Mzalendo anatiririka katika lugha ya mabeberu ili kutia ushawishi na kufikia malengo ya nchi nyonge. Lugha ni nyenzo mojawapo ya soft power ambayo awamu ya tano ya CCM imeshindwa kuitumia kwa kisingizio cha 'uzalendo wa kweli'
Wakati tukipitia video mbalimbali tunaona wazalendo wa kweli wa enzi hizo walitumia soft power hiyo vizuri kuelezea mapungufu ya sera za kibeberu, ukoloni mamboleo na unyonyaji kiasi waliweza kushawishi wananchi wa nchi beberu kubadili sera zao kwa manufaa ya nchi nyonge ziluzokuwa huru au zile zilizokuwa bado zikipambana na ukoloni mkongwe na ubaguzi wa rangi.
Hakika nimejifunza hawa wazee wetu walijua jinsi ya kuwaingia mataifa makubwa kwa ushawishi wa hoja kupitia soft power yaani lugha kubwa za kigeni wakati huohuo wakikitukuza Kiswahili.
Viongozi wetu wa sasa wanajificha nyuma ya 'uzalendo' huku wakikosa ushawishi na nguvu ya hoja kimataifa kwa manufaa ya nchi.
Mikutano mingi inafanyika Tanzania mfano SADC kikao cha 38 mwaka 2019 Tanzania imepewa uwenyekiti , Nordic Africa Summit 2019 na Asia Africa consultative Summit 2019 iliyofanyika Dar es Salaam Tanzania lakini ukiingia YouTube, magazine za kimataifa n.k hakuna archive /hazina / kumbukumbu yoyote kuipaisha na kuitangaza Tanzania. Tatizo kuu ni Lugha.
Mabalozi wa Tanzania wajitokeze kukubali kuhojiwa ktk lugha ya kigeni popote walipo nje na ndani ya Tanzania.
Source: AP archive