Jf Hard Talk "Mwifwa"

Jf Hard Talk "Mwifwa"

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Kama kawaida ya kikaango kutoka JF hapa tunamkaanga member mmoja kila siku maswali ya kistaarabu na majibu ya kiprofessional Zaidi.

Kwa leo tutakuwa na Ndugu yetu Mwifwa kama guest,uliza swali lolote unalotaka kujua kutoka kwake na taaluma yake kwa ujumla.

Nb;
Tafadhari zingatia kutumia Lugha ya kistaarabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nauliza.
1. Unazungumziaje maswala ya utandawazi na vijana

2. Matokeo ya form yametangazwa je ufaulu umepanda ama umeshuka ukizingatia unajumlisha na waliopata division 4 ambayo haitamsaidia mtahiniwa.

3. Kila kukicha maswala ya mahusiano yawe ya ndoa ama BF na GF yanachangamoto uvumilivu umepungua nini maoni yako na mtazamo wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kujua
-elimu yake
Degree 1
-mahusiano yake (kwenye ndoa au single)
Single
Afya
-anaishi wap (mkoa)
Pwani
-yeye ni MTU wa namna gani?
Mimi ni kijana wa kawaida sana, sio kama mnavyofikiria hapa JF, mwembamba lakini sio sana, mrefu wa kawaida, mweupe, mpenda utani, mkimya(hapa kabla hatukazoeana ndio nakuwa hivi, ila ukinizoea utakoma kwa utani[emoji3][emoji3][emoji3])
NB:naomba nijibiwe kiswahili (kiingereza sikimudu)

Bila shaka nitakuwa nimekujibu.
 
Degree 1SingleAfyaPwaniMimi ni kijana wa kawaida sana, sio kama mnavyofikiria hapa JF, mwembamba lakini sio sana, mrefu wa kawaida, mweupe, mpenda utani, mkimya(hapa kabla hatukazoeana ndio nakuwa hivi, ila ukinizoea utakoma kwa utani[emoji3][emoji3][emoji3])

Bila shaka nitakuwa nimekujibu.

Asante mkuu majibu yako mazur

Naona umekazia (mweupe,mrefu,mwembamba kiasi)😂😂🙆
 
Nauliza.
1. Unazungumziaje maswala ya utandawazi na vijana
Kila kitu kina pande 2(zuri na baya)

Utandawazi una faida kubwa sana kwa vijana ukitumika vizuri, mambo mengi yamekuwa rahisi kutokana na utandawazi ikiwemo namna na njia za kujikwamua kwa kutafuta pesa.

Pia utandawazi umekuwa janga kubwa kwa vijana maana unawalemaza katika kujibidisha na mambo yenye tija badala yake wanataka kutumia njia ya mkato kwa kivuli cha utandawazi mwishowe wanashindwa kufanikiwa ipasavyo.

Siku hizi vijana wanajiingiza kutafuta pesa kwa urahisi hasa kutumia mitandao(japo ikitumika vizuri unatoka pia) na kuacha fursa zingine lukuki mtaani ikiwemo ujasiriamali ama biashara au kilimo(japo kuna changamoto pia)

Janga kubwa la utandawazi ni mdororo wa maadili kwa vijana(hili kila mtu ni shahidi)
2. Matokeo ya form yametangazwa je ufaulu umepanda ama umeshuka ukizingatia unajumlisha na waliopata division 4 ambayo haitamsaidia mtahiniwa.
Kwa mujibu wa NECTA, ufaulu umepanda(maana wao ndio wenye takwimu zaidi ya mimi) japo kuna wenye four na zero kabisa maana kila mwaka huwa zinakuwepo
3. Kila kukicha maswala ya mahusiano yawe ya ndoa ama BF na GF yanachangamoto uvumilivu umepungua nini maoni yako na mtazamo wako.

Mimi naamini hizi nguzo za mahusiano na ndio nazitumia kwenye mahusiano yangu.
1. Uaminifu
2. Upendo kwa dhati
3. Ukweli

ukizingatia hivyo 3 mahusiano yatakuwa mazuri sana.
 
Back
Top Bottom