Kutoka Maktaba kweli tumetoka mbali enzi hizo Wachezaji wa Akiba walikuwa wanakaa chini kwenye eneo la kukimbilia tofauti na sasa hii ilikuwa timu ya Pilsner ya Dar Es Salaam Waliokaa chini kutoka kushoto ni Masatu Magessa,Rajabu Rashid,Muhidini Sisso,Mwarabu Ally na Abdallah Selemani "Kaburu" aliyesimama kushoto Dr. Gullam na wa tatu S. Mziray (Coach)
Timu za taifa ktk Zama mbili tofauti 80&90 . Kuna dhana na mtizamo wa wadogo zetu wanetu wa leo Kama kwa nini watu wa zamani wanasema wachezaji wazuri walikuwepo enzi za miaka ya 60 Hadi 90 .
Tukumbuke mpira ulianza miaka mingi Sana nyuma ya hizo Zama mfano akina lyimo na kitwana manara wao walicheza miaka 60 na japo manara alicheza had miaka ya 70 pia ligi yetu official ulianza miaka ya 60 baada nchi zetu mbili kua huru .
Vimepita vizazi vingi Sana miaka hiyo ya 60 akina Ali samatta baba wa samatta nk Hadi leo vijana wetu akina Aishi na bakar mwamnyeto .kwa mtizamo wa haraka haraka inaonekana Kama kipindi hiki ndio soka la nchi linapiga hatua kitu ambacho sio kweli sie Tanzania bado hatujayapita mafanikio yetu .kiukweli wachezaji wa zamani ni Bora kuliko wa Sasa huo ndio ukweli Tena Bora kwa kuachana kwa mbali mno .
Shida ya Tanzania sio nchi ya football tunao mashabiki tu wanaopenda Simba na yanga . mafanikio ya taifa stars walicheza afcon 80 Tena ktk Zama ngumu kufuzu africa zilikua team 8 Kama sikosei ndio mnaenda fainali za afcon zikiitwa mataifa huru .Simba ishafika nusu fainali ya caf champs league miaka ya 70 na kucheza fainali ya caf 93 pia walikua Moto ktk anga za kimataifa uko nyuma .yanga ishacheza Robo fainali caf champs league miaka hiyo ya 70 nk ,malindi ya Zanzibar ishacheza nusu fainali ya caf winners cup 95 au 96 .
Timu ya taifa kuingia ktk nafas ya 65 FIFA ranking 1996 yaan tulikua na watu kwel kwel ata world cup tungecheza .hizo Zama zote wachezaji wanaoleta mafanikio ni wazawa tu hamna mgeni .teams zetu hizi mbili zilivamiwa sijui na watu wa vipi lakini viongoz wa nyuma walikua na maono makubwa awa Leo hawana wengi ni wapigaji unaambiwz yanga walikua na magari Zaid ya 5 na jangwani kulikua hotel ya 4 star pia kumbi kubwa watu wanasakata mziki week end .
Kwahiyo Hakuna mafanikio ambayo wachezaji wa Leo wanayo au viongoz ambalo zamani halikufanyika .Kama afcon tulicheza na vilabu vyetu vilifika mbali kimataifa nk .
Hapo ni katikati ya jiji maeneo ya Posta, panaitwa Garden ama bustani ya jiji, pale kwenye kaburi moja lililogoma kuhama mpaka leo ambapo ni karibu miaka 200 sasa. Hiyo picha ni ya mwaka 1981 na pembeni hapo ni barabara ya Samora kama kibao kinavyoonyesha. Magorofa hayo mawili hapo mwanzoni bado yapo mpaka leo hivyo hivyo, yana bahati kweli kweli, kwani hayakuvunjwa, na lile kaburi moja lipo pale. Ukipita hapo utajionea mwenyewe kwa macho yako.
CHATCO CHARTER hiyo enzi zake, kwa wale watumiaji wa barabara ya Dar Moshi Arusha, wanalifahamu vizuri sana hili basi. Hapo ni paleeeee Segera kwenye machungwa mengi.
Peugeot 404 ikiwa barabarani, picha ni ya mwaka 1982, hapo ni maeneo ya Kibaha, nadhani atakuwa katokea Morogoro huyu. Peugeot 504 nazo zilikwisha kuwepo barabarani miaka hiyo, lakini bado Peugeot 404 nayo ilikuwa na hadhi/heshima yake nchini.
Hiii timu ya Malindi ya miaka ya 90
Ambayo ilitingisha sana
Kutoka kushoto waliosimama kocha Salum Madadi
Ally Bushiri
Edibily Lunyamila
Hamadi Hilika
Nico Bambaga (RIP)
Twaha Hamidu
Mfadhili marehemu Naushard Mohamedi
Waliochumaa kutoka kushoto Hassan Wembe
Juma Kidishi
Mzungu Julian Ivanov
Abuu Omari
Mbegu Mohamedi Nahodha
Victor Bambo
Dar long ago. Maeneo haya mpaka Magogoni yakimilikiwa na watu toka Baluchstan(nadhani ndio wabulushi). Abushiri akipigana na Mjerumani akipata sana msaada toka kwa hawa watu.Abushiri akavamia nyumba ya watawa iliyokuwa ambapo ilipokuja jengwa hotel ya Kilimanjaro na kuwachinja wote. Kisha akavamia watawa wengine Pugu na kuwachinja wote.Makaburi yao yapo ilipo Msimbazi centre leo. Mara baada ya Mjerumani kumkamata na kumnyonga Abushiri akawageukia hawa Wabulushi na kuwanyonga kwa wingi ili iwe mfano kwa wengine ikawa ndio mwisho wao kumiliki maeneo hayo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.