JF Member wengi hawana hela ila wanajiita Great Thinkers, Kivipi?

Ungekua na akili timamu huu muda wa kuandika utumbo ungetengeneza tangazo huko Insta...

Upate chochote kitu uhame kwa dada....
 
Kkaa washamba humu ni wengi
 
Unafikiri naanzaje kununua bidhaa zako mtu mwenyewe utambulisho wako upo nyuma ya pazia, au unafikiri ni nani anakubali kuuziwa mbuzi kwenye gunia, usituhalibie CV mzee, humu tupo vibopa wengi tu tumejazana.
 
Na wanaomba ela jamani watu wa humu! Hawajali unayo au huna πŸ™ŒπŸΎ
 
Kuwa identified kivipi wakati mtu unamtafuta kwa no na sio id?
Unakumbuka tangazo lako hukuweka namba za simu hata nikakufata PM kukuomba hiyo namba nikisema nakuunganisha na mtu?

Well upo sahihi na unaweza usiwe sahihi vile vile,jamaa yupo sahihi mazingira ya humu kuitiwa tu kitu bei rahisi hakuwezi kumfanya mtu ajianike hadharani nchi yenyewe imejaa mauwaji kila kona.
 
Hizo ni mbinu za kuteka watu upande wangu siwezi ku risk kama mtu yupo serious tangazo lake liwe direct sio ana acha maswali ili uende PM muombane number baadae Mafwele yupo mlangoni kwako
 
Unatuvuruga masta,siyo wote humu hatuna akili kingine kwanini usiishi uhalisia wako?ujifanye una hela wakati huna sasa huo si utakuwa ujinga!?

Fake ID hainifanyi ku-act vitu nisivyonavyo,kama maskini maskini kama tajiri tajiri sasa umvimbie mtu humu wewe tajiri wakati hakuna hata siku atataka kuonana na wewe si ujinga huo?
 
Relax.
Biashara haitaki hasira mkuu.
Nachoshukuru umeshapata solution ya biashara yako.
Ukitaka kuuza ka run ads Instagram, usipost tena humu.

Humu acha tuendelee kujadili jinsi ya kula tunda kimasihara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…