Jf Hard Talk "Mwifwa"

Jf Hard Talk "Mwifwa"

Mwifwa ni jina la wapi au lina uhusiano gani na wewe mpaka ukaamua kujiita humu JF
Lina maanisha ''Mpwa" kwa lugha ya kabila langu
La pili yasemekana pwani ni mkoa wenye viwanda vingi vipya vilivyojengwa na Jpm, Je, umewahi kuvishuhudia?
Sijawahi kuvishuhudia na kama vipo labda sehemu zingine sio mahala ninapoishi mimi
Habari ya siku nyingi mkuu
Kwema kabisa mkuu.

Mungu ni mwema!
 
Mwifwa taaluma ya Afya ni pana sana...hongera kwa hilo.
Je...umesomea Afya sababu ya FURSA au ni MAPENZI uliokuwa nayo kitambo?
Nilipokuwa O-level nilitamani niwe Mhandisi maana nilipenda nikasome PCM A-level.

Uwezo wangu kwenye masomo ulikuwa wa kawaida.

Wakati wa hatua za mwisho kumaliza mtihani wa NECTA form 4, tulipoanza kujaza comb na shule za Advance ambazo tutachagualiwa tukifaulu.

Nilianza kwa kuchagua comb ya PCB kwa kuchagua Ilboru kama chaguo la kwanza, lengo likiwa nikichaguliwa hiyo shule kwa comb ya PCB, baadae nikabadili niende PCM(maana nilifanya utafiti mdogo nikagundua unaweza kuwa na ufaulu wa One ya kawaida na unaweza kuchaguliwa shule kubwa kama Ilboru, Mzumbe, Kibaha, Tabora Boys kwa PCB)

Lakini mambo yakawa tofauti, nilichaguliwa shule nyingine ambayo sikuitarajia japo niliichagua kwa comb nyingine.

Wakati naenda kuanza Alevel nikaambiwa nibaki PCB maana nitasoma mambo ya Afya nikifika chuo endapo nitafaulu, basi hadi hapo nikabaki na PCB na nikakomaa kufanya juhudi za kufaulu(nilisota sana) hadi nikafanikiwa na nikafanikiwa pia kusoma mambo ya Afya.

Bila shaka nitakuwa nimekujibu.
 
Mkuu kulingana na taaluma yako ni ipi iliochangamoto kubwa unayopitia uwapo katika majukumu yako ya kikazi.

Ahsante.
 
Swali jingine

Ukipewa nafasi kama mdau Wa Jf nini ungependa kibadilishwe
Ningewashirikisha wana JF kutoa maoni kuhusu hilo jambo maana wao ndio wanaitambua kwa matumizi zaidi.

Halafu ndio ningechambua maoni kadhaa ya muhimu zaidi nikiwa na timu yangu ya JF na kuyafanyia kazi.

NB: Kuhusu privacy ningeongeza juhudi zaidi(japo za sasa zipo vizuri pia) maana siku ya jana au ya leo haiwezi kufanana na ya kesho
 
Ni Vitu Gani unaviangalia ukitaka kuingia kwenye mahusiano??
Kwa kuwa nishaingia kwenge mahusiano.

Nilitumia umakini sana kuingia kwenye mahusiano.

1. Niliweka nguvu nyingi na maarifa kwenye kumdadisi niliyetaka kuingia naye kwenye mahusiano.
2. Nilitumia lugha ya upole kwa hali ya juu sana.
3. Nilikuwa na subira sana huku nikiongeza juhudi kwenye kudadisi kama atanifaa au la.
4. Hatimaye aliingia kwenye 18 kiulani.

NB: Kwenye udadisi nilitumia sana kuulizana maswali, kujadili mada kwa pamoja, maswali yalijikita sana kwenye nyanja zote. Lakini mimi nilichunguza sana kuhusu ishu za kifamilia/ndoa. Huo mchakato wote umefanyika kwa njia za SMS na SMS zote zipo hadi sasa hivi na huwa tunajikumbusha halafu anabaki kuniambia ''ulihangaika sana"[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Ningewashirikisha wana JF kutoa maoni kuhusu hilo jambo maana wao ndio wanaitambua kwa matumizi zaidi.

Halafu ndio ningechambua maoni kadhaa ya muhimu zaidi nikiwa na timu yangu ya JF na kuyafanyia kazi.

NB: Kuhusu privacy ningeongeza juhudi zaidi(japo za sasa zipo vizuri pia) maana siku ya jana au ya leo haiwezi kufanana na ya kesho
ukikutana na Rais JPM utamwambia nini?

Unajiskiaje wanafunzi wanaochaguliwa Muhas toka mwaka 2015 kukosa mikopo kwa wingi sana?
 
Siku za hivi karibuni kumetokea wimbi la wafanyakazi wa huduma za afya (Madaktari na Wasaidizi) kuwapima wagonjwa baadhi ya magonjwa bila idhini ya mhusika, hili suala unalizungumziaje?
Kwa maadili ya Afya lazima pawepo na ruhusa ya mgonjwa au ndugu(kwa wagonjwa ambao hawajitambui au watoto)

Bila idhini ni kosa.
 
Nilipokuwa O-level nilitamani niwe Mhandisi maana nilipenda nikasome PCM A-level.

Uwezo wangu kwenye masomo ulikuwa wa kawaida.

Wakati wa hatua za mwisho kumaliza mtihani wa NECTA form 4, tulipoanza kujaza comb na shule za Advance ambazo tutachagualiwa tukifaulu.

Nilianza kwa kuchagua comb ya PCB kwa kuchagua Ilboru kama chaguo la kwanza, lengo likiwa nikichaguliwa hiyo shule kwa comb ya PCB, baadae nikabadili niende PCM(maana nilifanya utafiti mdogo nikagundua unaweza kuwa na ufaulu wa One ya kawaida na unaweza kuchaguliwa shule kubwa kama Ilboru, Mzumbe, Kibaha, Tabora Boys kwa PCB)

Lakini mambo yakawa tofauti, nilichaguliwa shule nyingine ambayo sikuitarajia japo niliichagua kwa comb nyingine.

Wakati naenda kuanza Alevel nikaambiwa nibaki PCB maana nitasoma mambo ya Afya nikifika chuo endapo nitafaulu, basi hadi hapo nikabaki na PCB na nikakomaa kufanya juhudi za kufaulu(nilisota sana) hadi nikafanikiwa na nikafanikiwa pia kusoma mambo ya Afya.

Bila shaka nitakuwa nimekujibu.

Asante sana kwa maelezo yaliyojitosheleza.

Chaguo lako la Shule likakutoa kutoka Uhandisi kwenda Afya.....
Je unafikiri ni mfumo wetu wa Elimu haujajikamilisha mpaka ukapitia hiyo changamoto?
Nina hakika wengi tu wamepitia njia uliyopitia....Any regrets?
 
Back
Top Bottom