Kulia kwangu ni mshindi wa Medali ya Shaba katika Ndondi kwenye All African Games mwaka 1978 Algiers nchini Algeria, Lucas Msomba. Kwa sasa Msomba, baadaye refa maarufu wa ngumi za kulipwa anaumwa na amekatwa mguu. Yupo Kibaha kwa Mathias, eneo linaitwa Jamaica ndio amejenga huko na anaishi huko. Kwa wadau wa boxing, atakayeguswa na ana nia ya kumsaidia anichek DM.
Arusha hiyo miaka ya 60. Naiona mbele hapo Peugeot 403 Familly ikizunguka hapo kwa utulivu sana na gereji ya SUBZALI hapo kwenye kona. Hapo kulikuwa na makutaniko ya barabara tatu, yaani Babati Road, Ngoliondoi Road na Sokoine Road, ila kama kuna mabadiliko basi tukumbushane. Karibu sana.
Timu ya Taifa ya Uganda, Uganda the Cranes ilipotembelea Uingereza mwaka 1956. Jamaa aliyeonyeshwa kwa alama ya mshale aliamua kuingia kifusi akapata Chuo huko na baadaye kusoma vyuo vingine vingi. Alikuwa Mwafrika wa kwanza kutoroka akiwa ziara za michezo. Mwaka 1966 aliandika kitabu maarufu sana kiitwacho “The song of Lawino”. Huyo ndiye mwandishi nguli aliyeitwa Okot p’Bitek. Picha hii ni ya taasisi ya Juba Fastlinks Investments
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.