JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Miaka 44 toka huyu mwamba atutoke
Marehemu MBARAKA MWiNSHEHE MWARUKA
ALIFARIKI TAREHE12-1-1979 akiwa na miaka 34

FB_IMG_1674061515841.jpg
 
Heri ya Siku ya Kuzaliwa ya 57 Rexton Rawlston Fernando Gordon 17 Januari 1966 anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii Shabba Ranks, ni mwanamuziki wa dancehall wa Jamaika. Mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990, alikuwa mmoja wa wanamuziki maarufu wa Jamaika ulimwenguni. Wakati wote wa umaarufu wake katika nchi yake kama msanii wa dancehall, alipata umaarufu huko Amerika Kaskazini na albamu yake ya studio, Just Reality, mwaka wa 1990. Alitoa albamu mbili za studio, As Raw as Ever na X-tra Naked, ambazo zote zilishinda Grammy. Tuzo kama Albamu Bora ya Reggae mnamo 1992 na 1993, mtawalia. Anajulikana sana kwa nyimbo za "Mr. Loverman" na "Ting-A-Ling", ambazo zilisifiwa ulimwenguni kote na kuzingatiwa kuwa nyimbo zake sahihi.

FB_IMG_1674179787556.jpg
 
Kama ulikuwa unasikia tu Scolastica Bus Services ndiyo hii, ni Scania 82M. Ilifanya kazi kama daladala miaka ile ya 80, nilikuwa nikìliona mara nyingi kule Posta baharini kabla mmiliki wake hajalipangia safari za mikoani. Ni moto wa kuotea mbali, acha kabisa hiyo gari. Wahenga wengi wanalijua hili basi.
FB_IMG_1674239797198.jpg
 
Kama ulikuwa unasikia tu Scolastica Bus Services ndiyo hii, ni Scania 82M. Ilifanya kazi kama daladala miaka ile ya 80, nilikuwa nikìliona mara nyingi kule Posta baharini kabla mmiliki wake hajalipangia safari za mikoani. Ni moto wa kuotea mbali, acha kabisa hiyo gari. Wahenga wengi wanalijua hili basi.View attachment 2489298
 
Hii ni siku Taifa Stars katika mechi ambayo walicheza vifua wazi kwani walilazimika kuvua jezi kufuatia jezi zao kufanana na za wapinzani wao timu ya taifa ya Sudan. Hivyo refa wa mechi hiyo Manyoto Ndimbo aliamuru Taifa Stars wavue jezi.

PICHANI : Mgeni rasmi alikuwa Rais Jaffar El Nimeiry wa Sudan akikagua timu. Baadhi ya wachezaji kuanzia kushoto : Mohammed Chuma, Omari Zimbwe na Kitwana Manara.
FB_IMG_1674239997459.jpg
 
Back
Top Bottom