Jf-arusha wing...safari updates

Jf-arusha wing...safari updates

Cheusie darling, naomba kukuuliza na samahani kama nitakukwaza. Kuna ubaya gani wa kujitambulisha kuwa mimi ndo cheusi na jina langu halisi ni Victoria? Sisi wapwa, watu wa Darisalama JF members, tunafahamiana kwa ID zetu za JF, real names na sehemu tunazoishi na kufanyia kazi. Na hatujawahi kukwazika kwa lolote. Huwezi kuamini hata spouse zetu sasa wanafahamiana? Kwanini mnajificha? Whats a big deal? Nawashangaeni kwakweli.

Nlitangulia kuwaombeni samahani....

Christopher......nimeshukuru kukufahamu....mimi naomba nijitambulishe rasmi hata kabla ya safari......kwa jina naitwa Perpetua Sarwat Gwandu......ninaishi Yaeda....ni katibu muhtasi makao makuu ya Yaeda......jamani naomba nisiulizwe tena siku hiyo.....labda kama kuna mtu atakuwa anataka muhtasari wa maendelea ya Yaeda
 
babu hebu vaa mawani yako usome tena coment yangu,mtu B ameomba watu wasitaje ID zao,mimi nikasema hilo pia ni wazo zuri ili ambao hawapendi kufanya hivyo watajisikia huru kuja bila kuhofia kujulikana ID zao,nikasema lkn lisiwe sharti kwamba watu wote wasitaje ID ili wanaopenda kutaja id na majina yao halisi wafanye hivyo.Nikasema mimi binafsi sitaona shida kutaja ID yangu na jina langu halisi.

Kwenu huko labda ni sawa, lakini kwangu binafsi si sawa kabisa kwa sababu mimi hapa kwenye jukwa hili nimesema mambo yangu mengi ya ukweli kabisa nikijua sifahamiki kwa hiyo nikajisema mwenyewe kwa uhuru sana. Na naweza kusema nimefaidika na hali hiyo, yamenifaa sana majibu niliyokuwa napata hapa. Sa staki mtu ajue "ahaa kumbe yule jamaa ndiye huyu" etc, mambo ya kunijua sana undani sitaki.

Nimewaelewa wapendwa, nlitangulia kuwaomba radhi. Ila tu mi, ntakuwa hepi nikujua alaaaa, kumbe huyu ndo cheusie, kumbe ndo Victoria tena anafanya kazi eapoti....nna kabinti kangu kamesomea freight end fowading, hebu kafanyie mpamgo hapo. Urafiki, unaendelea, undugu unakua...watu wote semeni AMINA. Nawaleteeni asprin kabla hazijaeksipaya. Kuliko kuzitupa ni bora mzimeze hata kama hamna maumivu. Kwa faida yangu na vizazi vyangu vingi vijavyo.
 
Christopher......nimeshukuru kukufahamu....mimi naomba nijitambulishe rasmi hata kabla ya safari......kwa jina naitwa Perpetua Sarwat Gwandu......ninaishi Yaeda....ni katibu muhtasi makao makuu ya Yaeda......jamani naomba nisiulizwe tena siku hiyo.....labda kama kuna mtu atakuwa anataka muhtasari wa maendelea ya Yaeda

Perpetua endelea kupokea wageni ngoja nifatilie zile shanga za vibuyu terati.
 
Nikikutana na hili jina Gwandu huwa nacheka sanaaa. We acha bana.
 
Perpetua endelea kupokea wageni ngoja nifatilie zile shanga za vibuyu terati.

sawa......halafu mwambie Nasyeku akupe zile zile rangi tulichagua.....ana tabia ya kubadilisha sana yule
 
Wakuu msiniache, mi nimehamia kwa Mromboo kumechangamka mbaya! Weka mimi kwenye hiyo orosa tasafali!
Mkuu, nashukuru sana kuwa umeonekana hapa...Karibu sana, nadhani ushapewa namba ya kuwasiliana nayo, tafwazali mkuu wangu{Orobhaiyan}, tuwasiliane.
 
Kwa hiyo mmekonkludi nini sasa waungwana?
Mkuu, ni kwamba tarehe ya safari ni 27/12...kwa maana hiyo, inaTAKIWA MSAFIRI KUJA aRUSHA tAREHE 26/12, ILI TAREHE 27/12 TUDAMKE KUELEKEA ENEO LA TUKIO...Jumanne(14/12) tuna kikao cha kuweka mambo sawa, na ndipo tutakapowajulisheni maendeleo.
Mkuu, tunaitarajia sana squad ya Dar...Kama inawezekana mkuu, jaribu kutupa hesabu kamili ya watu watakaokuja, ili tujue aina ya usafiri utakaotumika.
Nakusikilizia mkuu wangu.
 
I wish to be there as i resides in monduli.
Kesho hadi tarehe 23/12 nitakuwa magugu.
Mandalizi yanaendaje.
Mkuu, nashukuru sana kwamba umeona hii maneno...Ni kwamba ishu hii inafanyika tarehe 27/12/ 2010..ndiyo siku ya safari, kuanzia alfajiri saa 12.00 asubuhi...
Kwahiyo mkuu hujachelewa hata kidogo, na karibu Sana...Kwa details zaidi ingia PM yako, kuna namna ya mawasiliano.
Tunakutegemea mkuu Shycase.
NASIKITIKA KUWA KWA BINAFSI YAKO ULIAMUA KUCHAGUA KUTOPOKEA PM YOYOTE TOKA KWA MWANAJF YEYOTE, NA HIVYO HATUNA JINSI YA KUKUPA UTARATIBU WA MAWASILIANO.
AKSANTE MKUU.
 
Naunga mkono hii initiative. Mtatupa feedback ya progress. Ngoja wadau wa DSM tuige mfano wenu.
 
jamani haya mabadiliko ya tarehe yanatishia uwezekano wa mimi kuhudhuria,ila vyovyote itakavyokuwa nitakuwa pamoja nanyi ktk maombi.
Cheusi, usianze kutufanya tupate heart attack!...Hivi unajua kwenye utu uzima haitakiwi kushitua wenzako eeh?...Acha utani bana,...nilishakwambia namba yako ya siti ni C3, na kwenye siti ya watu 3 wewe kushoto, Wiselady kulia, katikati MFAMAJI...
 
Naomba tukubaliane kuwa tutakapokutana ni marufuku kufichuana id zetu, maana nahisi kuna uwezekano wa kukutana na watu tunaofahamiana na sitaki yeyote ajue kuwa huyu ndiye Mtu B. Tukikutana tutumie majina halisi, hapo ndipo naona networking itakuwa imetusaidia kufahamiana. Nitajitambulisha jina halisi kwa wenzangu lakini sitasema kuwa mimi ndiye Mtu B. Naomba tuelewane hilo kwanza. Nina sababu zangu za msingi sana.
Mkuu, naomba ondoa shaka kabisa juu ya hilo...Ni kwamba ID hazitatumika kabisa...na hazina nafasi, hapa kilichopo ni kuwa pamoja na kupeana madili, siyo kujua PAKAJIMMY NI YUPI...Kabla hata ya hili wazo lako, tulipanga kutoa hilo kama angalizo namba moja, lakini pia Mkuu wa kaya MAXENCE alitoa ushauri huo kwa msisitizo sana akisema kuwa ID hazina kazi kwenye shughuli zetu..
Hivyo mkuu, we nitumie namba ya simu tu, na mambo mengine yatafuata kwa hekima sana.
 
Kwenu huko labda ni sawa, lakini kwangu binafsi si sawa kabisa kwa sababu mimi hapa kwenye jukwa hili nimesema mambo yangu mengi ya ukweli kabisa nikijua sifahamiki kwa hiyo nikajisema mwenyewe kwa uhuru sana. Na naweza kusema nimefaidika na hali hiyo, yamenifaa sana majibu niliyokuwa napata hapa. Sa staki mtu ajue "ahaa kumbe yule jamaa ndiye huyu" etc, mambo ya kunijua sana undani sitaki.
Mkuu, uko sAwa kabisa...Kwa kuongezea tu ni kwamba nadhani mtu ajisikie huru kwa binafsi yake kutaja au kutotaja ID yake, kutokAna na ANAVYOPIMA MWENYEWE MAHUSIANO YAKE NA JAMII..
Naomba nisiongelee tena jambo hili...
NAWASILISHA.
 
Back
Top Bottom