Leo turudi nchini Uganda tuwaangalie Joseph wawili pichani: Joseph Kibwetere(1932) Kulia na Joseph Kony(1961) kushoto kushoto.
Wote wakifanya uhalifu wa kutisha kwa mgongo wa dini.
Kibwetere na kanisa lake alisimama katika msingi wa "Harakati za Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu" lakini mwanzoni mwa mwaka 2000 wafuasi wake wapatao 778 walikufa kanisani mwake kwa kuungua na moto na kupuliziwa sumu huku milango ikiwa imefungwa na yeye (Kibwetere) kutoweka, kitendo kilichotafsiriwa na polisi kama mauaji ya kupanga.
Joseph Kony kiongozi wa kundi la The Lord's Resistance Army (LRA) ambalo lengo lake ni kuleta utawala unaofata amri 10 za Mungu, lakini matokeo yake amekuwa na vitendo visivyofaa, anakabiliwa na tuhuma nyingi za utekaji,ubakaji,mauaji na ukatili wa kutisha.
Bahati mbaya hakuna hata mmoja aliyekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
View attachment 2862910
Sent using
Jamii Forums mobile app