Mashabiki wa soka wameamua kuishi kwenye kumbukumbu nzuri ya soka la zamani kabla ya mwaka 2010 lililokuwa na ushindani wa kweli. Soka la sasa limeharibiwa na pesa ya mafuta ya waarabu hakuna ushindani tena. Miaka hii akina Man U na R. Madrid wananyanyasika mbele ya Man City na PSG. Miaka hiyo huwezi kukuta huo upumbavu. Timu kama Ac Milan ya Kaka, Juve ya Del Piero, Roma ya Toti, Lazio ya Crespo, na Fiorentina ya Batistuta zilikua moto sana. Kule Spain kulikua na Valencia ya Mandieta, na Derpotivo la Coruna ya Diego Tristan. Ila sasa hivi hizo timu zimekua mdebwedo, wachezaji wazuri wote wanachukuliwa na timu zenye pesa ya mafuta hakuna ushindani tena.