JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Hii ndiyo Kivukoni ya enzi hizo, ni vumbi tupu hapo, PANTONI hapo bado saana. Mpiga picha alipiga picha hii akiwa hapa eneo la kivukoni ambapo siku hizi kuna stendi ya mabasi ya Mwendokasi na daladala. Kwa mbali unaweza kujionea sehemu ya Bandari ya Dar es salaam, Kanisa la Roma Mt Joseph na kanisa la Lutheran la Azania Front.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
USAFIRI DAR ES SALAAM

Enzi hizo usafiri hapa Dar ilikuwa mabasi ya UDA tu (UDA stands for USAFIRI DAR ES SALAAM).

Hakukuwa na daladala enzi hizo. Na tulikuwa na utaratibu mzuri wa kupanda kwa kujipanga foleni, tena tunapandia mlango wa nyuma na kushukia mlango wa mbele. Hii ni Leyland. Changamoto pekee ilikuwa WEZI WA MIFUKONI mpaka Vijana Jazz waliimba wakasema Abiria Chunga Mfuko wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiongozi wa bendi ya TP OK JAZZ, Bwana Franco Luambo Makiadi, mwenye shati jeupe, akiteta jambo na kiongozi wa bendi ya VIVA LA MUSICA Bwana Papa Wemba, mwenye mavazi meusi miaka ya 80 jijini Kinshasa wakati huo ikiitwa Zaire, siku hizi ni Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Karibu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchezaji wa zamani wa Uholanzi Patrick Kluivert (kushoto) akipongezana na Kapteni wake Pep Guardiola (Kocha wa Manchester City kwa sasa) baada ya timu yao ya Barcelona kuifunga Chelsea na kuiondosha katika ligi ya mabingwa Ulaya. Huo ulikuwa msimu wa mwaka 1999 / 2000.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sisi wahenga hizi ndizo starehe zetu kipindi Cha utoto mpaka kwenye ujana
Unaaangalia matangazo kwenye magazeti ndiyo unaamua wende wapi
Kama sinema unamua twende jumba gani?
Kama Dance unaaangalia ukacheze rumba gani leo na ukumbi upi?
Kama unataka kuungalia vikundi vya utamaduni wenyewe tuliita kibisa nayo unaaangalia wende wapi?
Wale waruka majoka yaani Disco vilevile unaaangalia ukarukie wapi
Zamani Raha tupu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi hizooooooooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…