JF bado ina watu wema. Ndugu Kalaga Baho ni miongoni mwao.

JF bado ina watu wema. Ndugu Kalaga Baho ni miongoni mwao.

Siku hizi mitandaoni hata JF kumekuwa na posts na comments nyingi sana za chuki. Single Mama na waalimu wamekuwa wahanga wakuu wa hizi chuki. Pamoja na wingi wa watu wenye roho mbaya ila bado wapo wachache wema. Kuna watu wako tayari kukusaidia bila kukujua wala kutaka chochote kitu kutoka kwako.

Kwa mamlaka niliyojipa nimeamua kumtambua ndugu Kalaga Baho Nongwa kuwa ni mtu mwema anayependa kuona watu wanapiga hatua. Kupitia uzi wake wa machimbo ya Kkoo nimepata contacts ambazo zimenisaidia kuokoa hadi 20% ya bajeti yangu. Machimbo anayotoa Kalaga Baho ni ya ukweli kabisa. Kikubwa hata watu wake anaowa-recommend ni waaminifu na wanatoa huduma iliyonyooka kama rula. MUNGU MBARIKI KALAGA BAHO... AMEN. Tuige mfano wake.

Ninatambua pia uwepo wa watu wema wengine kama Lucas Mwashambwa & Ephen, bibi Faiza, Tlaatlaah, USSR, Magonjwa mtambuka, bia yetu.
Safi kabisa hapo juu. Ila hapo chini naona utachafua hali ya hewa.
 
Uzi umenajisiwa na machawa wa ccm uliowataja.

Huyu master namkubali sana asee . alito code za viatu hivi karibuni nikaipenyesha kwa msela angu anajihusisha na biashara za hizo akakuta vilevile. huyu jamaangu yeye hatumii huu mtandao anasema mgumu mno

mkuu pojkea maua yako@Kalaga Baho Nongwa
Nayapokea mkuu shukrani
 
Kalaga Baho Nongwa naomba chimbo ya hizi mali
49CA008C-68ED-4E54-87D8-BD7A823F52E0.jpeg
 
mkuu kalaga baho. Chimbo la chupi, tait za kike zile za kuvaliwa na wanajamii wa uchumi wa chini. Naomba code mkuu
 
Back
Top Bottom