JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

Malcom lumumba nini kinakufanya uamini kuwa Russia ni zaidi ya USA linapokuja suala la nguvu za kijeshi baina ya nchi??
Mimi siamini kama Urusi ni zaidi ya Marekani kijeshi au Marekani ni zaidi ya Urusi: Ninachopingana na watu siku zote ni ule usemi wa kusema Marekani anaweza kucheza na Urusi au Uchina kama ambavyo anacheza na Syria, Iraq au Libya.
 
Mimi maswali yangu Ni kwa zero IQ NA sio malcom
Hivi hizi hard talk za jf huwa mnawasiliana kwanza na muhusika au inakuwa surprised mbona Malcom mwenyewe hatokezi..halafu mbona Mimi sikaangwi.
Nadhani kachelewa tu hawezi kufanya suprize kwa mtu ambae hujui atakuwepo online au la

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Malcom unaonekana ni mpenzi sana wa kusoma vitabu

Je kwa mwaka mzima kwa makadirio huwa unasoma vitabu vingapi?

Na ni aina gani ya vitabu unavyosoma?
Ndani ya mwaka naweza kusoma vitabu visivyopungua kumi ambavyo viko nje ya taaluma yangu.
Lakini ndani ya mwaka mzima huwa nasoma sana Machapisho yanayohusika na taaluma yangu, na hili nalifanya kila siku.
Nafanya hivi ili niweze kuandika sana, kazi yangu inanitaka kuandika na kufanya tafiti sana.
Vitabu ninavyosoma sana ni vile vya Historia, Uchumi, Siasa, Saikolojia na Sayansi ya Jumla.....
 
Taaluma yako nini Mkuu?

Au ntaipata hapo katika aina ya vitabu unavyosoma!
 
Heshima kwako, mkuu! Umesomea wapi na taaluma ipi? Unaongea lugha ngapi za kigeni? Na ni kitabu kipi kimekuinfluence kimawazo?
Hili ni swali gumu kidogo na naomba nikujibu nusu tu: Mimi ni Mwanasheria.
Vitabu ambavyo vimeni-influence ni vingi sana, lakini naomba nikutajie vichache tu: Biblia Takatifu na The Bramble Bush.
 
Taaluma yako nini Mkuu?

Au ntaipata hapo katika aina ya vitabu unavyosoma!
Mimi ni Mwanasheria japo sasa nimesoma tofauti kidogo katika huo usomaji wangu wa sheria.
Nimejikita katika masomo ya Uchumi wa Kimataifa (International Economics Law), Sheria za Kimataifa (International Law), Sheria za Vita (International Humanitarian Law), Sheria za makosa ya jinai ya kimataifa (International Criminal Law), Haki za Binadamu (International Human Rights Law), Masomo ya Sheria za Wakimbizi (Immigration and Refugee Law), Sheria za Anga na Usafirishaji (Aviation Law), Sheria za Umoja wa Ulaya (European Union Law), Sheria za Uwekezaji (Investment Law)na mengineyo mengiii...........................
 
Back
Top Bottom