JF Hard Talk "FaizaFoxy"

JF Hard Talk "FaizaFoxy"

Kwa sababu ndivyo media inavyokuaminisha na wewe bila kufikiri unakubali tu, hata ukweli unapodhihiri wewe kwa kuwa umeshajazwa ujinga (brain washed) wewe huuamini tena wewe upo kwenye ujinga uliojazwa nao.

Mfano hai. USA imeishambulia Iraq na kuuwa zaidi ya watu million mbili, watoto wadogo pekee zaidi ya million moja kwa kisingizio kuwa kuna silaha za maangamizi. Ulikuwa ni uongo tu. Hao siyo magaidi? Gaidi atakuwa Muiraq aliyeuliwa watoto zake anapojitetea! Au sivyo hivyo?

Ndiyo maana nnawaambia kwanini hamuusomi Uislam bila hiyana? Soma: QuranIndex.Net

Mambo ya nchi za watu maybe i am brainwashed media maybe kuna wakristo wanajilipua na kuua mamia ya watu wasio na hatia ila media zinaniaminisha kua ni waislamu boko haraka waliteka wasichana 300 na kuwaua wengine kuwasilimisha maybe ni wakrsito pia just media zinani brain wash achana na ya juzi kenya
Acha niongelee mambo ya hapa nchini ishu ya mbagala ubishani wa watoto wawili wadogo kuhusu msahafu kumgeuza mtu chura ukiukojolea baada ya yule mtoto kuukojolea watu wazima wakaamka na hasira kali kuanza kuchoma makanisa sidhan kama biblia ingekojolewa tungeinuka kuchoma misikiti kwa sababu sisi tunahubiri amani
Hilo pia hao watoto sikuwaona kwa macho labda media ziliwapaka paka
Niloliona kwa macho kibiti high school waislamu walichoma moto shule baada ya vijana wachache kwenda kutumia vyombo vyao vya kulia chakula kuwekea nyama wanadai ya nguruwe na ushahidi kukosekana wa kuwafukuza hao vijana shule
Waislamu wakaamua kuchoma moto shule?
Je ni sahihi kwa kosa la vijana wachache ambao ushahidi wake si rahisi kupatikana kuamua kuchoma shule??


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hilo ni kweli kabisa. Ilifikia mpaka Waislam kupunguziwa points zao wakati Ndalichako alipokuwa mkuu wa mitihani. Waislam mpaka wakaingia mitaani kuandamana mpaka Ndalichako akaachia ngazi.

Magufuli alipoingia madarakani akatuzaba Waislam kofi la kikelb kwa kumrudisha wizara hiyohiyo na kumfanya Ndalichako awe waziri wa elimu. Hatari.
Unaushahidi gani kuwa walikuwa wanapunguziwa point?? na kama una ushahidi mliwahi kwenda mahakamani ??
 
Sasa kaka si ameahakujibu pale juu. Mbona unarudisha mambo nyuma? Amesema uislam haufundishi mtu kuwa gaidi na ili kuekewa zaidi akakupa nyuzi ya kuifuata ili upate ufunuo zaidi. Sasa tena unarudisha kule kule. Ohooo

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo anataka ajibiwe kama alivyoaminishwa,anaona anajibiwa tofauti ndio maana anaonekana kama vile hakubaliani na jibu alilopewa.
 
nafahamu maana ya madrasa ni kufundishwa elimu ya kislam sasa nyinyi mmeegemea huko, elimu ya shuleni mnaona ya kikafiri mkifeli mnamsingizia ndalichako,wanaopasua wanapasua wanaofeli wanafeli na mpaka leo huko wanapoendekeza madrasa tu kama pemba na unguja maziro yanazidi kuongezeka
 
1) Heshima kubwa ya uzee anayo, angekuwa Muislam ningemuita Sheikh Nyerere, Sheikh kwa maana ya uzee wake.

2) Ningemshauri afanye flat tax rate ya 10% across.

3) Tanzania hakuna "wapinzani" kuna wapingaji, ndicho kinachowapa taabu hicho.

4) Al shabab kwa maana ya ugaidi, ntalaani vikali sana.

5) Siwafahamu hao ndugu zenu waliokimbilia Msumbiji na sifahamu hizo "hatua walizochukuliwa".
Asante Madame

Namaanisha lile sakata LA kibiti na zile operations zilizofanywa kimya kimya hata wakakimbilia Msumbiji..

~ukipata nafasi ya kukutana na kumshauri CAG Asad...utampa mawaidha gani.!?

~je wale magaidi wa juzi Kenya,waliovamia na kuua watu kisha kuuwawa hotelini...(wanapewa bikira 72 huko peponi.??)

~na unaweza kutoa sehemu ya kipato chako kufadhili/kusaidia harakati za Alshaabab.??



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwetu Kisiju, wazee walikuwa na mashamba hapo jirani ya Kisiju, Shungubweni - Mkuranga, ndipo ninapoishi sasa, nimezaliwa na kusoma shule za awali Dar Es Salaam.
Je unafahamiana na Mzee Mohamed Said huyu wa humu JF, Ahsante
 
Naomba mwaliko wako hata siku moja ya mwezi mtukufu nije kufuturu maana imani zinafanana ndugu yangu #inshaalah panapo uzima
Kwetu Kisiju, wazee walikuwa na mashamba hapo jirani ya Kisiju, Shungubweni - Mkuranga, ndipo ninapoishi sasa, nimezaliwa na kusoma shule za awali Dar Es Salaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1) Heshima kubwa ya uzee anayo, angekuwa Muislam ningemuita Sheikh Nyerere, Sheikh kwa maana ya uzee wake. Kwa Tanzania nikimuita Sheikh sintoeleweka.

2) Ningemshauri afanye flat tax rate ya 10% across.

3) Tanzania hakuna "wapinzani" kuna wapingaji, ndicho kinachowapa taabu hicho.

4) Al shabab kwa maana ya ugaidi, ntalaani vikali sana.

5) Siwafahamu hao ndugu zenu waliokimbilia Msumbiji na sifahamu hizo "hatua walizochukuliwa".
Hapo namba 3 umenichanganya.

Hebu explain nini hasa maana upinzani na nini kazi ya upinzani ktk nchi !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa huo upunguani. Nimekwepa nini na nimekujibu kwa muono wangu? Au kuna majibu ulishayapanga ujibiwe? Si ungenambia tu, swali hili nataka jibu hili.

Sharia haimkatazi mtu kupata elimu yeyote ile. Nadhani hafahamu kuwa hakuna dini iliyosisitiza kusoma kama Uislam. Aya ya kwanza ya Qur'an kushushwa ni "Soma".

Hivi " madrasa" unaoisikia unafikiri nini zaidi? Unajuwa kuwa neno "madarasa" la Kiswahili limetokana na hilo "madrasa"? Limit ya masomo ya madrasa ni Mwalimu au waalimu tu wanaofundishwa. Hakuna somo lisilofundishwa madrasa. Kumbuka hilo.

Neno "shule" ukienda Somalia hawalifahamu hilo, labda huyo Msomali ajuwe Kiswahili au Kijerumani kwani neno hilo limetokana na Kijerumani.

Nnaamini mtu ukiwa mjinga ndiyo unakubali kila unaloambiwa bila hata ya kufikiri au kuuliza.

Nakupongeza sana wewe kwa kuuliza kwani unaonesha unayosikia hayakuingii akilini. Hiyo ni akili nzuri.
Hahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jihad ni kama Kiswahili tu juhudi. Kila tulifanyalo tunatakiwa tulifanye kwa juhudi.

Binafsi sijaona mahali katika Uislam kumefundisha kuwa jihad ni "kupigania dini". Kupigana katika Uislam ni kwa kujihami tu.

Nimewahi kusikia kuwa "crusade" maana yake ni vita vya msalaba. Kweli?
Dahh Una akili sana .. wewe mama kusoma comments zako ni darasa tosha .. napenda jinsi ambavyo ulivyo na uwezo mkubwa sana wakujibu na kujenga HOJA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyewe umekiri "wanapusua tu", huko "kupasua" kwao ndiko kulimfanya Ndalichako awapunguze speed.

Laiti ungefahamu maana ya madrasa ungetamani hata leo hii ukasome huko.
Sema hapo
Screenshot_20190124-134501.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je Jamii Forum kwako unaweza kuifananisha na sehemu gani nyumbani kwako, Sebureni kwako, Jikoni kwako, Chumbani kwako, Kibarazani kwako, Jalalani/Dust Bin ama Msalani? Na kwanini ?
 
Back
Top Bottom