JF Hatd Talk "Malcom Lumumba


Moderator ndiyo aliweka majina madogo, mimi nilitaka MALCOM LUMUMBA.
Nini kiliniondoa na kunirudisha hapa JF: Naomba hili nilielezee siku nyingine mkuu.
Kuhusu kupata maarifa: JF kwangu ni chombo bora kabisa kwasababu huwa nafahamu nini watanzania wengi wasomi wanawaza.
Rating ya JF: Hapa naomba niipe JF 8,hizo mbili nawanyima kwasababu ya Credibility ya habari na vyanzo na siyo tatizo lao.
 
Mkuu Malcom Lumumba, unaionaje nchi yetu Tanzania, ndani ya miaka 20 ijayo hasa katika suala la elimu? Na unatoa mchango gani kuendeleza elimu ya nchi?
Msimamo wangu ni ule ule: tunahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye mfumo wa elimu kama tunataka kwenda na kasi ya dunia.
Wasomi wa Uchina wamesema kwamba ndani ya miaka kumi hadi kumi na tano kuna taaluma zaidi ya 15 ambazo zitapotea kutokana na kuzaliwa kwa Artificial Intelligence. Kama nchi sisi tumejiandaa vipi ???
 

Shukrani sana mkuu.
 
Asante for a comprehensive answer! Mkuu, unasema kuwa "siku hizi nguvu ya siasa ya dunia iko kwenye mikono ya taasisi za kimataifa (Power Devolution) na siyo nchi binafsi" lakini the trend around the world is getting more nationalistic. USA kuna Trump na Make America Great Again na anapuuziya maswala ya climate change, China is also flexing its military muscles in the South China Sea, etc. Is there a way to stop countries with narrow, nationalistic policies from endangering 'global stability'?

 
Uchumi wa Kimataifa (International Economics Law)
• Unahisi Afrika inatendewa haki kwenye mikutano ya Davos au tunaenda kama wasindikizaji?.

Sheria za Kimataifa (International Law)
• Ni sheria ipi kandamizi kwa mataifa ya kiafrica inayotumika sana.

Sheria za makosa ya jinai ya kimataifa (International Criminal Law)
• Nini mtizamo wako kilichotokea crimea.

Haki za Binadamu (International Human Rights Law)
• Nini mtazamo wako kuhusu LGBT Tanzania.

Sheria za Umoja wa Ulaya (European Union Law)
• Unaiongeleaje Brexit!, upo upande upi?.
 
Mkuu, unaona kuna haja ya Katiba Mpya hapa Tanzania? Kama jibu ni ndiyo, nini kifanyike kushindikiza serikali ilete katiba mpya??
Katiba mpya lazima ije mkuu, kama tunataka nchi itoke hapa ilipo. Wao wanasema mbona Marekani haijawahi kubadilisha katiba mimi nawaambia nyie ni waongo na hamjasoma sheria vizuri. Katiba siyo kitabu, katiba ni hali ya kisiasa (Political Situation) ambapo nchi inakuwa chini ya mfumo wa kisheria ambao unafahamika na raia wake kama ndiyo chombo cha kuongoza nchi. Hivyo baada ya kupata uhuru mwaka 1776 ile lose-confederacy ya Marekani ilikuwa inaongozwa na katiba ambayo haikuandikwa. Uingereza hawakutaka kuandika kwasababu waliona madhara ya kuwa na katiba ya kuandika. Haya ni mawazo ya Jaji Barnaba Samata na siyo mimi binafsi.

Hivyo Marekani ilibadilisha katiba kutoka ile isiyoandikwa na kuandika katiba mpya mwaka 1787, waliona umuhimu wa katiba mpya. Kwanini sisi tuogope mabadiliko ndugu yangu ????. Kinachochekesha ni kwamba katiba ya Marekani imepitishwa leo, kesho yake ikapelekwa bungeni ili ifanyiwe marekebisho kwasababu watu walipinga baadhi ya vitu vya mle.

Kuna mengi sana ya kuyabadilisha kwenye hii nchi ndugu yangu, hasahasa kuweka miiko mipya kwa Raisi wa nchi, Bunge na Mahakama. Kuna vitu hii mihimili inatakiwa ibadilishiwe...
 
Nisamehe narudi mara kwa mara na maswali, lakini majibu yako, mkuu, yananisisimua! Kwenye katiba ya marekani kuna 'checks and balances' ambayo inamzuia mwenye mamlaka kutumia mamlaka vibaya. Je, katiba yetu ya sasa inayo hizi "checks and balances'???!

 

Kuna kitabu cha Prof Harlord Hongju Koh kimetoka mwaka jana kinaitwa: The Trump Administration and International Law, ni kizuri sana na kimeyazungumzia haya mambo. Lakini sasa kitu ambacho nataka nikiri ni kwamba kweli mfumo wa sheria za kimataifa uliotengenezwa San-Fransisco mwaka 1945 una madhaifu sana: Mataifa yaliyoshinda vita ya dunia ndiyo yaliyopewa dhamana ya dunia, ndiyo maana hatuna amani mpaka leo.

Sasa tufanyaje: Wazo la wengi ni hili "WE NEED TO REFORM THE SECURITY COUNCIL" na kuruhusu mataifa mengine. lakini binafsi naona hili litaleta matatizo makubwa sana kama yafuatayo: Kwamba kuwe na uwakilishi wa mataifa mengi yakiwa na VETO. Leo tukiwapa VETO Ujerumani itakuwa ni tatizo kubwa kwasababu mataifa matatu makubwa ya umoja wa Ulaya yatakuwepo ndani UNSC (France, Britain and Germany) na watasumbua sana. Tukiwapa Arab League VETO unadhani Israel atakubali kirahisi ??? Tukimpa VETO India na Japan unadhani Uchina atakubali ??? Matatizo matupu.

Mtizamo wangu binafsi: THE UNITED FOR PEACE INITIATIVE ambapo The General Assembly inashika hatamu na kupiga kura juu ya hatma ya usalama wa dunia bila ya kura ya VETO kufanya kazi. Hii ilitumika mwaka 1950 kipindi cha vita ya Korea ambapo Urusi alikuwa anasumbua sana kwa kutokuwepo kwenye vikao vya UNSC basi The General Assembly ikapiga kura ile wapeleke vikosi kule Korea na vikaenda. Nadhani hii ndiyo njia pekee ya kuwafunga Speed Gavana haya mataifa makubwa, na huu mkakati mpaka sasa umezuia matatizo mengi sana duniani, japo mataifa makubwa ya UNSC hayataki kabisa kuusikia.
 
sasa nakuelewa.hongera mkuuu
 
Mkuu, nashukuru sana kwa kunijuza mambo mengi kwa undani! Swali langu la mwisho: Sijawahi kufika mahakamani, lakini kwenye movies nawaona majaji na mawakili wakiwa wamevaa mawigi (wanasema ni nyewele ya kondoo). Je, utaratibu huu upo hapa kwetu na ni nini sababu ya kuvaa mawigs (kuficha upara???) Asante sana na usiku mwema, mkuu Malcom Lumumba!
 
Uchumi wa Kimataifa (International Economics Law)
• Unahisi Afrika inatendewa haki kwenye mikutano ya Davos au tunaenda kama wasindikizaji?.
Kwanza kabisa World Economic Forum siyo chombo ambacho kinaendesha Uchumi wa Dunia, ni Forum kwa ajili ya mazungumzo mbalimbali ya kiuchumi. Lakini upande wa pili sasa, nadhani sisi Afrika tupambane na GATT na TRIPS ambavyo vinatuhusu moja kwa moja. Tupambane na mikataba ya kimataifa ya uwekezaji kwenye hii Forum hata tusipokwenda haidhuru sana kwasababu wenye sauti ni matajiri.

Sheria za Kimataifa (International Law)
• Ni sheria ipi kandamizi kwa mataifa ya kiafrica inayotumika sana.
Katika mikataba ya kimataifa ambayo siipendi basi ni hii ifuatayo:
-The Treaty of Rome for International Criminal Court (ICC)
-The Pelindaba Treaty (Huu mkataba umezuia nchi za kiafrika kufanya tafiti za kinyuklia)

Sheria za makosa ya jinai ya kimataifa (International Criminal Law)
• Nini mtizamo wako kilichotokea crimea.
Kilichotokea Crimea kinaangukia sanasana kwenye Public International Law na siyo International Criminal Law. International Criminal Law inahusika na uhalifu wa kivita wa mtu moja moja. Sasa kimtazamo wa kisheria, kitendo cha Vladmir Putin kuvamia Crimea kijeshi ni Act of Aggression ambacho ni kinyume kabisa na Mkataba wa Kimataifa uitwao The Kellog-Briand Pact wa mwaka 1927 unaozuia nchi kutumia vita kama sera ya nchi. Lakini upande wa pili wametumia sheria ya kimataifa hiyohiyo kujistify Aggression kwa kutumia The Principle of Self-Determination kwa kufanya referendum.

Haki za Binadamu (International Human Rights Law)
• Nini mtazamo wako kuhusu LGBT Tanzania.
LGBT siyo haki za binadamu: Kitafsiri haki za binadamu ni "Inherent entitlements that enable human beings to develop certain faculties". The right to life develops faculties like happiness and prosperity, what does homesexuality develop ??? (Nothing)

It has never been a human right, it is not a human right and it will never be a human right. Japo sasa sipendi kuona watu wanafanyia fujo binadamu wenzao kisa tu ni mashoga. Ushoga upingwe lakini siyo kwa kupitia Inhumane and degrading measures.

Sheria za Umoja wa Ulaya (European Union Law)
• Unaiongeleaje Brexit!, upo upande upi?
Kihistoria Charles De Gaulle wa Ufaransa hakutaka kabisa Uingereza iingie kwenye Umoja wa Ulaya kipindi hicho unaitwa The European Economic Community. Uingereza wenyewe hawakutaka kuingia kwenye ule umoja hadi Winston Churchill akasema hivi "I love the French and Belgiums, but we must not allow ourselves to be pulled down to that level" Uingereza wao walianzisha The European Free Trade Area lakini baada ya kuona Umoja wa Ulaya unapiga hatua ndiyo akaamua kujiunga nao, alituma maombi mara ya kwanza wakamkatalia, alikuja kuruhusiwa baada ya Charles De Gaulle kutoka mwaka 1969.

Mimi nasema hivi European Union was better off without Britain, kwasababu miaka kumi ya mwanzo baishara baina ya wale wanachama wa mwanzo ilikuwa inakuwa kwa asilimia 28.4% sasa Uingereza anapotaka kutoka nasema atoke tu lakini atajuta sana. Maana Umoja wa Ulaya ndiyo The Ultimate Future kwasasa.
 
Na mimi nina swali kwa mtoa mada,ID yangu ya kwanza nilipoingia JF nilikuwa najiita ZERO IQ mwaka 2013 badaye niliibadilisha.Je kwa ww ni kitu gani kilicho kuvutia hadi kutumia ID hiyo?
Mkuu mala ya kwanza kujiunga Jf nilijiita Mzizi mkavu baada ya kugundua kwamba id ziko duplicated niliwaomba mod wanibadili na kuniita Zero iQ, ukiniuliza uliwaza nini kujiita hivyo sina jibu kwa sababu ilikuja Automatic

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Checks and Balances ni Legal Theory ambayo ina supplement the set backs kwenye The Doctrine of Separation of Powers. Hivyo ungeanza na kuuliza kwamba: Je, nchini kwetu kuna Separation of Powers ??? kinadharia na kiutendaji ipo nusu-nusu (Partial). Maana kipindi cha watu kama wakina Mzee Nyalali na Samata ulikuwa husikii serikali na mahakama vinavutana na kila mtu alijua mipaka yake. Japo kuna sehemu Nyerere alishawahi kuwavamia majaji ofisini kwao na kunyang'anya mafaili na hata kuwatishia lakini yote tisa kulikuwa na mipaka sana. Lakini sasa siku zinavyoenda hata Separation of Powers inakuwa ni Myth tu ndiyo maana nasema tuweka mipaka ya Raisi kupitia katiba mpya.

Raisi hatakiwi awe Imperial President.Ataharibu na kuvuruga taswira nzima ya nchi yetu............
 
Ok but kwa mie kuna wimbo wa mabeste unaitwa chupa moja nilikuwa naupenda na katika mistari yake ali mention neno IQ zero akiwa na maana baada ya kulewa chupa moja ya bia akaona kila kitu ni sawa.
 
Siku hizi haupo kabisa, na ulikuwa ni utamaduni ambao tuliiga kutoka kwa waingereza tu. Siku hizi hata ukiingia chambers unakutaka na Jaji kavaa shati la Batiki na hana shida, mimi nilibaki nacheka sana tu. Japo nisema kabisa suala zima la Legal Practice sijahusika nalo kwa muda mrefu sana, mimi nahusika na Research na mambo mengineyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…