JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Sanaaa nakumbuka nilishawahi kufikia pale nikitokea Kigoma nikapita na Taulo(niliiba[emoji1787][emoji1787])

Basi nilikua naona ufahari sana nikilianika pale nyumbani kwangu Gungu kigoma nilikua naonekana bonge la mshua. Ujana raha sana
Kwani sasahivi wewe ni mzee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muheshimiwa punguza hasira hapa tunapeana elimu na kukumbushana yale tuliyosahau kwa namna moja au nyingine mbali na kuburudika, lakini kumbuka pia kuwa elimu haina mwisho.

Hamna shida mkuu nimekusoma
 
Umenikumbusha mbali kidogo kwa picha hii, na hii ilipigwa ndani ya manowari ya kijeshi ya Jeshi la Afrika kusini wakati wa kikao maalumu cha usuluhishi kati ya Serikali ya Zaire chini ya Rais Mobutu na Waasi chini ya Laura Kabila may 2,1997 wiki 2 kabla ya rais Mobutu kupinduliwa na Waasi wakiongozwa na Laura Kabila.

Utaona hapo Mobutu alikuwa tayari ameshajichokea kwa maradhi ya saratani ya tezi dume huku akisaidiwa kushikwa mkono na Rais Mandela na kumsaidia kuketi kwenye kiti.
Ilitegemewa baada ya kikao hiki Rais Mobutu angetangaza kujiuzulu lakini alikaidi, na hii ilitokana na hulka yake ya ubabe na kiburi.

Mobutu alifariki miezi minne baadae(september) ukimbizini Jijini Rabbat, Morocco.

Afrika iliwahi kupata viongozi wa mkono wa chuma sana hapo nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…