JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

Mzalendo anatiririka katika lugha ya mabeberu ili kutia ushawishi na kufikia malengo ya nchi nyonge. Lugha ni nyenzo mojawapo ya soft power ambayo awamu ya tano ya CCM imeshindwa kuitumia kwa kisingizio cha 'uzalendo wa kweli'

Wakati tukipitia video mbalimbali tunaona wazalendo wa kweli wa enzi hizo walitumia soft power hiyo vizuri kuelezea mapungufu ya sera za kibeberu, ukoloni mamboleo na unyonyaji kiasi waliweza kushawishi wananchi wa nchi beberu kubadili sera zao kwa manufaa ya nchi nyonge ziluzokuwa huru au zile zilizokuwa bado zikipambana na ukoloni mkongwe na ubaguzi wa rangi.

Hakika nimejifunza hawa wazee wetu walijua jinsi ya kuwaingia mataifa makubwa kwa ushawishi wa hoja kupitia soft power yaani lugha kubwa za kigeni wakati huohuo wakikitukuza Kiswahili.

Viongozi wetu wa sasa wanajificha nyuma ya 'uzalendo' huku wakikosa ushawishi na nguvu ya hoja kimataifa kwa manufaa ya nchi.

Mikutano mingi inafanyika Tanzania mfano SADC kikao cha 38 mwaka 2019 Tanzania imepewa uwenyekiti , Nordic Africa Summit 2019 na Asia Africa consultative Summit 2019 iliyofanyika Dar es Salaam Tanzania lakini ukiingia YouTube, magazine za kimataifa n.k hakuna archive /hazina / kumbukumbu yoyote kuipaisha na kuitangaza Tanzania. Tatizo kuu ni Lugha.

Mabalozi wa Tanzania wajitokeze kukubali kuhojiwa ktk lugha ya kigeni popote walipo nje na ndani ya Tanzania.

Source: AP archive
 
23 Jul 2015
(18 Jan 1976) Tanzanian President Julius Nyerere at a press conference in Delhi where he says why his country supports the Popular Movement for the Liberation of Angola.
Source: AP Archive
 
14 Oct 2019
United Republic of Tanzania Minister of Foreign Affairs H.E. Palamagamba Kabudi highlights the importance of financial inclusion, including the country's National Financial Inclusion Strategy, during the special event “Financial Inclusion for Development: Building on 10 Years of Progress” at the 74th UN General Assembly in New York City on 25 September 2019.
Source: UNSGSA
 
Wakati wa kukomunika ukifika nilikuwa naona ufahari sana kusimama pembeni yake.

Angemfuatia Nyerere 1985 hii nchi isingeshuhudia mambo ya EPA escrow na upuuzi mwingine.
 

Ishu ya sauti kunani kwani? Sijui ni kasimu kangu au sijui ni kitu gani.....

Picha zinaonekana vizuri na sauti yako wewe mleta mada inasikika vizuri tu, lakini sauti ya Moringe Sokoine menyewe Hanna kitu zaidi ya kuona midomo inachezacheza tu!!!
 
Hilo la kushindwa kuendesha uchumi ni analysis nyepesi sana kwa suala very complicated. Linahitaji mjadala unaojitegemea. Hukuwatendea haki hao magwiji wa uongozi.
 
Hilo la kushindwa kuendesha uchumi ni analysis nyepesi sana kwa suala very complicated. Linahitaji mjadala unaojitegemea. Hukuwatendea haki hao magwiji wa uongozi.

Hawezi kwa sababu ya unafiki tu. wakati wa miaka ile baada ya J K Nyerere kuonyesha kwamba asingegombea tena 1985 Sokoine was unchallenged kutokana na aliyokuwa anafanya. Baada ya kufariki SAS ndiye angechukua, lakini unafahamu what happened.
 
Du! aisee hiyo Sauti hapo imenikumbusha Operesheni Zinduka!
Nevertheless, Edward Moringe Sokoine was a no nonsense PM. Continue Resting in Peace huku ukishuhudia muendelezo wa fikra na matamanio yako kupitia Rais Magufuli
Mkuu operation zinduka ndio ilikuaje?
 
Ile sarafu yenye makonakona yenye thamani ya shilingi tano, ilipewa tu jina la 'daladala.' Hiyo haikuwa na maana kwamba sarafu hiyo ilikuwa na thamani ya dola 1 kwa wakati huo. Dola moja ilikuwa sawa na shilingi 7.
Tuweke historia sawa hapa. Kwanza tujue hiyo coin ya shilingi tano ilianza kutumika tarehe 9/12/1971 kama kusherehekea miaka 10 ya Uhuru wa Tanganyika.
Wakati huo official rate ya dola kwa shilingi ilikuwa dola moja sawa na shilingi tano. Uki google mitandaoni inaonyesha sawa na shilingi around 7. Lakini officially kwa serikali ya TZ ilikuwa sawa na shilingi tano.

Pia hiyo shilingi tano ilikuwa na muonekano sawa na dola tano.
Hicho ndio chanzo cha hiyo shilingi tano kuitwa dala.
Mwaka 1983 kulipotokea matatizo ya usafiri Dar. Sokoine akaruhusu mabasi ya watu binafsi yatumike. Wakati huo kama sikosei nauli ya UDA na Kamata kwa usafiri wa Dar ilikuwa sh. Tatu. Magari binafsi wakawa wanaiba kwa shilingi tano.
Huo ndio ukawa mwanzo wa hizo basi kuitwa dala dala. Yaani nauli yao ilikuwa shilingi tano.
 
Mkuu Ole, ngoja nikuache tu mkuu, kwa sababu naona haya yatakuwa majibishano yasiyokuwa na msingi. Wewe unaandika meengi yasiyokuwa na uthibitisho wowote.
Uliahidi kuleta 'exchange rates' hapa, sizioni.

Unaweka habari ya kuumizwa Ndugu Sokoine isiyokuwa na mwanzo wala mwisho, na unataka tuamini tu!

Kiufupi hujatoa habari yoyote ya kuonyesha unafahamu chochote kuhusu hayo unayoandika juu yake.
 
"...alionea 'wananchi' kwa sababu alisimamia zoezi la kuwakamata na kuwaweka kizuizini..." umetumia neno 'alionea' kwa maana kwamba hapakuwa na sababu ya kuwakamata hao wananchi? "Ulanguzi" haikuwa sababu, na hasa ukichukulia wakati husika na taifa likikabiliwa na hali ngumu ya kivita?

Na wakati unasema hapa kwamba "Mzee Mwinyi aliondoa tatizo la ulanguzi wa bidhaa bila kulazimika..." Hapa nina hakika huna maana ya kwamba Mzee Mwinyi aliruhusu "UHUJUMU" au sio? huoni kwamba wakati uliruhusu kufanya hivyo? Vita ilikwishapita, kwa hiyo ilikuwa ni sawa kuliweka taifa katika hali tofauti. Na bado huoni kwamba hata kodi zilikuwa hazikusanywi ipasavyo! Hiyo ndio ilikuwa sawa?

"Sokoine alifanya kazi kubwa.wakati wa vita.." Kazi gani, ambayo inafanya makosa aliyofanya huko kabla ya vita yaendelee kumwondolea sifa? Huoni kwamba msimamo wake kabla ya vita, wakati wa vita na baada ya vita, yote kwa pamoja ndio yanayofanya aonekane kuwa mzalendo wa kweli kwa taifa lake?

Sidhani kuwa mtu ambaye hakuwepo wakati wa Sokoine, ataelewa kwa kuambiwa tu 'Sokoine alifanya kazi kubwa wakati wa vita.'

Vita zidi ya uhujumu ujumi haikulenga kumkomoa mtu. Hali ya maisha ya wananchi wote ilikuwa ni ngumu.

Wakati taifa linapokuwa linakabiliwa na hali ngumu, halafu ukawaonea aibu watu wanaohujumu juhudi zinazofanywa ili taifa liondoke kwenye hali ngumu, sijui faida ya kufanya hizo juhudi za kuondokana na hali ngumu.
 
Reactions: Ole
Pia hiyo shilingi tano ilikuwa na muonekano sawa na dola tano.
Mkuu huenda hili la mfanano wa muenekano wa kiumbo kati ya sarafu ya TZS 5 na USD5 ndio jibu sahihi.
Lakini taarifa rasmi za kihistoria toka vyanzo mbalimbali Dola 1 ya Marekani haijawahi kuwa sawa na Shilingi tano ya Tanzania tangu Tanganyika ipate uhuru.

Hiyo Official record ya serikali tunaomba utuambie reference tunapata wapi? Hata kama ni BOT tutafuatilia kuthibitsha.
 

Sawa, lakini swali langu la kwanza hukujibu, maana ndio tabia yako nilikwambia wakati huo mimi nilikuwa Dar wewe hata hukusema ulikuwa wapi? Pengine ulikuwa hujazaliwa then unataka kujifanya mjuaji na kuwaanisha watu kwamba lipo jambo ambalo unalielewa. Nimekupa hata jina la Mwandishi wa habari wa Waziri mkuu wakati ule, what else can you expect. Nitakwenda kwenye maktaba yangu nifukue baadhi ya magazeti ambayo ni kumbu kumbu inshallah nikipata nitaweka humu.
 

Uko sawa Mgosi.

Mkate ulikuwa ni shilingi 4

Soda zilikuwa ni shilingi 6

Na basi la ikarus (leo twayaita mwendo kasi) nauli ilikuwa senti 30 au thumni mimi nilikuwa nikipanda kituo cha Faya kwenda mjini posta ya zamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…