Jezi ya Yanga ni 'NZITO'

Jezi ya Yanga ni 'NZITO'

Ungekuwa unajua mambo hayo ungeisaidia chadema Yako kunusa harufu ya usaliti wa kina Bi mdee!!.
Kumbe usaliti una harufu.[emoji23].. Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi
 
Safari hii wachezaji wataota nundu migongoni. Siyo kazi nyepesi kucheza huku ukiwa na mzigo wa magofu ya misukule mgongoni na utando wa buibui .

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
[emoji3532]Jezi hawakaweka yale matundu ya kupitisha hewa

[emoji3532] Dizaini ya mashono ni ndogo sana na ya kulipua bora liende

[emoji3532] Collar za jezi za buibui na lile gazeti lenye sahihi kwa ni raundi kabisa na kwa mbali zinaonekana kama shanga za kike za kimasai

[emoji3532] Huyu mbunifu anajaza madude kwenye jezi kana kwamba kuna mtu anafuatilia kimeandikwa nini, waachane naye wamrudishe yule jamaa aliyekuwa kiongozi zamani alikuwa anabuni jezi za kimchezo bazo wachezaji na mashabiki wakivaa uwanjani wanaremba uwanja
Hata uwezo wa kushona chupi ya hawala yako huna unaongelea jezi za timu?
 
Yanga inaweza kuwa na msimu mbaya kuliko mingine yote katika historia yake tangu kuanzishwa kwakwe.. Nimetumia neno INAWEZA kwakuwa bado ina nafasi ya kufanya jambo

Rangi, maumbo na michoro kiroho huwakilisha vitu vikubwa sana.. Na in fact hesabu za kiroho ziko kwenye hayo mambo matatu..RANGI, MAUMBO NA MICHORO...!

Kwenye rangi sio ishu tena kwakuwa waliozichagua walishazipitisha na zikapata kibali cha kiroho... Rangi ya kijani inawakilisha uhai na ni rangi yenye nguvu sana kiroho.. Hata hiki chama cha ccm kinaishi mpaka leo hii kwa kudra za kiroho za rangi ya kijani.. Soma vitabu hivi kama rejea Green Traveller na The Hog!

Maumbo pia yana nguvu kubwa sana kiroho, na ndio maana watu huchukua muda mwingi kubuni ama kutumia umbo lenye uhai ama connection na roho.. Hapa sizungumzii uchawi na ushirikina vilabuni.. Ukitaka kujua nguvu ya maumbo tembelea majumba ya maonesho yenye maumbo na picha za vitu mbalimbali na ukae sehemu ya utulivu.. Hisia utakazopata ni tofauti kabisa na hisia utakazopata utakapoingia jumba lisilo na mapichapicha.. Hivi vitu huumba roho..

Michoro hasa yenye kuwakilisha vitu vyenye uhai hii ndio huwa hatari zaidi kama isipochaguliwa kwa umakini mkubwa.. Michoro ya maeneo, viumbe hai na chochote chenye kiasili na uhai imebeba maroho mazuri na mabaya

Kwa kutaka utofauti lakini bila kuzingatia mambo haya ya kiroho.. Timu ya Yanga msimu huu imekuja na jezi zilizoelemwa na michoro ya maeneo mbalimbali ya mji wa Dar na kwingineko na vitu vingjne pia vinavyowakilisha mpaka GPS nadhani[emoji3]..
Matokeo yake jezi kimwonekano inakuwa nyepesi lakini kiroho imelemewa mnoo

Ina picha ya askari monument pale Posta... Ni mnara unaowakilisha roho zilizokufa vitani
Kuna michoro ya uwanja wa fisi[emoji24]
Kuna maeneo mbalimbali ya makaburi
Kuna kila aina ya michoro yenye kukumbusha machungu na mambo ya kuumiza pia.. Haya yote yamekusanywa kwenye kitambaa kisichozidi mita moja

Ni maroho mangapi kwa pamoja yanabebwa na mchezaji mmoja kwa wakati mmoja.. Hapo achilia mbali na yale mahirizi .. Mwisho mchezaji anajikuta ni mwepesi wa kilo 60 lakini akicheza utadhani ana kilo 135 kamili..[emoji23]

Ni mtazamo tuu wa kiroho tusitupiane mawee
Mtani Uzito Wa Jersey ya Yanga Unakuhusu Nn? Unaivaa?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
zile jezi zinavaliwa tu kwa sababu ya mambo ya kiushabiki. Azam watengeneze kama zile uone kama hawajavaa timu na viongozi pekee
JamiiForums239619264.jpg
 
Mbunifu ni zero kabisa...duniani kote wabunifu wanatumia falsafa moja ya kwamba The beauty lies in its simplicity...ndio maana hata gari ukijaza maurembo linachukiza..sasa yeye anajua kurembesha ni kujaza makolokolo. Hawa wabunifu wa kinondoni wakasome
Hilo ndilo na mimi nilitaka kusema, ubunifu upo katika simplicity. Logo na hata jezi inabidi hata mtu wa kawaida tu aweze hata kuichora mwenyewe kwenye karatasi.

Sasa sisi wabunifu wetu ndiyo hawa. Ni kujazana ujinga tu kwenda mbele. Embu pitia uzi wangu mwingine ninaoiongelea CCM na YANGA.
 
Back
Top Bottom