Vyombo vingi vya habari vya nje vilielezea ajali na kifo chake kwamba aliuawa.
TANZANIAN PREMIER IS KILLED
13/4/1984
TANZANIAN PREMIER IS KILLED; WAS LEADER'S HEIR APPARENT TANZANIAN PREMIER IS KILLED; WAS LEADER'S HEIR APPARENT?
Reuters
Hizi siasa za Afrika ni siasa mbaya sana na ndizo zimepoteza viongozi wengi wazuri na ambao kama wangeendelea kuwepo, basi baadhi ya nchi nyingi za Afrika ikiwepo Tanzania zingekuwa mbali kimaendeleo.
Hayati Mwalimu alianza kuzungumzia kustaafu siasa tangu katikati ya 1980 na hapo ndipo mapigano ndani ya
corridors of power yalipoanza.
Kwa kwa mtizamo wangu ni kwamba hayati Sokoine huenda alitumia hiyo vita ya wahujumu uchumi kutaka kujijenga kisiasa na hivyo kusababisha mtafaruku ndani ya CCM ambamo kuna wanasiasa wengine walitamani kuwa maraisi.
Hivyo kufikia mwaka 1983 kuna viongozi kadhaa waandamizi ambao walianza kutajwa na miongoni mwao alikuwemo hayati Sokoine, hayati Rashid Kawawa na Aboud Jumbe Mwinyi, Cleopa Msuya na mzee wetu Salim Ahmed Salim.
Kumbuka Sokoine alifariki akiwa mdogo sana at 46 na hao wazee walikuwa mbele yakle kisiasa na kiuzoefu.
Kuna kitabu chaitwa
The Dark Side of Nyerere Legacy ambacho kimeandikwa na Ludovick Mwijage na anaeleza mengi.
Ila naunga mkono juhudi za hayati Sokoine katika kuhakikisha kwamba hakuna wahujumu uchumi na walanguzi wa bidhaa kwa wakti ule.
Hivyo hata sasa tukiona kiongozi anapambana na nguvu nyingi za fedha na bidhaa kufichwa na kisha baadae akaja hadharani kubainisha majaribu juu ya I=uahi wake basi wapata fursa nzuri ya kuwaelewa wale wote wasoitakia mema nchi yetu.
Nina mengi sana ya kuyaeleza lakini naomba niishie hapo.