JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Mkuu huyo Lt. Col. Suma ndo chanzo cha jina la SUMA Jkt au
 
Hii timu ya Taifa star ya mwaka 1980
Ambayo ilifuzu kwenda Nigeria
Kutoka kushoto waliosimama Peter Tino
Tenga
Marehemu Mambosasa
Hussein Ngulungu
Marehemu Mohamedi Kajole Machela
Jella Mtagwa
Kocha Marehemu Joe Bendera
Waliokaa kutoka kushoto Ahmed Amasha
Nimemsahau
Nimemsahau
Mohamedi Salim
Mohamedi Rishard
Wahenga karibuni tuje tudadavue
Wenu mhenga mwenzenu Mzee wa zilipendwa Baba Adede Mwinyii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
King Cross hiyo, Leyland Clydesdale (CD). Enzi hizo usafiri vijijini ni mgumu na ukilikosa basi leo mpaka kesho, nakumbuka utakuta basi linahudumia vijiji karibu vitatu halafu linalalia kijijini kwenu nyumbani kwenu na linaanza safari alfajiri hapo hapo kijijini kwenu. Mimi nilikuwa nachagua siti ya dirishani kule mbele kabisa kwa dereva ili nione barabara na miti inavyorudi nyuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…