JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Nani huyu
Majeruhi wa mjumbe
20200720_200050.jpg
 
Napata hisia za ajabu kwenye hizi picha..ni kama nilikuwepo huko miaka hiyo ya zamani[emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
Hata mimi mkuu kuna picha hapo juu wanafunzi wanapiga ngoma duu yani Kama napajua ivi.
 
Umenikumbusha mbali kidogo kwa picha hii, na hii ilipigwa ndani ya manowari ya kijeshi ya Jeshi la Afrika kusini wakati wa kikao maalumu cha usuluhishi kati ya Serikali ya Zaire chini ya Rais Mobutu na Waasi chini ya Laura Kabila may 2,1997 wiki 2 kabla ya rais Mobutu kupinduliwa na Waasi wakiongozwa na Laura Kabila.

Utaona hapo Mobutu alikuwa tayari ameshajichokea kwa maradhi ya saratani ya tezi dume huku akisaidiwa kushikwa mkono na Rais Mandela na kumsaidia kuketi kwenye kiti.
Ilitegemewa baada ya kikao hiki Rais Mobutu angetangaza kujiuzulu lakini alikaidi, na hii ilitokana na hulka yake ya ubabe na kiburi.

Mobutu alifariki miezi minne baadae(september) ukimbizini Jijini Rabbat, Morocco.

Afrika iliwahi kupata viongozi wa mkono wa chuma sana hapo nyuma.
Uko vizuri Sana kwenye historia.
Leo naomba unipe historia ya Thomas Sankara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ongeza nyama kidogo mkuu
Mkuu,huyu ni Fred Rwegima,Mnyarwanda aliezaliwa na kukulia ukimbizini Uganda,akajifunza vita vya msituni Tanzania,(inasemekana eye ndo aliemshika Paul Kagame mkono mpaka kwa M7 aliekuwa masomoni UDSm),wakaanza Vuguvugu la kuikomboa Uganda, akashika nyadhfa mbali mbali ktk Jeshi la Uganda,lkn Baadae akaona kuna haja ya kuikomboa tena Nchi yake ya Asili Rwanda,wakiwa na kundi la kijeshi la wakimbizi wa kinyarwanda kutoka Uganda wakaivamia Rwanda...huko ndiko uhai ulikomtoka...kifo chake ndio kilichofanya Major General P kagame kukatisha masomo na kurudi kuendeleza harakati....Ni shujaa wa nchi ya Uganda na Rwanda kwa pamoja.
 
Ooh[emoji122]
 
Back
Top Bottom