Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Mnajidanganya. Endelea kupitia uzi nimeelezea kwa kina kuhusu ndoa ya Kiislam. Hakuna kuoa au kuolewa Kiislam. Ni kuoana. Mahari ni "symbolic" inaweza kuwa hata aya ya Qur'an tu na si lazima iwe cha kuliwa kama ulivyodai.
Na mahari Kiislam inaweza ikarudi atapokuwacha mke. (Unafahamu kuwa mwanamke anaweza kukuwacha kisheria ya Kiislam?) Fikiri.
Auntie Faiza, Mahari katika ndoa ya kiislamu ni kitu cha lazima iwe chochote lakini ni lazima na hii ni kulingana na Kauli ya mtume mtukufu (saw).
Kuolewa ni kitendo cha msichana au mwanamke kupokea posa, kupokea Mahari na kisha kufunga ndoa chini ya mzazi au wakili wake na kisha kuchukuliwa kwenda kuishi kwa mumewe--- hapo anakua kaolewa na mume anakuwa kaoa kwa kutekeleza hayo masharti niliyoyataja kwa ufupi.
Kuoa na kuolewa ni ndoa kati ya watu wa jinsia tofauti. Lakini KUOANA ni ndoa kati ya watu wa jinsia moja (mashoga), na ndiyo maana ukiwakuta mashoga kama ni wanaume kila mmoja utasikia akimtaja mwenziwe eti "MY HUSBAND" na ukiwakuta mashoga wa kike (Lesbians) utasikia kila mmoja akimwita mwenzake eti,"MY WIFE"😁😁.
Kwahiyo unapozungumzia juu ya kuoana unazungumzia juu ya ndoa za mashoga.
Katika Lugha ya kiarabu neno kuoa ni يتزوج (yatazauji) na neno kuolewa ni تتزوج (tatazauji) kuonesha utofauti kati ya jinsia mbili, na kiarabu ndiyo mama wa lugha zote za dunia.
Auntie Faiza tafakari sana hili jambo, mimi hivi sasa nilitaka kuja kuoa mke wa pili huko Mkuranga kwa hali hiyo ya KUOANA sasa naogopa kuja kuoa😁😁😁.