Jezi zilizokamatwa sio feki ni michezo ya Kariakoo, Sandaland kazidiwa maarifa

Bila shaka hata ndege huwa unapanda private jet mashaallah
 
Bibi ana kiherehere halafu hakuna asilolijua yeye kila kitu anakijua , ovyo kweli huyo bibi na ana mdomo mchafu kama choo cha stendi
Basi miaka hiyo akijifanya anaishi Canada ilikuwa shida tupu.. Siku nilipokuja kumuumbua kwamba hayuko Canada yuko hapo Kariakoo alipotea jukwani wiki nzima [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mambo ya jf hayo wengine hawapo kwa sasa hahaaaaaa
 
GSM ajajikita kwenye biashara za nguo zaidi ya jezi za Yanga,GSM kaa uulize macartels wako wengi tena kubwa lao kabla ya ujio wa GSM alikua anashirikiana hadi na viongozi wa vilabu kutengeneza jezi fake,kuna msimu Yanga ilivaa jezi 8 na tracksuit juu,kama una kumbukumbu nzuri kuna match Yanga waliingia na tracksuit ikiwa joto kali,ujio wa GSM kwenye uwekezaji wa jezi umewaumiza waagizaji jezi fake kwa kiasi kikubwa,na baada ya GSM kuingia kwenye jezi hata simba nao wakashtuka wakamleta vunja bei japo nae alikua nyuma ya hao hao,labda huko kwenye shida zingine ila kwenye jezi fake GSM aihusiki hata chembe
 
Kumtaja mtu mwenye mzigo kama ule unatakiwa nawe uwe fit sana.. Kwakuwa utakuwa tayari umetangaza vita ya visasi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ni kweli kabisa Kkoo kuna umafia sana. Hata kwa mfano ukiwa na idea kali unataka uifanye halafu mtaji wako mdogo utashangazwa kuona ndani ya muda mfupi kuna wababe wameingiza mzigo kama wako makontena kadhaa na anauza bei karibu tu na uliyouziwa wewe China. Yaani automatically unaanza kuwa mteja wake. Kkoo kuna watu wana hela hadi kero. Kuna mama mmoja wa kikinga anauza masweta ya shule. Akiagiza samples ni 3000pcs wakati wajasiriamali wadogo wakiagiza 1000pcs jasho limewatoka. Kwenye mambo ya nguo kuna manyangumi hapo Kkoo.
 
Hizi ni biashara za watu wakubwa ndani ya serikali na chama dola. Usishangae kusikia majina ya watoto wa viongozi wakuu yakitajwatajwa
 
Hizi ni biashara za watu wakubwa ndani ya serikali na chama dola. Usishangae kusikia majina ya watoto wa viongozi wakuu yakitajwatajwa
Trust me hawatatajana.. Kinachofanyika sasa ni kusikilizia tuu.. Kama pressure ikizidi atatafutwa mbuzi wa kafara aswekwe ndani kwa 'makubaliano maalum' Kisha adhaminiwe..

Kesi ya vitenge iliishia wapi?
Kesi ya bomba la mafuta Kigamboni je?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi waziri wa michezo atuambie ni nani muhusika. Mbona kaa kimya pamoja na naibu wake Mwana FA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…