JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Kabla ya ujio wa FM enzi hizo hakuna Mtanzania mwenye redio asiyejuwa majina ya Watangazaji hawa - David Wakati, Sara Dumba, Eda Sanga, Sango Kipozi, Omar Jongo, Ahmed Jongo, Ben Kiko, Bart Kombwa, Tido Mhando, Masoud Masoud, Yusuph Omar Chunda, Abdallah Majura, Mikidadi Mahmudu, Betty Mkwasa, Tumbo Risasi, Salimu Mbonde, Sekioni Kitojo, Juliasi Nyaisanga, Charles Hilary, Swedi Mwinyi, na wengineo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lang'ata hiyo enzi zake miaka ya 80. Kama kuna mtu alikwambia kwamba Leyland CD haikimbii, basi huyu mwamba ilikuwa ni habari nyingine, moto wa kuotea mbali Dar Moshi Arusha. Kampuni hii hata hivyo baadaye watoto walikuja kuivuruga ikagawanyika ikazaliwa "KIKAMBALA" yaani (KIKOSI KAMILI MBALI NA LANG'ATA). Kwa hiyo kukawa na Lang'ata na hiyo Kikambala. Hayo mabasi yalifanana rangi na kilakitu isipokuwa majina tu na wamiliki wake, hata hivyo hazikudumu zikaja kufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Kadenge na mpira, Kadenge na mpira..."
Kadenge mwenyewe ndo huyu anachukuliwa kuwa mmojawapo wa wanasoka bora zaidi kuwahi kutokea nchini Kenya, Enzi hizo tukifatilia matangazo ya mpira kupitia Sauti ya Kenya ikicheza timu yake ya Abaluhya Football Club (AFC Leopard) lazima umsikie huyo mwamba akifanya vitu vyake. Joe Kadenge alifariki mwaka 2019 akiwa na umri wa miaka 84.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CD mkuu unanikumbusha route ya Iringa to Dar,kampuni ya KWACHA ilikua na Leyland CD,iliyobatizwa jina la Novallonge Swela,bus hii ilitamba sana,ukiwa Makanyagio ,muziki wa bus hii Mkwawa ulikua unasikika toka maeneo ya Ilala, kipindi nchi Ina heshima na adabu
 
Nakumbuka kuna siku moja baada ya mazoezi tukauchiwa rifle tuchukue nyumbani. Hebu imagine leo mtoto wa miaka 15 aachiwe silaha kama hiyo achukuwe nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa mwaka 1986. Hayo ni maeneo ya Posta ya zamani jijini Dar es salaam na mbele hapo linaonekana Kanisa la Lutherani la Azania Front. Hapo barabarani naona daladala ISUZU ELF ikizunguka kuja huku stendi baharini kwenye Mikungu kupakia abiria. Pichani pia naona gari ndogo nyeupe ikiwa imepaki hapo na vijana wa zamani nao hapo wakiwa wamekaa kwenye ukuta. Karibu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…