JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

..hata nyinyi mnaosifia mnatoa sifa za jumla-jumla ktk masuala ambayo ni complicated.
Huna sababu yoyote ya kutuiga sisi. Onyesha mfano ili nasi tujifunze toka kwako.

Lakini usisahau kwamba, mjadala huu uliuanza wewe, kwa bandiko lako ambalo ni hisia tu ulizokuwa nazo.
 
Mzee Mwanakijij

Thanks MMM kwa clip. Ninatoka nje kdg ya mada sorry.

Kama hii ilikuwa ni mwaka 1978 ina maana alikuwa na miaka 40 akiwa waziri mkuu kwani alizaliwa 1938 na he looks young kbs. Imezuka tabia siku hizi ya vibwagizo kama "waziri kijana" sijui imetoka wapi hii mm sifahamu.

Marehemu Sokoine alikuwa PM akiwa na miaka chini ya 40 na Baba wa Taifa Mwal Nyerere alikuwa PM pia tena mkuu wa nchi 1961 tulipopata uhuru akiwa na miaka 39 sasa wewe una miaka 45 unajiita waziri kijana ili iweje na ujana upi huo?

Matokeo yake kuna viongozi wanatufanyia mambo ya ajabu ajabu tu simply eti kwa sababu wao ni mawaziri vijana what a hell ujana upi huo so special na kuna watu wakiwa chini ya umri wako waliongoza nchi hii na hawakuwa na huo ujinga?.
 
Huna sababu yoyote ya kutuiga sisi. Onyesha mfano ili nasi tujifunze toka kwako.

Lakini usisahau kwamba, mjadala huu uliuanza wewe, kwa bandiko lako ambalo ni hisia tu ulizokuwa nazo.

..wewe unataka kuninyanyasa tu.

..nilisema sheria ya uhujumu uchumi ilipitishwa baada ya "watuhumiwa" kuwekwa kizuizini.

..kweli, au siyo kweli?

..nilisema baada ya Sokoine kuongoza zoezi la kukamata wahujumu uchumi na walanguzi, bado uchumi wetu ulibaki umedorora, na bidhaa hazikuonekana madukani.

..kweli, au siyo kweli?

..nilisema Marehemu Sokoine anastahili kuenziwa kama Waziri Mkuu aliyeongoza wakati wa vita.

..Je, anastahili, au hastahili?

..Mimi nasifia pale alipofanya vizuri, na nakosoa alipokosea. Na kwa maoni yangu alikosea ktk kile kilichoitwa vita dhidi ya wahujumu uchumi na walanguzi.
 
Nimeona ameshuka kutoka kwenye Mercedes Benz made in Germany baba wa Capitalism.

Usiamini communist hata siku moja, Stalin na Mao waliuwa watu zaidi milioni 100 kueneza communism, Mwalimu Nyerere alikuwa anatibiwa London na siyo Soviet Union au China!

Was JKN a communist? I don't think so....alikuwa mjamaa
 
Nashauri wizara ya habari na utamaduni itenge bajeti ya kudigitize old videos na old audios zote za viongozi muhimu na pia za historia muhimu ya taifa tangu enzi za ukoloni.

Na hizo digitized videos na audios ziwe stored TBC au na pia makumbusho ya Taifa au na pia National Library au na pia UDSM Library.

Na ziwe available to the public for free au at a small price.

Nadhani kuna technology ya kudigitize old videos na old audios.

Wanaweza pia kuomba mashirika mbali mbali ya habari na maktaba mbali mbali za dunia wawape hizo old videos na old audios.

Hii ita saidia sana katika kuhifadhi kumbu kumbu sahihi ya historia ya Tanzania.

Pia itasaidia sana kwenye mambo ya utafiti, pamoja na kwenye mambo ya kuandika historia ya viongozi.

Hansard zote za bunge tangu uhuru (na LEGCO ya enzi za ukoloni) nazo ziwe digitized. Pamoja na maadhimio yote muhimu ya TANU, na CCM (enzi zile za chama kimoja).
 
"Quality" nadra sana kuwa nazo viongozi wengi.
Kassim Majaliwa, anajitahidi sana katika mazingira magumu

Mkuu Chakaza, umetoa 'ushuhuda' kama wa 'walokole', ila wao huweka chumvi nyingi. Pongezi kwako na heshima mkuu.

Cheki wanavyojipendekeza wazee wetu wa sasa, je viongozi wa namna hii wanaweza kutoa ushauri unaopingana na mkuu wao kwa ajili ya kumsaidia nchi isiteketee kijamii, kisiasa, kiuchumi na kisera?

15 Nov 2019
MAJALIWA Atokwa MACHOZI MAGUFULI Alivyomwaga MAMILION

Cheki wanavyojipendekeza wazee wetu wa sasa, je viongozi wa namna hii wanaweza kutoa ushauri unaopingana na mkuu wao kwa ajili ya kumsaidia nchi isiteketee kijamii, kisiasa, kiuchumi na kisera?

Kwanini unafikiria ni kwa sababu anajipendekeza na siyo wajibu wake kupitisha ujumbe huo?
 
Mkuu operation zinduka ndio ilikuaje?
Flashback miaka 4!
Baada ya Mbowe "kuuza chama", watu wenye akilizao wakafyatuka na kuamua kuelimisha watanzania kupitia "OZ". Kama hukupata nafasi ya kusikiliza, summary yake ni kwamba....Kwa waliozoea janjajanja-economy, "CHADEMA ya Lowassa ni afadhali kuliko CCM ya Magufuli..."
Fast track miaka minne mbele, tunawashuhudia humu wakilia na kusaga meno.. anyways ukipata muda pitia..hii ni moja ya operesheni muhimu sana kwenye historia ya nchiyetu...ingependeza ingeandikiwa kitabu sambamba na "My Life, My Purpose"

Screenshot_20191117-015007.jpeg
 
BTW msingi wa kuitwa daladala ulikuwa hivi: Shillingi tano za Kitanzania zilikuwa sawa na dola moja ya marekani na pound sterling 1 wakati huo tulikuwa tunabadili kwa shillingi 7 (saba). Hivyo mabasi hayo kuitwa daladala.
No, dola moja ilikuwa ni shilingi tano ndiyo asili ya sh tano kuitwa dala (dolar). Wakati huo nauli ilikuwa ni sh 5 ambayo ni dola moja! So nauli ni dola dola ( dala dala) hapo ndiyo asili ya jina dala dala! Kuhusu paundi ni kwamba paundi moja ilikuwa ni tsh 20 ndiyo maana sh. 20 ilikuwa inaitwa paundi
 
National Achives ya Video enzi hizo ilikuwa kwenye film rolls ikifanywa na Taasisi ya Vielelezo, Audio-Visual Institute pale ilipo TBC Kijitonyama.
By the time wanaziunganisha kuunda TVT, ile 1998, film rolls ilikuwa tayari fazed out. Hivyo zile digital zote tunazoziona za sherehe za uhuru, ni kwa hisani ya foreign achievers.

Shirika la Habari la China, Xinua linazo lots of our early events katika digital achievers zao na pia Cuba wanazo.

Issue ni TBC kuziomba tuu.
P
Dr Rioba nazani atakua amesoma hapa
 
Sawa, leta ukweli wewe kwenye hilo? Kwa nini mabasi hayo yaliitwa daladala? Nipo 110% right.
Ulipokosea ni kwamba hujaeleza msingi halisia japo ulikuwa unakuja kwenye ukweli.

Nakusaidia kuweka usahihi; nikwamba utingo/makonda walipokuwa wakiwaita abiria walikuwa wanatamka 'panda gari dola dola moja' matokeo yake neno doladola likaanza kupata hathari za kimatamshi nakuzaa daladala.

Sawa na neno 'chenji' unamwambia konda hapo zamani nirudishie 'chenji' yangu, lkn kwasasa utasikia vijana wa Daresalama wanasema 'chenchi' hizo ni athari za kimatamshi ambao hutokea pale wazungumzaji wa lugha mbili ama lugha mbili zinapo gongana katika matumizi ndani ya eneo moja.

Sawa na neno 'want' huko Marekani ya zamani wenyewe waliita 'NEW WORLD' mzungu wa Kiingereza akiwa katika shamba angeweza kumwagiza mwafrika asiyekuwa anajua Kimombo huko Marekani ya zamani mfano 'tell him that I want ten sacks' Mwafrika anarudia kama alivyoagizwa na mzungu lkn anajikuta anasema 'wan sakisi' muda ulivyokuwa unazidi pakazaliwa neno 'wanna'.

Kwa wajuvi wa lugha ya kikoloni wanahita 'Pidginization' ambayo huzaa pidgin ambayo wakizaliwa watoto nakuanza kutumia maneno 'daladala, chenchi,wanna etc' katika matumizi ya kawaida na wakidhani yako sahihi basi hii lugha huitwa Creole.

Mfano wa hizi Creoles ni Gurah huko Marekani ya kusini, Jamaican, Guiyana, Topksin huko Seoraleon n.k.

Neno Marekani lenyewe ni Creole kwani limetokana na athari za kimatamshi kutokana na ujina(nomino/noun) wa neno 'American' yaani Amerikani ... merikani..Marekani.
 
Cheki wanavyojipendekeza wazee wetu wa sasa, je viongozi wa namna hii wanaweza kutoa ushauri unaopingana na mkuu wao kwa ajili ya kumsaidia nchi isiteketee kijamii, kisiasa, kiuchumi na kisera?

15 Nov 2019
MAJALIWA Atokwa MACHOZI MAGUFULI Alivyomwaga MAMILION

Hii ni ibada na si vinginevyo ni bahati sana kwamba tumefika hapa.
 
National Achives ya Video enzi hizo ilikuwa kwenye film rolls ikifanywa na Taasisi ya Vielelezo, Audio-Visual Institute pale ilipo TBC Kijitonyama.
By the time wanaziunganisha kuunda TVT, ile 1998, film rolls ilikuwa tayari fazed out. Hivyo zile digital zote tunazoziona za sherehe za uhuru, ni kwa hisani ya foreign achievers.

Shirika la Habari la China, Xinua linazo lots of our early events katika digital achievers zao na pia Cuba wanazo.

Issue ni TBC kuziomba tuu.
Pascal mayalla ur are very bright brother, huwa nasoma sana post zako JF ur are very geneous bro. u come with all facts no one can compete with you, one day natamani tuonane mkuu nijifunze upendo na busara zako mkuu..
 
kwa wr
Ulipokosea ni kwamba hujaeleza msingi halisia japo ulikuwa unakuja kwenye ukweli.

Nakusaidia kuweka usahihi; nikwamba utingo/makonda walipokuwa wakiwaita abiria walikuwa wanatamka 'panda gari dola dola moja' matokeo yake neno doladola likaanza kupata hathari za kimatamshi nakuzaa daladala.

Sawa na neno 'chenji' unamwambia konda hapo zamani nirudishie 'chenji' yangu, lkn kwasasa utasikia vijana wa Daresalama wanasema 'chenchi' hizo ni athari za kimatamshi ambao hutokea pale wazungumzaji wa lugha mbili ama lugha mbili zinapo gongana katika matumizi ndani ya eneo moja.

Sawa na neno 'want' huko Marekani ya zamani wenyewe waliita 'NEW WORLD' mzungu wa Kiingereza akiwa katika shamba angeweza kumwagiza mwafrika asiyekuwa anajua Kimombo huko Marekani ya zamani mfano 'tell him that I want ten sacks' Mwafrika anarudia kama alivyoagizwa na mzungu lkn anajikuta anasema 'wan sakisi' muda ulivyokuwa unazidi pakazaliwa neno 'wanna'.

Kwa wajuvi wa lugha ya kikoloni wanahita 'Pidginization' ambayo huzaa pidgin ambayo wakizaliwa watoto nakuanza kutumia maneno 'daladala, chenchi,wanna etc' katika matumizi ya kawaida na wakidhani yako sahihi basi hii lugha huitwa Creole.

Mfano wa hizi Creoles ni Gurah huko Marekani ya kusini, Jamaican, Guiyana, Topksin huko Seoraleon n.k.

Neno Marekani lenyewe ni Creole kwani limetokana na athari za kimatamshi kutokana na ujina(nomino/noun) wa neno 'American' yaani Amerikani ... merikani..Marekani.
kwa WARAKA huu hapa Olle atakuwa hana cha kusema
 
Asante MMK kwa hii kitu. Lakini naona Sokoine hakuwa Mzalendo maana alutoa hotuba yake kwa lugha ya mabeberu!
 
Back
Top Bottom