Mtumishi Wetu
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 5,712
- 1,910
UPDATE 2:Wana-JF wa Arusha,
Wababa :Enda-Subhai!
Wamama :Endakwenya!
Wote :Subhati Ngerai, habari-ya-Ngaji?..Engai Engoitoi!...poleni sana!
Wapendwa,
Nia yangu si ubaguzi wa Makabila au maeneo, lakini kama mjuavyo, Maasai ndio mila/kabila PEKEE linalojaribu kushindana na kasi ya mabadiliko yaliyoasisiwa na ujio wa wageni nchini!
Nia ya post hii ni kuwajulisha wana-JF wa Arusha na maeneo ya jirani kwamba kuelekea mwisho wa mwaka 2010 tuna Mpango Kabambe wa kuasisi mijumuiko ya kijamii, ambapo kwa kufanya hivyo tutakuwa tunatekeleza kwa vitendo upiganiaji haki wetu, ambao kwa bahati mbaya umekuwa kimabandiko-zaidi kuliko uhalisia..Charity begins home...na tuanze sisi wenyewe kuonyesha kwamba mambo haya yanaweza kubadilishwa na kutendewa kazi ya kuonekana kwa macho...lets go substantial!
Jana (9/12/2010-Uhuru wa Tanganyika) wana-JF kama 5 wa hapa Arusha, tukiwa na m-JF mgeni toka Dar tulikutana mahali kwaajili ya kufahamiana na kubadilishana mawazo, tukagundua kwamba ni jambo jema sana kukaa pamoja na kuongea, na hatimaye tukaona umuhimu wa kufanya kitu cha kirafiki.
Tuliazimia kuwa tu'organize safari ya kutembelea mbuga yoyote ya wanyama iliyoko pande za huku kama ambavyo tutakubaliana, kabla ya Krismas, yaani kati ya tarehe 15-23/12/2010...
Tumegundua kuwa Arusha kuna members wengi sana(huenda kuliko Dar:grouphug🙂...!
Kwa members wote mtakaokuwa interested, tafadhali aidha onyesheni kwenye bandiko hili, au nitumieni PM, ili pamoja na mengine tufanye kikao cha awali cha logistics.
NB:
Members wa nchi nzima mtakaokuwa Arusha/Moshi kwaajili ya X-MAS au LIKIZO au vyovyote mnakaribishwa sana ili tuungane pamoja!
Ngongo.. Rutashubanyuma, na wengineo, tunahitaji sana inputs zenu!
UPDATE 1:
Mkuu Maxence Melo atahudhuria kwenye hii safari, na ameomba kuwa na maongezi na members wa Arusha, na hata kujibu maswali mbalimbali kuhusu Jf na mengineyo.
Tarehe imebadilishwa(kwa convinience ya Melo na wanaJF wengine toka Dar, imekuwa 27/12/2010, badala ya 23/12.
Kutakuwa na kikao cha Maandalizi Siku ya Jumanne, tarehe 14/12/2010, saa 11.00 kamili jioni...tumeweka muda huo kuwawezesha wanaotoka makazini waweze kuhudhuria.
Venue itatolewa kwa wale waliowasilisha namba zao kwa pioneers wa mpango huu, hivyo jitahidi kutuma namba yako kwenye namba iliyokuPM kwaajili ya suala hili.
UPDATE 3
Jana (14/12/2010)tulifanikiwa kuanzisha kikao(pilot-meeting), ambacho kilifanikiwa sana..Kwa ujumla ni kwamba tulitengeneza skeleton yote ya safari nzima, na matukio ya baada ya safari.
Tume'schedule kikao kingine kufanyika IJUMAA,17/12/2010, SAME VENUE, SAME TIME(0500PM)....
WITO WANGU KWA WALE AMBAO WAMEKOSA KIKAO CHA MWANZO, NAWAOMBA MSIKOSE KIKAO KIJACHO, ni muhimu sana, na ni burudani!
Baada ya kikao hicho cha Ijumaa tutatoa taarifa rasmi na FINAL kwa Umma wa JF juu ya taratibu za ushiriki(Mkono mtupu haurambwi).
Aksanteni tena.
UPDATE 4:
Maamuzi ya kikao cha jana ni kama ifuatavyo:
1.Safari itakuwa na awamu 2 ndani ya siku 1,ambapo ni(a)Kwenda Mbugani(b)Kikao na Mkuu Maxence..kwa maana hiyo kuwasili(wa mbali)ni 26/12, na safari 27/12.
2. Bajeti iliyoandaliwa inainclude Usafiri, Chakula, Vinywaji,(cold-drinks) na Viingilio getini.
Lakini pia baada ya kurudi Arusha, kuna gharama za Ukumbi-wa kukutania kwa Maongezi na Mkuu, Barbeque ya uhakika na Vinywaji, na zawadi ya Sungura kwa Mkuu, (tumesikia anapenda sana kufuga)!
3.Kwa bajeti hiyo, kila atayeungana nasi atachangia ths 50,000/=tu kama gharama ya kucover vitu hivyo vyote.
4.Kuna members ambao wako pamoja na sisi, tarehe hizo watakuwa na majukumu, lakini watachangia ili kuonyesha mshikamano.
5.Michango yote itumwe kwa M-PESA kwa namba 0762-320630.
6.Deadline ya michango hii ni tarehe 24/12/2010
7.Mliopo nje ya Arusha, tafadhali wahisheni contributions ili tuweke mambo sawa.
8.Eneo la kikao cha Maongezi baada ya Safari linahifadhiwa kwa sababu za Usalama.
5.Hali ya uthibitisho wa members mpaka leo iko hivi:
Waliothibitisha kusafiri na kuchanga.
1.Preta
2.Mzee wa Rula
3.Mr.Miela
4.Crashwise
5.Mtumishi Wetu
6.EekaMangi
7.Derimto
8.Wiselady
9.PakaJimmy
10.Hmethod
11.Lilyflower
12.Chipukizi.
Watakaochangia,lakini hawana ukakika kupata nafasi ya kusafiri:
13.Loner
14.Gerald2008
Ambao bado hawajathibitisha
15.Bucho
16.Baba Ubaya
17.Kings01
18.Msindima
19.Margwe
20.Mzee wa Serengeti
21.Ndallo
22.Ntavyo
23.Samora
24.Vince
25.Ngongo.[/QUOTE]
Ndugu yangu PJ,
Kweli umefanya kazi kubwa kuweza kutukutanisha group yote ya Arusha JF members, aksante kwa kazi nzuri, ubarikiwe. Kweli kivyangu nilifurahi ingawa niliondoka mapema maana ninakaa mbali kidogo na mji with no reliable transport.
Lakini kiukweli nilifurahi saana kukutana na wadau wa JF LIVE. Mlivyo amua ni sawa tutajitahidi kushiriki.
Best Regards.