JF Karibuni Tanzania Professionals Network


My brother Pundit, thank you for your useful contribution. I am not very sure if you are able to understand swahili, if YES, please go through some of my responses as I have already made detailed clarifications on the matter of having different professionls in a single group (TPN). Please let me know if you may need any additional clarification.

However we at TPN still welcome any ideas which will assist to polish and shape TPN. We have agreed in principle to refine our objectives and focus on our main core issues. Thank you so much for your advise on this regard.

We have also taken note on the question of Membership and we will try to put it in a clear form.

As to the matter of grammer and the texts . . . LOL, well, I am not an expert in language nor a Legal matters, but I can assure you my brother that our Legal Advisor went through the consititution as well as other members. It could be an ommission or it could be the way it is supposed to be. I promise to do consultation on that matter and if necessary rectify.
 

Mzalendo Kichunguu, asante sana kwa mchango wako makini. Nauthamini sana. Kimsingi tumekubali kuwa yale maneno yanayoleta mkanganyiko ni lazima tuyabadilishe.

Napenda tu kuwahakikishia kuwa ndani ya TPN kuna watu ambao si lazima wawe wamemaliza elimu ya juu. Nakumbuka nimewaona wengi ndani ya TPN na hata katika meetings. Kuna ndugu moja yuko pale Temeke yeye si graduate lakini anaweza kutengeneza betri za gari kwa kuweka cells zingine. Tunao pia wanamziki wakongwe ambao si graduates nk.

Napenda nikuahidi kuwa tutalifanyia hilo mabadiliko na kuriboresha. kama utakuwa na maoni yoyote mengine au kama unapenda kutoa mchango wa kimaandishi, tafadhali kuwa huru kufnya hivyo.
 
Naomba ufafanuzi kabla sijakukurupukia.

Mkulu Kuhani, usije ukanihukumu kusulubishwa ngoja nijitahidi kutoa ufafanuzi . . . . LOL

Tunaposema mtu yeyote mwenye positive attitude tuna maana yule ambaye masuala ya kimaendeleo atakuwa anayaangalia kwa mtazamo chanya badala ya mtazamo hasi.

All professionals - Mkuu hili nimelitolea sana maelezo kama umesoma baaadhi ya responses zangu . . . . LOL. Hata hivyo maana ya Professionals katika katiba ina maana wale waliosomea fani fulani, lakini pia wale wenye ujuzi katika fani yoyote bila kujali elimu yake.

Tumekubali kuwa hili linahitaji marekebisho na kuboreshwa zaidi katika Katiba ya TPN.

Mzalendo Kuhani kama unayo maoni yoyote mazuri ya kuboresha tafadhali tuwasiliane
 
Mr. Mtsimbe you are handling matters very presidentially in this thread. It seems to me that those who gave you the presidency did no mistake. Keep it up.

Asante sana kwa compliments zako Mzalendo Zemarcopolo . . . If I go by your saying . . . "To whom much is given, much is expected"

Mkulu, mimi nimepewa madaraka ambayo niliyaomba mimi mwenyewe na kisha kuchaguliwa. Katika dhana halisi, uongozi ni dhamana.

Ni dhamira yangu binafsi kuwa katika kipindi changu cha uongozi nifanye kazi kwa bidii na ubunifu na uaminifu wa hali ya juu ili kipindi changu kikiisha wenzangu watakofuatia waone pia ni kitu gani tumefanya. Tungependa TPN ijengwe katika misingi imara na ndio maana nimeona nijipitishe hapa katika tanuru la moto ili kusafishwa na kuja na kitu kizuri.

Wote mlio tayari naaomba tusaidiane kuijenga vema TPN
 

Katiba haiendani na maelezo yako. Nimeyasoma yalivyojipinga. Ndio maana nikaomba ufafanuzi.

Ahsante.

Swali langu la mwisho, kama jibu lako halitazua maswali mengine. Kama utajibu:

Je, matatizo ya Katiba yako umeyajua hapa leo, au hata kabla ya kuja kuinadi hapa bila ku disclose toka mwanzo kwamba the seminal document yenu ina mushkeli katika kutueleza nyinyi ni kina nani na mnakubali kumkaribisha nani katika chama chenu cha Wenye Digrii na Mashirika ya Biashara kama ilivyo sasa mpaka hapo mtakapofanya amendment.

Ahsante tena.
 


Mzalendo Mwanakijiji, nafurahi kwa ukaribisho wako hapa JF. Na hongereni kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya. Mwenye macho haambiwi tazama, mchango wa JF unaonekana.

Nimefurahi pia kwa mchango wako na nakumbuka hata katika makala yako huko nyuma ulielezea concerns zako. Nitajitahidi kufafanua uliyoyaeleza.

Ukiangalia vema background ya TPN (refer tovuti pia) utagundua initially ilikuwa ni kikundi cha graduates wachache waliomaliza UDSM miaka ya kuanzia 1990 na baadaye kujiunda kwa upana zaidi na kuwa TPN. Kilichotokea ni kuwa kulionekana dhahiri kuwa Wanataaluma kwa maana ya Graduates tulikuwa hatuna kitu cha kutuunganikiha katika mambo ambayo ni Cross-Cutting. Wakati huo huo concern kubwa na ya wengi ilikuwa ni vipi wainue na kuboresha hali zao za maisha kwa kufanya miradi huku wakiendelea na ajira zao. Hii lilikuwa ni tatizo la kimsingi kwa graduates wengi ukiacha wale ambao walikuwa na mafanikio ya kibiashara tayari.

Katika vyama vingi vya Kitaaluma agenda hii aidha haikuwapo kabisa ama kama ilikupwapo si kwa maana pana ya kumwezesha kiuchumi mwanataaluma moja moja au kikundi.

Kwa hiyo wazo la awali lilikuwa ni kuwaunganisha wanataaluma wa background hiyo. Katika kipindi hicho pia ilionekana kuwa wanataaluma wengi walikuwa na hamu na kiu ya kuchangia katika maendeleo ya nchi hasa katika kuanzisha miradi mbalimbali. Wengi walikuwa ni maofisa walioajiriwa katika nafasi mbalimbali na wengine wamejiajiri katika biashara au makampuni yao.

Lakini mbali ya hilo pia kulikuwa na Changamoto kuoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kikwete. Utakumbuka kuwa katika hotuba yake ya kuzindua Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pale Dodoma siku ya tarehe 30th December 2005 alisema hivi, nanukuu:

"Katika Dunia ya Utandawazi na Ushindani Unaoambatana nao, Watanzania wasomi watabaki nje iwapo hawatakuwa wabunifu zaidi, wakaungana na kuanzisha kampuni kubwa za wazalendo, lakini wakikubali kuungana, na kuanzisha kampuni kubwa zinazoendeshwa kwa misingi halisi ya kibiashara na. sio ubabaishaji, serikali, kupitia vyama vya taaluma zao, itawaunga mkono, itawasaidia na itawawezesha"

Hili pia lilileta changamoto katika kuundwa kwa TPN. Zaidi ya hayo huko nyuma kuliwahi kuwa na discussion ya BRAIN DRAIN ambayo conclusion yake ilizaa 50 BELIEFS OF TPN ambazo zinapatikana katika tovuti under RESOURCE CENTRE.

Baada ya background hiyo sasa tuangalie masuala ya msingi uliyoyataja:

Jina - awali jina lilichaguliwa kuliflect wanataaluma katika background liliyoitaja hapo juu. Wengi walikuwa ni maofisa katika sehemu zao za ajira na wengine wahadhiri wa chuo kikuu, nk. Baadaye wigo wa membership ukapanuliwa ukiwahusisha Wanataaluma wote kwa maana ya graduates na pia wanataaluma kwa maana ya wenye fani zao bila kujali elimu yao. Jina hili lilikuwa na maana pia ya kutoa taswira kwa Wanataaluma wote kuwa sasa tuna mahali petu pa pamoja. Nadhani upungufu huu itabidi ufanyiwe kazi hasa katika membership clauses ili kuliflect wanataaluma vizuri wanataaluma ambao si graduates.

Katika maana pana zaidi nakubaliana na maoni yako. Tunao members wengine ambao si graduates lakini wana fani zao mfano, wasanii, wakulima, wahitimu wa vyeti kutoka vyuo vya ufundi stadi nk.

Asante sana kwa maoni yako mazuri Mwanakijiji na tutajitahidi tuyafanyia kazi.
 

Mzalendo Kuhani, naona una muelekeo wa kuwa mkali na kuanza kutoa hukumu . . . LOL usijali nitajitahidi tena kufafanua. Mwanzoni ulihighlight in red na kuatka ufafanuzi walau sasa umetoa maelezo nimekuelewa.

Kwanza si kweli TPN ni chama cha watu wenye madigrii na mashirika ya biashara . . . sijui hili umelitoa wapi. Nadhani huko nyuma nimetoa maelezo ya kutosha. Nakumbuka nilipaste hata quote kutoka katika constitution kuelezea qualification ya wanachama ingawa pia nilikubali kuwa maelezo yake inabidi ya boreshwe. Pia sidhani kama kiongozi napimwa kwa maandishi au maneno, kwangu mimi kiongozi anapimwa kwa matendo.

Naomba tena niweke quote ya membership kutoka katika katiba:

3.1 MEMBERSHIP.

Membership of the Organization shall be open to:

3.1.1 Individuals who is of sound mind and attained the age of majority who are interested in furthering the work of the Organization and who will be appointed and approved by the Executive Committee and who have paid for the registration fees and annual subscription laid down from time to time by the Executive Committee. Must be Tanzanian Graduates from Higher Learning Institutions within or outside the country with a POSITIVE ATTITUDE, and;

3.1.2 Any corporate or unincorporated association or body which is interested in furthering the Organization's work and that has been approved by the Executive Committee and has paid for the registration fees and annual subscription (any such body is being called in this constitution "member organization").

3.1.3 Honorary Membership given to other individuals, groups or Corporate which supports the Vision, Mission and Objectives of Tanzania Professionals Network.


Kwa ufupi mwanachama anaweza kuwa:
1. Graduate of Higher Learning Institutions
2. Corporate Association or body
3. Uncorporate Association or Body
4. Other Individuals who do not fit in the three above but have interest of joining TPN.

Kwa lugha rahisi na kwa ujumla ni kuwa yeyote anaweza kuwa mwanachama ili mradi awe graduate wa elimu ya juu, au kampuni ambayo inaafiki malengo ya TPN au mtu yeyote hata kama si graduate ambaye anaafiki malengo ya TPN.

Mimi ni mmoja wa viongozi wa TPN na nina wadhifa wa Rais wa TPN.
 
Maelezo bado yananipa maswali mengi kuliko majibu.... tupo pamoja bado Sanctus.

Bado napiga hatua na I sincerely hope that there will be light at the end of the tunnel.

Mzalendo Mzozo, bado niko sambamba na wewe. Tafadhali nijulishe kama kuna ufafanuzi unahitaji.
 

Mzalendo Mama, tuliwahi kuliongelea hili katika TPN. Mawazo yaliyokuwapo ni kuwa yeyote atakayepatikana kna kuhakikishwa wenda kinyume na maadili ya Kitaaluma ikiwa ni pamoja na ufisadi, nk atafukuzwa unachama
 

Ndugu yangu Mzozo, nashukuru sana kwa pongezi zako. Kwa kweli bado sana nahitaji mawazo na critics nyingi mimi na wenzangu ili kuboresha. Nataka kukuhakikishia kuwa thread yote hii, nitaitawanya kwa members wa TPN ili nao waweze kutoa mawazo yao. Sina uhakika kama wengine ni members hapa JF.

Kama unataka kutuma mwaliko rasmi wa kujiunga JF kwa members wa TPN nakushauri utume email ya utambulisho kwa secretary@tpn.co.tz nina imani atashughulikia na kutoa maagizo isambazwe kwa members. Sasa hivi circulation list ni zaidi ya members 1000. Jisikie huru.
 
Sanctus..

Umefanya kitu kimoja ambacho ni very rare hapa.. you didn't snap! labda kuja kwa jina lako mwenyewe na katika capacity yako kept you in check! Asante kwa uungwana wako maana wakati mwingine JF inaweza kumpush mtu hadi akaamua kuomba togwa azimulie.

Nadhani jambo moja ni dhahiri kwamba TPN inahitaji mabadiliko ambayo ni ya lazima ili iende na lengo lake lakini pia ili iweze kuakisi kwa haki matamanio ya wanachama wake wa sasa na wale wa baadaye. Muda uliotumia hapa natumaini umekupa mwanga wa yale ambayo bila ya shaka tayari unayajua au mengine mapya. Nakuomba tu ukiweza print hii kitu na uisambaze kwa uongozi wenu.

Lakini kubwa zaidi ni haja ya nyinyi kukutana hata kama katika extra ordinary meeting (kama imo kwenye Katiba) ili kufanya mabadiliko yanayohitajika ili kuifungua TPN kwa wanachama wengi zaidi na wapya. Endapo hili litaweza/linapangwa kufanyika mapema ni bora zaidi kwa sababu kuna watu ambao bila ya shaka wamekuwa wakisubiri mabadiliko hayo ili na wao waweze kujiunga nanyi.

Asante sana.
 

GM asante sana bro. Kuna mambo mengine yanahitaji sacrifice na hata kutake risk. JF si mchezo, ni tanuru, we si unaona hoja za wakulu, unaweza ukaingia mitii hivi hivi.

Wenzangu wa TPN wako na kila mtu akiwa na majukumu yake. Of course wote tunaweza kutofautiana katika utendaji na commitment lakini lengo letu ni moja na nina uhakika kila mtu ana umuhimu wake na mchango wake. Ila ningefurahi sana kama members na viongozi wote wangekuwa active sana. TPN ingekuwa mbali sana.

Hoja hii ni ngumu, ngoja nife nayo tu mimi mwenyewe hata kuniua niueni lakini siachii . . . haaa haaa LOL
 

Ndugu yangu Akilimtindi, nakubaliana na wewe . . . yote sawa tu na tuone mambo yanavyokwenda kwa sasa. Mimi nadhani mtu anweza kuwa JF lakini pia ni members wa TPN. Pia mtu anaweza kuwa members wa JF lakini pia ni member wa TPN. Mimi nadhani kikubwa ni kufocus katika malengo makuu ili mradi tu yaliyokusudiwa yanafanikiwa. Na si lazima kudisclose identity yako ya JF ukiwa TPN.
 


Mkuu sana Kuhani . . . , nimelieleza sana kwa kirefu hili. Kwa wale ambao wamepata nafasi ya kuhudhuria Networking Events, haya mambo huwa yanaelezwa na kueleweka. Pamoja na clearity inayotakiwa katika Katiba, bado kwa kutumia katiba hiyo hiyo iliyopo mengi yameweza kufanyika. Hata hivyo hilo litaboreshwa.
 

Mzalendo Mwanakijiji natambua sana with due respect kuwa JF si mahala pa mchezo, mimi napaita Tanuru na Moto . . . LOL. Madhumuni ya kuja hapa pamoja na kutoa mualiko, nilitaka tupitie katika Tanuru hili ili tuweze kujisafisha na pia kijiboresha kwa kupata michango yenu ya mawazo na mitazamo yote.

Kwa hakika tutakuwa na AGM mwezi wa nane na hili la kuboresha katiba litakuwa ni moja wapo.

Hawa wakulu humu JF wakishamaliza kutoa maoni yao nitayakusanya yote na kudistribute kwa TPN Members ili yafanyiwe kazi pamoja na wao pia kutoa maoni yao. TPN inathamini sana michango yote yenye mwelekeo wa kujenga na kuboresha.
 

Mtu ambae yuko kundi la kwanza, la digrii, ambae haafiki malengo ya chama, anaweza kuwa member kwa mujibu wa katiba? Kama anaweza basi nyinyi mtakuwa hamna "sound mind" mnayoitaka kwa wengine.

Kama hawezi kujiunga basi Katiba yenu inaipiku ile sheria mbovu kuliko zote duniani inayosema Rais wa Tanzania asilipe kodi.

Let X = sharti la kuhitimu madigrii.
Let Y = sharti la kuwa shirika au chombo kingine, "unincoporated body."
Let L = sharti la kuafiki Lengo la chama.

Wanachama wa Kundi la kwanza: Sharti X, na sharti L

Wanachama wa Kundi la pili: Sharti Y, na shart L

Wanachama wa Kundi la tatu: Sharti L.

Kwa hiyo, huwezi kuingia kama hujatimizia L. Sawa?

Na ukishatimiza L, huhitaji X na Y tena!

Kwa hiyo X na Y hazihitajiki! Clause 3.1.1 na 3.1.2 zinauawa na Clause 3.1.3

Hapo mnachekesha.

Unless, unless, ukitimiza sharti la madigrii, basi sio lazima uafiki malengo ya chamaaa haa haaaa a haaaaaaa!

This is hilarious! Endrew Chenge couldn't write such legal comedy.

Swali la nyongeza: Je, "unincorparted body" mtakayo ruhusu inaweza kuwa kama nini, kundi la mtaa wa pili la wacheza ngoma ambao hawako organized kwa saaana?

Anza upya.

Tena!
 
Sanctus,
... mimi sijawa 'professional', ila kwa kuonesha umwanapinduzi wenu kunasiku mbeleni nitajaribu kujiunga, natumaini nitakidhi mahitaji... na katiba mliyonayo sasa itakuwa "imeshaboreshwa" vya kutosha iwapo watu makini kama akina Kuhani watazidi kuwapa challenge muhimu kuhusiana na muundo wa chama kwa nia ya kukiendeleza.

Akhsante kwa mwaliko.

SteveD.
 

Well Spoken Sanctus, and thanks again for your invitation, in some sense umedemonstrate some sound leadership skills za kuhakikisha unazama na chombo chako, Congratulations! Count me in!
 
Ingawa sijasoma majibu yote yaliyotolewa na Mheshimiwa Mutsimbe, ni dhahiri kuwa ameonyesha kuwa na uwezo wa juu sana wa kuchukua hoja za watu mbali mbali na kuzikabili katika mwelekeo wa kuleta maendeleo ya maana kwa jumuia anayoongoza bila kuwa na jazba. Hiyo ni sifa nzuri sana kwa kiongozi; laiti wanasiasa wetu nao wangekuwa namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…