JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Boma,enzi ya utawala wa Mjerumani -Tukuyu
Endapo mjerumani angeshinda vita kuu ya kwanza,majina ya miji yetu yangechukua sura tofauti sana.
Tukuyu ikiitwa Neu Langenburg.
Lushoto ikiitwa Wilhemstal.
Kisarawe ikiitwa Hoffnungshoh.
Moshi ikiitwa Neu moschi.
Mbulu ikiitwa Neu Trier.
Mikese ikiitwa Neu Bonn.
FB_IMG_1704166266079.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ni mwaka 2009 nikiwa na CHELEA MAN pamoja na PNC wakiwa wamoto kabisa kutoka kundi la TIP TOP CONNECTION chini ya BABU TALE tukiwa tumemaliza kupiga show katika wilaya ya KONGWA-DODOMA,Baada ya kumaliza show tulileteana mzozo mkubwa na CHELEA MAN wakati wa kugawana mapato kitu ambacho kilisababisha kila mtu harudi kivyake hotelini lakini kulivyokucha asubuhi CHELEA MAN akanipigia cm Ili tuende tukayamalize na ndipo tulipoaamua kuyamaliza na kila mtu akachukua chake kwahyo hiyo picha tulipiga baada ya kuyamaliza,daaa inanikumbusha mbali sana..
FB_IMG_1704360382924.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni SCANIA 82M kama ninavyoifahamu. Kama ulikuwa ukisikia tu, SCOLASTIKA, SCOLASTICA basi ndiyo hii sasa. Ni daladala iliyokuwa ikikimbia sana na kujizolea umaarufu mkubwa sana jijini Dar es salaam miaka ya 80, na hata mmiliki wake alipokuja kuipangia safari za mikoani bado ilikuwa ni moto wa kuotea mbali. Wakongwe wengi wanaikumbuka hii gari.
FB_IMG_1704426580651.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha ya kwanza ni basi la Shirika la Reli Tanzania na picha ya pili ni basi la AMTCO LTD ya Tanga Dar miaka ya 80. Acha kabisa, bodi imara na lenye kupendeza yaani ilikuwa hata likipata ajali, litanyooshwa na kupigwa rangi na linarudi tena barabarani. Inaonekana kama muundaji wa bodi za haya mabasi alikuwa mmoja. Lakini yote kwa yote unakumbuka wapi Muhenga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo turudi nchini Uganda tuwaangalie Joseph wawili pichani: Joseph Kibwetere(1932) Kulia na Joseph Kony(1961) kushoto kushoto.
Wote wakifanya uhalifu wa kutisha kwa mgongo wa dini.
Kibwetere na kanisa lake alisimama katika msingi wa "Harakati za Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu" lakini mwanzoni mwa mwaka 2000 wafuasi wake wapatao 778 walikufa kanisani mwake kwa kuungua na moto na kupuliziwa sumu huku milango ikiwa imefungwa na yeye (Kibwetere) kutoweka, kitendo kilichotafsiriwa na polisi kama mauaji ya kupanga.
Joseph Kony kiongozi wa kundi la The Lord's Resistance Army (LRA) ambalo lengo lake ni kuleta utawala unaofata amri 10 za Mungu, lakini matokeo yake amekuwa na vitendo visivyofaa, anakabiliwa na tuhuma nyingi za utekaji,ubakaji,mauaji na ukatili wa kutisha.
Bahati mbaya hakuna hata mmoja aliyekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
FB_IMG_1704478142282.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo turudi nchini Uganda tuwaangalie Joseph wawili pichani: Joseph Kibwetere(1932) Kulia na Joseph Kony(1961) kushoto kushoto.
Wote wakifanya uhalifu wa kutisha kwa mgongo wa dini.
Kibwetere na kanisa lake alisimama katika msingi wa "Harakati za Kurejeshwa kwa Amri Kumi za Mungu" lakini mwanzoni mwa mwaka 2000 wafuasi wake wapatao 778 walikufa kanisani mwake kwa kuungua na moto na kupuliziwa sumu huku milango ikiwa imefungwa na yeye (Kibwetere) kutoweka, kitendo kilichotafsiriwa na polisi kama mauaji ya kupanga.
Joseph Kony kiongozi wa kundi la The Lord's Resistance Army (LRA) ambalo lengo lake ni kuleta utawala unaofata amri 10 za Mungu, lakini matokeo yake amekuwa na vitendo visivyofaa, anakabiliwa na tuhuma nyingi za utekaji,ubakaji,mauaji na ukatili wa kutisha.
Bahati mbaya hakuna hata mmoja aliyekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.View attachment 2862910

Sent using Jamii Forums mobile app
20231224_095052.jpg
 
Hapa ni Kasulu kwa kijerumani 'Verschanshuis' (Kasulu): Hii ilikua ni makao makuu ya Gavana enzi za Heinrich von Schnee gavana wa mwisho wa kijerumani kabla ya kuondolewa na uingereza ndipo jengo hili likaitwa 'British Organization East Africa Management Admission' (BOMA)., Kasulu,Kigoma
FB_IMG_1704677397451.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom