Jf members mpunguze uongo kidogo

Jf members mpunguze uongo kidogo

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2022
Posts
1,770
Reaction score
2,841
God is good all the time, All the time....(don moen).

Humu ndani kuna vijana wanatupiga za uso nyingi sana. Mpaka sasa nimeshawakariri members 21 (kwa Id zao), hawa watu ni waongo, ninaposema ni waongo ujue ni waongo kweli kweli (standard gauge). Ni kweli mnafurahisha na kuchangamsha lakini mnazidisha!

Kuna mtu anakuja na stori yake ya kujitungia tungia tu, halafu anavaa uhusika yeye mwenyewe, mwisho wa siku (tena siyo mwisho wa siku, kesho yake) utoana analeta mada nyingine ambayo ukilinganisha na ile ya kwanza, hazileta picha kabisaa!

Kama unajijua unakuja hapa kufurahisha (uongo) na huwezi kukumbuka ulisema/utasema nini kwenye nyuzi zako, basi tumia nafsi ya mtu mwingine ~yeye, ali, wao n.k, siyo "Mimi" nikawasha gari langu nikaondoka (mfano lakini) halafu mwisho wa siku unakuja hapa kulalamikia "ajira".

Kwani hilo gari ni la mkopo? Ok ngoja ninyamaze ili kuepuka shambulio na mkija kivingine, naanza kuwataja mmoja baada ya mwingne, si nawajua!
 
God is good all the time,
All the time....(don moen)

humu ndani kuna vijana wanatupiga za uso nyingi sana!

mpaka sasa nimeshawakariri members 21,(kwa Id zao) hawa watu ni waongo: ninaposema ni waongo ujue ni waongo kweli kweli (standard gauge)

ni kweli mnafurahisha na kuchangamsha lakini mnazidisha!!

kuna mtu anakuja na stori yake ya kujitungia tungia tu alafu anavaa uhusika yeye mwenyewe, mwisho wa siku, (tena sio mwisho wa siku: kesho yake) utoana analeta mada nyingine ambayo ukilinganisha na ile ya kwanza, hazileta picha kabisaa!

kama unajijua unakuja hapa kufurahisha (uongo) na huwezi kukumbuka ulisema/utasema nini kwenye nyuzi zako,
basi tumia nafsi ya mtu mwingine ~yeye,ali ,wao nk
sio "mimi" nikawasha gari langu nikaondoka(mfano lakin) alafu mwisho wa siku unakuja hapa kulalamikia "ajira"

kwani hilo gari ni la mkopo??
...ok ngoja ninyamaze ili kuepuka shambulio!

na mkija kivingine, naanza kuwataja mmoja baada ya mwingne, si nawajua!!
Haya magari haya🤔🤔
 
God is good all the time, All the time....(don moen).

Humu ndani kuna vijana wanatupiga za uso nyingi sana. Mpaka sasa nimeshawakariri members 21 (kwa Id zao), hawa watu ni waongo, ninaposema ni waongo ujue ni waongo kweli kweli (standard gauge). Ni kweli mnafurahisha na kuchangamsha lakini mnazidisha!

Kuna mtu anakuja na stori yake ya kujitungia tungia tu, halafu anavaa uhusika yeye mwenyewe, mwisho wa siku (tena siyo mwisho wa siku, kesho yake) utoana analeta mada nyingine ambayo ukilinganisha na ile ya kwanza, hazileta picha kabisaa!

Kama unajijua unakuja hapa kufurahisha (uongo) na huwezi kukumbuka ulisema/utasema nini kwenye nyuzi zako, basi tumia nafsi ya mtu mwingine ~yeye, ali, wao n.k, siyo "Mimi" nikawasha gari langu nikaondoka (mfano lakini) halafu mwisho wa siku unakuja hapa kulalamikia "ajira".

Kwani hilo gari ni la mkopo? Ok ngoja ninyamaze ili kuepuka shambulio na mkija kivingine, naanza kuwataja mmoja baada ya mwingne, si nawajua!
Wivu unakusumbua kwakuwa huna nyumba wala magari kama members wenzako wote wa JF
 
Hivi mtu kuwa na gari ndiyo kuyapatia maisha,
Nimetoa mfano wa gari tu lakini humu chai ni nyingi mno!
hata hivyo kama utaweza kupata gari kwa nguvu zako mwenyewe bila kuiba, kutapeli, kurithi au shortcut yoyote basi wewe hupaswi kuwa mtu wa kulialia
 
ujinga, umasikini, na maradhi ndio adui wa maendeleo

njoo hapa tukusaidie mawazo ufikie ndoto zako, sio kujifanya unaweza sana
Umaskini nilishauaga kabla wewe hujazaliwa... Maradhi yananiogopa maana yakinishika naenda India kuyasambaratisha.... Ujinga nilifuta nilipopata PhD yangu pale Oxford University
 
Umaskini nilishauaga kabla wewe hujazaliwa... Maradhi yananiogopa maana yakinishika naenda India kuyasambaratisha.... Ujinga nilifuta nilipopata PhD yangu pale Oxford University
kama unaamini PhD inafuta ujinga, basi wewe bado ni mjinga. ila hujijuwi
 
Humu kuna chai kinoma leo mtu anaweza kukupa ushauri wa biashara ya magari na anakusisitizia yeye ndio biashara anayoifanya mpaka kajenga ghorofa mbili Mbezi,halafu wiki ijayo anajisahau anaanza kuulizia duka gani zuri kwa spare za guta lake analouzia maji gongo la Mboto maana limeharibika anashindwa kupata pesa ya kula!! Yaan vurugu tupu
 
Back
Top Bottom