Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mie mshangazi ndio nasubiri mali zakoSasa chaputa mie nimefanyaje huko.
Alafu wee inaelekea ni mshangaz
Kooonyoo😆Nyokooook
😅😅😅😅Ulitaka akupe wewe mkuu?
May God bless your union sir! Mwenyezi Mungu akutunzie mama/dada yetu!Mimi nina 22yrs katika ndoa lakini alilofanya Jet Lee naweza kulifanya pasina shaka hata punje(japo sijafanya). Kuna type ya wanawake if you've lived with them through thick and thin unajua ni yapi hawawezi kuyafanya na ni yapi wanaweza though as the saying goes "never trust a woman" hivyo kazi kwenu wananzengo kusuka au kunyoa.
Njoo uchukue...daktari wangu kaniambia nina miaka 2 tuu ya kuishi so njoo haraka nikukabidhiMie mshangazi ndio nasubiri mali zako
Ila huyo ni wa Jet Li, Hawa wa kwetu sijui wamachame mara wapare ukae kwa akili zote.Vijana wa kiume msio na imani na kila mwanamke bado nyie hamjaona mengi na hamjui undani wa watu hao. Ni hivi wanawake wazuri na wenye utu ndani wapo tena wengi tuu. Dhana za kukaririshana kuwa wanawake wanapenda hela na ni wasaliti baada ya kupata pesa sio. Jichunguzeni hata wanaume pia wanapenda sana hela ila kwa kuzifanyia kazi. Na wapo wanaume ambao ukiwakabidhi hela kama za urithi hutawaona tena yaani wanatelekez kila kitu na hakuna cha maana watakachokifanya. Mke wa Jetli ni JetLi mwenyewe anajua kilichopo moyon mwa mwanamke huyo.
hapana huyo dada alstahili hicho unless lbda abadilike baadaye alikuwa ROYAL sana kwa jamaa na kihistoria alikuwa wametoka mbali sana na jamaa tangu enzi anajitafuta mpk kujipataOne man DOWN
Nakuja 💃💃💃Njoo uchukue...daktari wangu kaniambia nina miaka 2 tuu ya kuishi so njoo haraka nikukabidhi
Miaka yote hiyo anakimbilia wapi kama kasimama kutafuta kwa jina lako mpe hadhi inayostahili Big up Jet leeJe bibiye akikimbia itakuwaje!??
Wachina wana maadili sana na serikali itasaidia kusimamia mali.Mwigizaji Li Lianjie 'Jet Li' amewaacha mashabiki wake midomo wazi baada ya kufunguka kuwa amemkabidhi mke wake Nina Li Chi utajiri na fedha zake zote.
Mwigizaji huyo mwenye utajiri unaokadiliwa kuwa zaidi ya dola milioni 260, kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni ameweka wazi kuwa uamuzi huo haukutokana na matatizo yake ya kiafya ambapo anasumbuliwa na ugonjwa wa hyperthyroidism na matatizo ya mgongo bali ni kwa sababu anaimani kubwa kwa mkewe.
View attachment 3217800
"Upendo wake wa kwanza, anastahili zaidi. Kwa hakika, kwa miaka mingi, Nina amekuwa kitu kikubwa kuliko tu kuwa mpenzi wangu yeye ni mshauri, nguzo yangu ya nguvu. Alikuwa daima upande wangu, Li wakati nilipokuwa chini kabisa, alinisimamia. Anasimamia kila kitu ili niweze kuzingatia kazi yangu na afya yangu. Lolote lile, namwamini. Yeye ndiye sababu naweza kuwa ninavyokuwa leo."
Nina ambaye ni mke wa Li alitwaa taji la Miss Asia mwaka 1986, wawili hao walikutana na kuanzisha uhusiano mwaka 1988, aidha moja ya sababu inayomvutia Li kutoka kwa mkewe ni kumtii kuacha shughuli zake za urembo na kujikita zaidi kulea familia.
View attachment 3217801
Uaminifu huo wa Li kwa mkewe uliibua mijadara mbalimbali katika mtandao wa Twitter (X) mashabiki wakiwapongeza wawili hao kwa kuaminiani wakiandika "Hii si kuhusu pesa, somo la upendo ni kuhusu kuthamini mtu ambaye amekuwa upande wako kupitia kila kitu,".
Mkali huyo wa filamu za ngumi ambaye amewahi kuonekana kwenye Mulan, League of Gods, The Founding of a Republic, War na nyinginezo alifunga ndoa na Nina mwaka 1999 na wamebahatika kupata watoto wawili pamoja. Hata hivyo anadai kuwa hata akitaka kununua kitu chochote basi atamuomba mkewe pesa.
Baba yangu hakunisomesha international ili niwe mke wa nyumbani.Ni sahihi na ni dhahiri ni mwanamke mnyenyekevu na msikivu kabisa kwani sio rahisi hawa wa huku kwetu manzese kukusikiliza hata ufanyaje.Kwa ngazi aliyofikia huyo mwanamke kwenye urembo ingekuwa huku kwetu umambie aache kazi utajuta kwa majibu mabovu na ya jeuri atakayokupa.mf:-
"Yaani niache kazi yangu eti nikae nyumbani, hilo haliwezekani maisha yangu yote bora nisiolewe"
Ukosefu wa unyenyekevu na uaminifu unawakosesha wanawake wengi kufurahia maisha, wakibadilika unakuta jua limeshazama.