JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

Hivi kulikuwa na uhujumu uchumi au sera mbovu na mitazamo hasi ya kijamaa ndiyo iliyopelekea watawala wetu kuwaona matajiri wanahujumu uchumi ?

Mimi sijawahi kulielewa hili suala la uhujumu uchumi ulikuwa ni uporaji wa kidola tu na wala haukuwa na msaada wowote kwa wananchi badala ya kuzalisha mateso na ufukara.

Watu wanamsifia Sokoine kwa kupora Mali za watanzania ambao walizipata kwa uhalali no wonder hata sasa kuna uporaji wa kidola na unyanyasaji unaitwa vita ya kiuchumi while in fact ni matokeo ya sera mbovu tu za watawala wetu.
 
Siku hizi unarukia rukia tu mambo, umeshamaliza suala la uchaguzi wa serikali za mtaa. Uliandika mada utafikiri mtu asiyejua wala hajawai kufika Tanzania.
 
Hawa watu wengine wanasifia tu hata wasiyoyajua. Uchumi wa Kenya umeshikiliwa na watu wachache sana.

Walichofanikiwa Kenya kwa kiasi kikubwa ni elimu. Hili ndilo litakalowanyanyua haraka mbeleni.

Tunaposema elimu tuna maana gani? Isije ikawa ni lugha ya kiingereza.
 

Nafikiri ni vizuri kwanza watu waelewe maana ya kuhujumu uchumi. Kuwa na pesa nyingi sio msingi wa wewe kuwa muhujumu uchumi. Mfano huyu raia wa Somalia aliyekiri kwamba aliikoseshea TRA 8 billion na amekubali kuilipa pamoja na kuwataja washirika wake.

 

Bagamoyo
Binadamu tumetofautiana, emotions kila mtu inampata kwa nafsi yake. Wewe huwezi kum-judge kwa kutoa machozi kwa sababu kila binadamu yupo tofauti na wewe/mwingine, huwezi kuelewa Waziri Mkuu anafahamu siri nyingi sana za Serikali kuliko wewe na mimi, vile vile kwa nini alitoa machozi. Utakuwa humtendei haki Waziri Mkuu Majaliwa.
 

Scandavia wamemix ujamaa na ubepari kwa maana uchumi umeshikwa na private sector kinachotakiwa uchumi ushikwe na private sector ili wakatwe kodi kubwa ambao utumiwa na serikali kuwasaidia masikini
 

Kuwa na ardhi kubwa isiyo na tija ni matumizi mabaya.Ardhi wapewe wenye kuzalisha ili wazalishe kuchochea ongezeko la uchumi na kupunguza tatizo la ajira nchin
 
Sijui kwanini TBC hawajaamua kudigitize collection yao ya videos za mambo mbalimbali ya enzi na enzi...




Mayalla, Mwanakijiji, Nyani, etc.. mnaishi kwenye utopia...

Hata ma nchi ambayo yana television ya taifa toka enzi za mitume hupati archive footage kirahisi rahisi mitandaoni, kwenye youtube, etc.. etc...

Juzi baada ya Mkapa kujitetea kwenye kitabu chake eti alikuwa hajazoea maswali magumu ya HardTalk mwaka 2001 kwenye mauaji ya Wapemba, nilirudi kutafuta ile footage (ambayo nilishaiona) nikatuta BBC wameshaindoa! Haipatikani!

Hivi vitu vina haki miliki kali! Kwa hiyo Mwanakijiji na Mayalla mnaposema wange digitize film rolls zao, wange digitize halafu iweje, wazisambaze bure Youtube?

Zanzibar walikuwa na national TV, mbona hatujawahi kuona speech ya Karume mwanzo mwisho hata moja ?? Mbona hatujawahi kuona video footage ya kusaini Muungano? Ina maana kweli ZBC na RTD hawaku cover Muungano???

Radio Tanzania wana rekodi zote za audio, si ndio ? Mbona hatuzisikii? Paskali, Mwanakijiji, mkinatafutia hii spichi hapa (RTD walikuwepo siku ile viwanja vya Mnazi Mmoja, microphone inasema RTD) nitauza shamba langu la Kilombero nikulipeni mamilioni yeyote yatakayopatikana...



Rais anamzodoa Waziri (aliyepigwa pini katikati ya polisi) ambae kaletwa uwanjani kutoka rumande Ukonga, kutoka hapa akaenda kuuliwa, shtaka lake limetamkwa kwenye bango nyuma ya Rais: KIBARAKA... Nilikuwa sijazaliwa lakini nataka kusikia matusi na reasoning capacity na hukumu za majukwani za BABA WA TAIFA, kama je, ni kama hizi hizi za kileo?
 

Mkuu Bu'yaka

Alikuwa Waziri gani huyo? Na mwaka kama unakumbua.
 
Mkuu Bu'yaka, hapa tunazungumza vitu viwili tofauti, Mzee Mwanakijiji ametaka TBC wa digitize video zao za zamani for easy accessibility, wewe unazungumzia copy rights as if zipo ila ziko restricted.

Mwaka juzi katika kusherehea miaka 50 ya reli ya Tazara, Wachina wameipa TBC hundreds of video footages za Mwalimu, na ujenzi wa Taraza, lila milestones zimekuwa properly video documented.

Kwenye issues za public events, video zake ni public documents, hazina sababu ya kuwa na copy rights restrictions. Hata hivyo kwenye digital world, kuna jinsi ya ku protect kidigitali, mfano kwa DSTV, unaweza kurekodi kila kitu kwenye format ya Full HD kupitia DSTV explora kwa kutumia PVR, hicho unachorekodi unaweza ku playback hata mara 100 lakini huwezi kukirekodi ukapata Full HD quality. Hivyo issue ya copyright sidhani kama ni issue, issue huku kwetu ni uwepo wa hizo video. Pale TBC kuna mamia ya rolls za 16mm films ambazo kuwa digitized ni issue.

P
 
Mkuu Bu'yaka

Alikuwa Waziri gani huyo? Na mwaka kama unakumbua.

WAZIRI MWANDAMIZI!

Wakati wanatiliana saini ya kuunda nchi yeye ndie alikuwa shahidi namba moja, alikaa katikati kushikilia makaratasi yasipeperuke!



Alitiwa kizuizini, akaletwa kuzodolewa Mnazi Mmoja, akarudishwa kizuizini, akaenda kuuliwa. Spichi ile ya BABA WA TAIFA ya kubainisha mashtaka yake, na hukumu yake, na adhabu yake ndio naitafuta.
 
Hata kabla ya kifo chake, ndege iliyotakiwa kumrudisha Dar es Salaam kutoka Dodoma ilichelewa, basi akasema hakuna shida nitakwenda Dar kwa gari, hapo ndipo alipokutana na mauti kule Morogoro (Dumila).


Hakupata ajali Dumila, alipata ajali Dakawa eneo linaloitwa Wami Sokoine kwa sasa
 


Bado urasimu upo mpaka leo katika dunia ya dijitali!!?

Nini kinasubiriwa kuwabandua hao wanaoendekeza huo urasimu?

Urasimu huo unaweza kuwa chanzo cha kupotea kwa utanzania halisi kwakuwa kizazi kipya hakijui wala hakiwezi kujifunza mambo mengi yaliyofanywa na Mw. Nyerere na hata Sokoine, binafsi naona tunayo nafasi kurejesha elements za uzalendo kwa nchi yetu kwa kuweka vipindi vingi kabisa vya hao wawili.
 
Kwanini usiseme ni Hanga badala ya kufanya kama watoto wanaocheza Kombolela?
 
Mkuu Phillipo, na bila kuwepo mambo ya EPA CCM ingekuwa historia kama KANU au UNIP.
Nadhani hapo tuko pamoja sio?
Suala sio pesa..suala ni mikakati..mlichukua 12bn kutoka kwa Edwadi...Slaa akauliza..tunachukua Asset au Liability?? Mkagunaguna mala mkauchunaa...matokeoyake ni historia
 
Reactions: Ole
Hakupata ajali Dumila, alipata ajali Dakawa eneo linaloitwa Wami Sokoine kwa sasa
Dumila na Dakawa kuna umbali wa maili kama 22 ukiangalia google maps. Wami Sokoine ni jina jipya kutokana na ajali ile. My recollection ndio hizo na wakati ule hakukuwa na lami. Barabara ya lami haikupita baadhi ya sehemu kwa hiyo siwezi kubishana kwa hilo. Kwa hiyo alipata ajali Wami Sokoine.
 
Kwenye issues za public events, video zake ni public documents, hazina sababu ya kuwa na copy rights restrictions.

there is no such thing as public documents for public events

Paskali, ukibeba kakamera kako ka gulioni, ukaenda kwenye mkutano wa wazi wa Chama Cha TADEA ukawapiga video ukaondoka, hiyo ni mali yako milele!

Na kama kamera ilikuwa ni ya TBC, footage ni mali ya TBC milele!

Na kama ulikuwa uko kwenye masaa ya kazi ya Clouds Media lakini umebeba kamera mbili, yako na yao, hiyo ni mali ya Clouds Media milele, they don't care which camera you used!

You should know this better than anybody...

Ndio maana walikuwa wanamlaani Issa Michuzi, wakati ule wa shamba la bibi, awamu ya Kikwete, anachukua archive picha za kazini Daily News na Maelezo anapeleka Michuzi Blog, mali binafsi, sidhani kama bado anafanya vile vi ujanja ujanja any more... angeshafungwa Segerea

Hivi vitu vina haki miliki! Huwezi kuvikuta youtube bure bure!
 
Fungueni uzi wa Waziri Hanga sasa. Hanga na muungano 1964 Sokoine 1980's wapi na wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…