Vunjabei alishailipa Simba hela, kazi imebaki kwake kuzirudisha. Nadhani umekuwa mvivu tu wa kufuatilia mikataba. Ngoja nikukumbushe:
Mkataba wa Simba na Vunjabei ni kwamba Vunjabei ametoa 2B kwa Simba, atauza kwa bei yoyote na kwa wingi wowote, anabaki kuzitafuta kuzirudisha kwenye mauzo. Hii ni pre paid
Mkataba wa Yanga na GSM ni kwamba anatafuta kwanza wateja, atauza kwa bei yoyote na kwa wingi wowote, ila kila jezi ataipa Yanga sh. 1,300/=. Hii ni post paid
Wakati Simba hatawakuwa na haja ya kufuatilia Vunjabei ameuza jezi ngapi, Yanga wao inabidi wafuatilie GSM ameuza jezi ngapi ili asije akawapiga, maana kila jezi itakayouzwa wana vihela hapo