JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

JF Hatd Talk "Malcom Lumumba

Mkuu naona kabisa maswali yatakuwa shallow, mpaka nianze kurudi kureview threads zake na zilivyokuwa umiza kichwa, ntajichosha tu.

Ntasoma maswali yenu na mimi hayo hayo ntakuwa nasema, na mimi nilitaka kuuliza hilo hilo, umeniwahi.
Yeah ndio maana ni ka-watag watu makini ambao wanaweza kuuliza maswali critical zaidi ambayo yatakuwa yame utendea haki huu uzi kutokana na hadhi ya weledi wa kufikiri ambayo anayo muhusika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah ndio maana ni ka-watag watu makini ambao wanaweza kuuliza maswali critical zaidi ambayo yatakuwa yame utendea haki huu uzi kutokana na hadhi ya weledi wa kufikiri ambayo anayo muhusika

Sent using Jamii Forums mobile app

Kabisa mkuu, mimi ntaenda nayo thread taratibu mpaka mwisho, nikipitia madesa yangu usiku naweza kupata cha kuuliza kama kitakuwa bado kuulizwa.
 
Mkuu Malcom Lumumba Kama itakupendeza naomba unijibu na hili, kwenye katiba ya nchi fulani hakuna uwezekano wa kuwekwa kitu kama dira ya taifa ya nchi hiyo na kutungiwa kasheria ili kila raisi anayeingia madarakani aanzie alipoishia mwenzie na sio kuendeshwa na utashi wa mtu mwenyewe mfano Tz. kwa kipindi kifupi kimepita na kilimo kwanza, brn, nchi ya viwanda na sasa bize na ununuzi wa ndege. (mi sio mwana siasa na sifungamani na upande wowote na wala sina kadi ya chama chochote)
 
Mtoa mada unapokuwa unaandaa interview Kama hii kwa mtu critical thinker kama Huyu " basi uwe unajitahidi Kuwaalika watu ambao wana fanana walau na kariba yake ya kufikiri kwaajili ya Kumuuliza maswali yenye Tija ...

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini nahisi ajachelewa sana mambo ndo kwanza yameanza ingekuwa vyema mkuu Zero IQ angewa tag wakuje uku tujifunze kupitia maswali yao na majibu ya mkuu wetu wa leo mana huyu bwana ana reference za kutosha.
 
Mkuu Malcom Lumumba Kama itakupendeza naomba unijibu na hili, kwenye katiba ya nchi fulani hakuna uwezekano wa kuwekwa kitu kama dira ya taifa ya nchi hiyo na kutungiwa kasheria ili kila raisi anayeingia madarakani aanzie alipoishia mwenzie na sio kuendeshwa na utashi wa mtu mwenyewe mfano Tz. kwa kipindi kifupi kimepita na kilimo kwanza, brn, nchi ya viwanda na sasa bize na ununuzi wa ndege. (mi sio mwana siasa na sifungamani na upande wowote na wala sina kadi ya chama chochote)
Inawezekana japo hatuwezi kuweka kila kitu ndani Katiba ya nchi: Maana hata hiyo dira ya nchi mkishaifikia basi itawabidi mfanye mabadiliko ya katiba na kuweka dira nyingine mpya. Kiufupi tu ukitaka wanasiasa wasicheze na nchi kuna kitu wanakiita The Eternal Clauses na Entrenched Clauses ambavyo huwazuia wanasiasa au bunge katika kufanya mabadiliko fulani bila kura ya maoni.

Katiba ya Ujerumani ina Eternal Clauses na Entrenched Clauses ambazo hata bunge haliwezi kubadilisha hata siku moja: Hili linajenga dira nzuri ya taifa kwasababu wanasiasa hawawezi kujiamulia tu kila wanapotaka. Ni marufuku kwa serikali kugusa haki za raia, kutaka kubadilisha mfumo wa dola hasa kwenye mgawanyiko wa madaraka na mambo mengine mengi....
 
Back then nakumbuka ID yako ilikuwa ni Caps zote (nahisi ile ID ulikuwa na madini zaidi ya hili). Baadae ukaaga kwamba unaaga kwamba unaachana na JF, baada ya muda sana ukarudi kwa ID hiyo hiyo ila ukabadilisha Caps kama inavyoonekana sasa.

Swali:
  • Ni kipi kilikuondoa JF?
  • Kwa nini uliamua kurudi?
  • In terms of giving and receiving hapa JF (knowledge wise), uzani unalalia wapi zaidi kwako? Do you give more or receive more?
  • How would you rate JF (1 - 10) as a knowledge tool?
Asante.
 
Ukitazama hali ya dunia ya sasa hivi, ni kitu gani kinachokuletea matumaini kwamba mambo yatukuwa mazuri na ni kitu gani kinakujaza hofu kwamba tunakoelekea sio pazuri???! Asante!
Swali gumu sana hili: Lakini ntajitahidi kujibu kwa kadiri ya uwezo wangu.
Nianze na matatizo, kuna suala zima la mabadiliko ya hali ya hewa, Ongezeko la watu duniani, Ukuaji wa teknolojia kubwa bila uwajibikaji wowote na Ongezeko la umasiki duniani. Haya yananiogopesha sana na yatakuja kuleta madhara makubwa sana.

Lakini napata matumaini kwasababu, siku hizi nguvu ya siasa ya dunia iko kwenye mikono ya taasisi za kimataifa (Power Devolution) na siyo nchi binafsi, hivyo ni rahisi sana kufanya mazungumzo na kuzuia matatizo ya kimataifa. UN ina udhaifu wake mkubwa lakini katika kufanya mambo mengine imesaidia sana, kama suala la elimu, wakimbizi, afya, kutatua majanga mbalimbali na mazungumzo. Tumekaa zaidi ya miaka 70 bila matatizo makubwa kwasababu ya UN, AU, ARAB LEAGUE kama kusingekuwa na mazungumzo kabisa na basi matatizo yangekuwa makubwa sana.

Pia upande mwingine teknolojia inaleta tumaini, genetic engineering inaweza kutuondolea kabisa magonjwa kama kansa na kumfanya mwanadamu aishi miaka mingi zaidi. Teknolojia mpya za anga zinatupa matumaini makubwa kwamba kuna siku wanadamu wanaweza wakaishi sayari nyingine,...

Haya machache....
 
Back
Top Bottom