JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Marangu
3b0a08d6a3ba319c4db7fc5272af22a8.jpg
 
HEMEDI MOUSSA MAHIZA KIPA MAHIRI ENZI ZAKE. ALIDAKIA AFRICAN SPORTS YA TANGA, RELI MOROGORO(Alikokua akifqnyia kazi) ALISHACHAGULIWA TIMU YA TAIFA YA VIJANA MARA KADHAA..... WAHENGA MNAMKUMBUKA???
FB_IMG_1683390742108.jpg
 
Marehemu REMMY ONGARA wimbo ambao ulitambulisha kwenye muziki ulikuwa siku ya kufa wa bendi ya makassy
Mawazo mawazo ya mutu muzima kama akikwambia neno ..usibishe
Neno la muzee ukibisha bure unapata shida.
FB_IMG_1683391146991.jpg
 
Miaka ile baadhi ya mwanamuziki wa bendi ya Empire Bakuba ilipotembelea bendi ya maquis
Kutoka kushoto PAPII TEX
MAREHEMU MOBALI JUMBE
ASSOSSA
MAREHEMU PEPE KALLE
MAREHEMU MAFUMU BILALI
FB_IMG_1683391246892.jpg
 
Huyu ni marehemu TUNGARAZA
ALICHEZEA SIGARA BAADAYE YANGA
Jina lake la utani aliitwa bolizozo alipewa baada ya kuifunga simba
FB_IMG_1683391327787.jpg
 
Huyu jamaa alikuwa staa wetu wakati tunaangalia vikundi vya utamaduni enzi zile
Jina lake aliitwa AMRI ATHMANI
JINA LA USANII MZEE MAJUTO
sisi wakati tunamuona aliitwa KING MAJUTO
mzee alikuwa anajuwa kwenye maigizo yake ambayo wewe unaweza kulia na nyimbo zake zenye kusikitisha asante sana king umetufurahisha enzi zetu ukiwa na makundi DDC KIBISA,BANTU,UJAMAA NA TOT
FB_IMG_1683391421324.jpg
 
John Steven Akhwari ni mwanariadha mstaafu. Alizaliwa mwaka 1938 kule Mbulu- Mkoani Manyara. Aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic mwaka 1968 nchini Mexico, katika mashindano ya riadha ya kilomita 42. Washiriki walikuwa 75, lakini waliomaliza shindano ni 57 pekee, huku John Steven Akhwari akimaliza wa mwisho kabisa.
Kwa nini alimaliza wa mwisho? Baada ya mbio kuanza, walipofika kilomita ya 19, mshiriki mojawapo alimparamia, kumsukuma na kuanguka vibaya mno. Aliumia begani, na goti la mguu wa kulia lilitenguka. Gari la huduma ya kwanza lilimfikia na kumpa matibabu, akaweza kusimama tena na kuendelea na riadha.
Umaarufu wake duniani . Watu waliomhudumia walimlazimisha kuaihirisha shindano na apande kwenye gari lakini alikataa katakata. Aliendelea na riadha huku akichechemea. Alifanikiwa kumaliza kilomita zote 42, jioni ya saa 1 kwa saa za Mexico. Watu wachache waliokuwa wamebakia uwanjani walimshangilia sana.
Mwishoni kabisa, waandishi wa habari walimuuliza, Kwa nini aliendela kukimbia ili hali ameumia kiasi hicho? Aliwaambia Nchi yangu Tanzania haikunituma maili 5000 kuja Mexico kuanza hili shindano bali walinituma kumaliza shindano.
Katika mashindano ya Olimpic na mpaka hivi leo Bwana John Stephen Akhwari anatambulika kama
'The Greatest Last- Place Finish Ever' . Japo hakushinda tuzo yoyote lakini ameonyesha uvumilivu, ujasiri na wenzetu wamekuwa wakimtumia kufundishia watoto na vijana wao kwamba they must struggle to finish the race, not just to start it.
Kwa bahati mbaya sana, watanzania walio wengi hawamjui. Huyu ni mfano wa kuigwa, ilistahili kauli yake hiyo ingekuwa nukuu muhimu kwa vijana wetu.
John Stephen Akhwari - Inspirational Story - Athslife
John Stephen Akhwari - Wikipedia
FB_IMG_1683391619913.jpg
FB_IMG_1683391625198.jpg
 
ALIKUWA MCHEZAJI WA KIUNGO KATIKA TIMU YA PAN,YANGA
Marehemu MOHAMEDI YAHAYA ,"TOSTAO"
Aliwahi kuchezea timu ya yanga kids na timu ya kiwanda cha bia
Pia aliwahi kucheza mpira ulaya
FB_IMG_1683391844958.jpg
 
Back
Top Bottom