JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

FB_IMG_1667864624829.jpg
 
RAY C....Rehema Chalamila, huyu ni msanii wa Bongo flavour kutoka Iringa, amezaliwa 1982...alianza muziki 2001 na ameshinda TUZO za kimziki zaidi ya saba..ikiwemo... Tanzania music wards 2007 .Amepotea kidoogo kwenye ulingo wa burudani..lakini juzi ametuarifu ya kwamba , makubwa yanakuja....tusubiri tu...
FB_IMG_1669711669348.jpg
 
YUPO WAPI MTOTO WA PABLO ESCOBAR—MANUELA ESCOBAR!!?
#UZI
[emoji100]Japo vitabu vya Kihistoria vinamtaja Manuela Escobar kama ndiye aliyekuwa mtoto pekee wa kike wa "The King of Cocaine", Pablo Escobar, Maisha yake ya sasa ni tofauti kabisa na maisha ambayo labda baba yake angetaka yawe
20221129_114957.jpg
 
Japo kuzaliwa na kukulia katika familia ya ‘A notorious Colombian drug’, Pablo Escobar, kulimfanya Manuela kuionja ladha ya maisha mazuri tangu akiwa mtoto mdogo, lakini Kumekuwa na maswali Mengi sana juu ya maisha yake na wapi aliko mtoto huyo wa pekee wa gwiji, Pablo Escobar.
20221129_115052.jpg
 
Tangu kuuawa kwa baba yake Manuela, Yaani Pablo Escobar, mwaka ule wa 1993 pindi Manuela alipokuwa na Miaka 9 Mpaka Leo hii, Ni Manuela pekee kutoka kwenye ile familia ya Pablo ambaye hajawahi kutuhumiwa kwa kosa lolote lile, Kisheria.
20221129_115222.jpg
 
Manuela alizaliwa Mwaka 1984, kipindi ambacho jina la baba yake hususani katika ulimwengu wa biashara haramu za madawa ya kulevya, lilikuwa likiimbwa kila kona ya dunia hii.
20221129_115330.jpg
 
Katika Umri mdogo wa Manuela, ndipo kulikua na ukubwa wa jina la baba yake katika biashara za kuuza Cocaine,hivyo nitakuwa sahihi kama nitasema kuwa,Manuela hakuwa akijua ni nini baba yake anakifanya kwa ajili ya maisha, ila alichokuwa akijua ni kuwa chochote atakachoomba atapewa
20221129_115420.jpg
 
Inaaminika pamoja na u-nunda wake wote Pablo, hususani katika biashara zake za Cocaine, Pablo alikuwa anakuwa Mwepesi sana linapokuja suala la Manuela.

Hata katika kilele cha Makusanyo ya pesa ya Pablo Pale kwenye genge lake la Medellín Cartel, Pablo alikuwa tayari kutoa kiasi kwa ajili ya kitu chochote ambacho Manuela angehitaji.

Hata wakati Mshike mshike kati ya Pablo na Mamlaka za Ulinzi na Usalama za Colombia Umeanza, Pablo alikuwa yupo tayari Kufanya chochote ili familia yake iwe salama, hususani Binti yake Manuela.
20221129_115516.jpg
 
Kwa Mfano, Miaka ya 90’s Mwanzoni, wakati familia yake imejificha kule katika safu za milima ya Colombia ili kuepuka kuonekana na Polisi wa nchini humo, Pablo aliteketeza ‘$2 Million in cash’ ili tu… Manuela apate Joto, Maana baridi ilikuwa kali sana.
20221129_115723.jpg
20221129_115755.jpg
 
Baadae Pablo aligundua kuwa, Familia yake isingeendelea kuwa salama kama angeendelea kubaki nayo kwa Karibu, hivyo alimuamuru Mkewe Maria Victoria Henao, awachukue watoto wake na kisha akaishi nao katika ‘Safe House’ fulani hivi ili kuepuka Madhira ambayo yangewagika kutokana na,kuendelea kubaki Karibu na Pablo.

Na hatimaye, December 1993, Pablo Escobar died just as violently as he lived.
20221129_115854.jpg
20221129_115919.jpg
 
Kifo cha Pablo hakikuwa mwisho wa kila kitu, hususani katika familia ambayo ubini wake ilikuwa ni ‘Escobar’.

Baada tu ya kifo cha Mzee wao, Familia Nzima ya Marehemu Mzee Pablo Escobar, yaani Manuela Escobar, kaka yake Juan Pablo, na mama yao Maria Victoria Henao, wakahama nchi
Walijua kuwa, baba yao alikuwa ameshatengeneza maadui wengi sana katika ardhi ya Colombia ambao wangeweza Kuwatafuta wao kwa ajili ya kujilipizia Kisasi, hivyo wakaamua kutafuta makazi katika Nchi nyingine.
20221129_120042.jpg
 
Walitafuta Makazi katika nchi kama Mozambique, South Africa, Ecuador, Peru, na Brazil, kabla ya kuja kukita kambi katika nchi ya Argentina Mwaka 1994, huku wakitumia majina yasiyokuwa yao kabisa kabisa.

Mama Mtu akawa Victoria Henao Vallejos badala ya Maria Victoria Henao,

….kukosa ushahidi.

Lakini, Mbona Hata Kizimbani walionekana kaka mtu na mama Mtu, swali kubwa katika watafiti wa mambo likawa ni “Where in the world was Manuela?”

Katika makala iliyoandikwa katika tovuti moja ya chombo cha habari cha kule Colombia kifahamikacho kama El Tiempo,

….kukosa ushahidi.

20221129_120158.jpg
20221129_120228.jpg
 
Ikafichuliwa kuwa, Manuela Escobar kwa sasa alikuwa akitumia jina la “Juana Manuela Marroquín Santos” huko Buenos Aires Nchini Argentina.

Ikasemekana Kuwa,Manuela kwa sasa alikuwa aliishi katika nyumba moja ya kupanga iliyopo katika jengo lililokuwa likifahamika kama
Jaramillo

Wengine wakasema, alikuwa akiishi na kaka yake, na hao wote walikuwa wakiendelea kuyala mabaki ya mabilioni ya fedha alizokuwa amezitengeneza baba yao kupitia biashara zake za Cocaine enzi za uhai wake.

Lakini uhalisia ikawa ni kuwa, Manuela alikuwa akijaribu kuishi maisha ya,chini sana ili asijulikane kuwa alikuwa ni mtoto wa Pablo, na hii ilikuwa ni kwa manufaa ya usalama wake.

Kwasababu ya kuhofia kuwa maadui wa baba yake labda wangemtafuta ili kulipa kisasi, Manuela alipata mpaka tatizo la Msongo wa Mawazo.
20221129_120550.jpg
20221129_120533.jpg
20221129_120528.jpg
 
Kaka yake na mama yake, walijitokeza hadharani na hata wakaandika vitabu kila mmoja juu ya maisha yao na Mzee Escobar yalivyokuwa enzi za uhai wao, ila Manuela hakuwahi kufanya hivyo.

Inaaminika, bado amekuwa akijificha ficha sana, japokuwa hajawahi hata kufanya uhalifu wowote.
20221129_120702.jpg
 
Kwa mujibu wa Kaka Yake Manuela, Yaani Juan Pablo (ambaye kwa sasa anafahamika kama Sebastián Marroquín), aliwahi kukiri kuwa Manuela ameshawahi hata kujaribu kujitoa uhai wake, kutokana na Msongo wa Mawazo.

Inasemekana kwa sasa, Manuela anaishi na Kaka yake huyo (ambaye ameoa)
20221129_120933.jpg
 
Back
Top Bottom