King _Of_Everything
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 695
- 1,354
Ngoja nikubadilishie swali madam maana naona unalikwepa mnoo hili neno Gaidi, Hawa Al-Shaabab wanajinasibu kwamba wao wanapigania kuanzisha Taifa la Kiislamu litakalo ongozwa na Sheria za Kiislamu na hata katika eneo wanaloshikilia Nchini Somalia wanatawala kwa Sharia, Hakuna watoto kwenda Shule ni Madrassa tu, Je wewe kama mwenye Ufahamu wa kutosha juu ya DINI hii unadhani wako sahihi ama wnakosea? Je kwako wewe hii ni JIHAD?Ndiyo hao ninaosema mimi. Gaidi kwa mmoja mpigania Uhuru kwa mwengine.
Ukiwasoma boko haram wanasema wao wanapigania haki lakini ukiwasoma wanaowapinga wanaweka hawa ni magaidi.
Ukiwasoma Alshaabab wansema wao wanipigania Somalia kwa kuvamiwa na majeshi ya nje. Lakini wengine wanasema ni magaidi.
Hayo hayakuanza leo wala jana. Ndiyo maana nikakupa mfano wa Mandela.
Ukipitia mitandaoni na kutaka kujifunza, utakuta kuna Red Brigades Walikuwa Italy, nao ni hivyo hivyo.
Utakuta kule Ireland utawasoma kina Sinn Vein na kundi lake la IRA nao waliitwa magaidi.
Hakuna dini yenye amani kama Uislam. Uislam ungekuwa na ugaidi hapa Tanzania kungekuwa hakuna dini nyingine kwani Uislam ulikuwepo hapa zaidi ya miaka 1000 kabla ya Ukristo.