JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

FB_IMG_1654312562728.jpg
 
Tom Mboya.
Majina Kamili, Thomas Joseph Mboya. Alizaliwa 1930 na Kufa Julai 1969. Miongoni wa mashujaa waliohakikisha kuwa Kenya imepata Uhuru kutoka kwa wabeberu kwa kutumia vikundi za Trade Union.
Wengi huku Kenya humuona kama The president that Kenya never had. Baada ya kenya kujinyakulia Uhuru alikua mmoja wa Mawaziri wa Jomo Kenyatta. Pia alikua na programme ya kupeleka Waafrika wa Kenya nchi ya America kwa masomo zaidi wakiwemo Barack Obama Senior (Babake Barack Obama) na Wangari Maathai ambaye ni Mwanamke wa Kwanza Africa kushinda tuzo la Nobel Peace Prize.
Mboya aliuawa 1969 kwa kupigwa risasi jijini Nairobi alipokua akitika kwenye Pharmacy. Kifo chake kilisababisha chuki Kubwa baina ya makabila ya Waluo na Wakikuyu. Aliyempiga risasi alikua anaitwa Nahashon Njenga ambaye alikua mkikuyu.
Kabla ya kifo chake. Wengi walikua wanamuona kama mtu ambaye angekua Rais wa pili wa Kenya baada ya Jomo Kenyatta.View attachment 2051239
Thomas Joseph Odhiambo Mboya aka Tom Mboya
 
Back
Top Bottom