Timu za taifa ktk Zama mbili tofauti 80&90 . Kuna dhana na mtizamo wa wadogo zetu wanetu wa leo Kama kwa nini watu wa zamani wanasema wachezaji wazuri walikuwepo enzi za miaka ya 60 Hadi 90 .
Tukumbuke mpira ulianza miaka mingi Sana nyuma ya hizo Zama mfano akina lyimo na kitwana manara wao walicheza miaka 60 na japo manara alicheza had miaka ya 70 pia ligi yetu official ulianza miaka ya 60 baada nchi zetu mbili kua huru .
Vimepita vizazi vingi Sana miaka hiyo ya 60 akina Ali samatta baba wa samatta nk Hadi leo vijana wetu akina Aishi na bakar mwamnyeto .kwa mtizamo wa haraka haraka inaonekana Kama kipindi hiki ndio soka la nchi linapiga hatua kitu ambacho sio kweli sie Tanzania bado hatujayapita mafanikio yetu .kiukweli wachezaji wa zamani ni Bora kuliko wa Sasa huo ndio ukweli Tena Bora kwa kuachana kwa mbali mno .
Shida ya Tanzania sio nchi ya football tunao mashabiki tu wanaopenda Simba na yanga . mafanikio ya taifa stars walicheza afcon 80 Tena ktk Zama ngumu kufuzu africa zilikua team 8 Kama sikosei ndio mnaenda fainali za afcon zikiitwa mataifa huru .Simba ishafika nusu fainali ya caf champs league miaka ya 70 na kucheza fainali ya caf 93 pia walikua Moto ktk anga za kimataifa uko nyuma .yanga ishacheza Robo fainali caf champs league miaka hiyo ya 70 nk ,malindi ya Zanzibar ishacheza nusu fainali ya caf winners cup 95 au 96 .
Timu ya taifa kuingia ktk nafas ya 65 FIFA ranking 1996 yaan tulikua na watu kwel kwel ata world cup tungecheza .hizo Zama zote wachezaji wanaoleta mafanikio ni wazawa tu hamna mgeni .teams zetu hizi mbili zilivamiwa sijui na watu wa vipi lakini viongoz wa nyuma walikua na maono makubwa awa Leo hawana wengi ni wapigaji unaambiwz yanga walikua na magari Zaid ya 5 na jangwani kulikua hotel ya 4 star pia kumbi kubwa watu wanasakata mziki week end .
Kwahiyo Hakuna mafanikio ambayo wachezaji wa Leo wanayo au viongoz ambalo zamani halikufanyika .Kama afcon tulicheza na vilabu vyetu vilifika mbali kimataifa nk .
Sent using
Jamii Forums mobile app