Mwifwa
JF-Expert Member
- Apr 3, 2017
- 48,474
- 125,866
Yote yana maanisha jinsia ya kike.Ningelipenda kufahamu unaelewaje? ama unatofautishaje:-
-Msichana
-Binti
-Mwanamke
Lakini yanatumika kuelezea au kuwakilisha hadhi fulani ya jinsia ya kike.
Msichana:
Hili hutumika sana nyanja za elimu kutambua jinsia ya kike.
Pia hutumiwa sana na jamii kuwakilisha umri wa ujana wa jinsia ya kike(mtanisamehe maana sina uhakika na hili jibu).
Binti:
Hutumiwa sana na wazazi kutaja mtoto wao wa jinsi ya kike.
Mwanamke:
Hutumiwa sana kuwakilisha jinsia ya kike katika umri wa utu uzima.(japo mtoto akifikia balehe anakuwa katika umri wa utu uzima, kulingana na definition ya kubalehe ya Sayansi ya Shule ya msingi)
NB: Hapo ni kulingana na uelewa wangu