JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Jengo hili la kwanza kabisa la mahakama kuu tanzania linadaiwa kujengwa na mkoloni wa kingereza kabla hata ya uhuru,

Baada ya uhuru ndipo ilipowekwa hiyo nembo hapo, kwasasa inadaiwa halitumiki, yanayotumika ni majengo mapya

JE KUNA UKWELI HAPO?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ama kweli tumetoka mbali. Hiyo picha ni miaka ya 1980-85 jijini Dar es salaam. Kwa heshima na taadhima na utii bila shuruti, mwache kamanda avuke kwanza. Naona hapo kuna Peugeot 404 Pick up hilo gari jingine silijui mtanisaidia. Kule nyuma naona kuna Malori ya KAUDO na KAUMU na matela yao ng'ambo ya barabara. Karibu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni Askari monument maeneo ya posta miaka ya themanini 80, mpiga picha alikuwa upande huu huku wa jengo la IPS. Mbele naona Peugeot 403, Jengo la Benki ya nyumba Tanzania kama linavyosomeka na kushoto kule ni jengo la NBC.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Scania ni gari sio hizi za kichina miaka 4 Kwisha habari.nakumbuka unatoka na scania Mbeya-Arusha via chalinze ngoma inafika bila kuzimwa engine Wala spana.
 
Leo nimekutana na chogo ikanikumbusha mbali sana. Home wazee waliinunua nikiwa darasa la nne, kwa wenge na furaha mpaka nikavunja mkono[emoji41].

Kabla ya hapo ni wazee watatu tu walikuwa nayo kijijini, kwa mzee mmoja ilibidi tufanye kazi nyumbani kwake kwa muda fulani ndipo tupate fursa ya kuangalia mieleka, we did it wholeheartedly.[emoji41]

Gone are the days [emoji27]!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia inakimbia sana Mshana Jr Sikuhizi wale jamaa wa kupinga picha mitaani hawapo Tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…