajawahi kupiga madili hasa wafanyabiashara?
Yeah acha tutumbuliwe ila leo furahia la Jestina,ila na wewe iko siku hata kama sio jipu,hata kipele lazima unacho na siku kikitumbuliwa pia ufurahie hivi hivi.