JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

CASTRATION OF SLAVES(KUHASIWA WATUMWA)
-Watumwa wengi waliopelekwa bara la Asia alitolewa maeneo yafuatayo:-
.Abisynia
.Darfur.
.Korodofan
. Zanzibar
.Na maeneo mbalimbali ya bara la Africa
N:B Masikitiko makubwa ni kufanyiwa vitendo vya Kuhasiwa/kukatwa viungo vyao vya uzazi pasina ganzi ili pelekea wengi wao kupoteza maisha kwa kupoteza damu nyingi sana na walifanya kwa kuwa wengi wa hao watumwa walipelekwa kuwa kama ma house girl na ma house boy na walinzi wa makasri ya kifalme.
-Mfamo mzuri ni huyo mwamba pichani anaitwa Moorish Eunuch alikuwa muhanga wa kukatwa nyeti enzi za biashara ya utumwa ulifanywa na Mwarab alifanya bega kwa bega na Mzungu.View attachment 2612366
Ukikatwa nyeti unajisaidiaje haja ndogo?
 
Mwaka 1982 vijana watano wa Tanzania wenye umri wa kati ya miaka 21 na 25-Mussa Memba, Mohamed Ali Abdallah na nduguye Abdallah Ali Abdallah, Mohamed Tahir Ahmed na Yassin Memba-walioteka ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATC) kisha wakailazimisha iende Nairobi, Kenya na baadaye Ulaya.
FB_IMG_1683469879208.jpg
 
Mathias alisafiri tarehe 26 Septemba 1983 kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza na basi la KAMATA na kulipa nauli shilingi 200 (angalia jina la tiketi). Mimi nilisafiri Agosti 1985 kutoka Kyela, Mbeya kwenda Dar es Salaam na basi la KAMATA na kulipa nauli shiligi 43. Hii ilikuwa ni nusu nauli, nauli kamili ilikuwa ni shilingi 86. Safari yetu kutoka Kyela ilianza saa 4 asubuhi, tulifika Dar es Salaam kesho yake saa 11 jioni. Mimi sikuhifadhi tiketi yangu, lakini niliyoiweka hapa nimeipata kwa Joel Wilson Msella.

Ili kupata shilingi 43 kwa ajili ya nauli yangu ilinibidi niuze maziwa mwezi mzima. Kila siku nilikuwa ninapeleka lita moja ya maziwa kwa mama mmoja aliyeitwa Ijeje aliyekuwa anaishi karibu na Misheni ya Roman Catholic. Nilifanya zoezi hilo mwezi mzima na mwisho wa mwezi nikalipwa pesa. Utaratibu ule ulikuwa unaitwa 'kipande'. Ilikuwa kila siku tunapeleka maziwa lakini tunachukua pesa mwisho wa mwezi.

Enzi zile ilikuwa mtoto akitaka pesa ilimlazimu kuifanyia kazi. Ilikuwa ama tuuze maziwa, au tuuze korosho. Maziwa na korosho vilikuwa ni ndani ya uwezo wetu lakini mpunga ni lazima kikaliwe kikao cha baba na mama ndio uuzwe. Kuuza maziwa kilikuwa kikao kati ya baba na mtoto ingawa mama ilikuwa lazima ajue. Lakini korosho ilikuwa ni nguvu yako kuokota.

Je, umewahi kusafiri na KAMATA, KWACHA au Railways miaka hiyo? Je, unajua kuwa serikali ndiyo iliyokuwa na makampuni ya usafiri? Je, unajua kuwa utaratibu wa watu binafsi kuanza kumiliki mabasi ulianza mwaka 1990 baada ya serikali kuacha kumiliki makampuni ya usafiri?
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?


Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 7 Mei 2023
FB_IMG_1683542380835.jpg
 
Le Groupe Loketo. Wanachama (L-R) Jean Baron(RIP) Aurlus Mabélé (RIP) Diblo Dibala Freddy de Majunga Marc Macaire Bendi hii ilitufurahisha kwa muziki wa soukous mapema miaka ya 90. Kiongozi wa bendi Aurlus Mabélé alipewa jina la "Mfalme wa Soukous".

FB_IMG_1683768179690.jpg
 
Huyu mjusi Kuna aina ukiwakuta kwenye miti ya Miembe dodo miarobaini .pamoja na michongoma walikuwa na vichwa vikubwa pamoja na shingo pana
Wahenga wanamtambua vyema
Lakini pi tuliwahi kuaminishwa kitu kuhusu huyu mwamba
Hasa sisi watoto wakiume unaambiwa akikukuta mtini
Ana Jambo lake
FB_IMG_1683769011059.jpg
 
Huyu ni marehemu TATU SAIDI KHAMIS MSENGI
AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1947
Na amefariki mwaka 2016
Jina la shakila ni jina la utani
Alianza kazi ya muziki wa taarabu kwenye miaka ya 60
Ametumikia bendi mbalimbali pale tanga akiwepo BLACK STAR BAADAYE LUCKY STAR ZOTE ZA TANGA BAADAYE JKT
TUNAKUMBUKA BI SHAKILA KWA MCHANGO WAKO KWENYE MUZIKI WA TAARABU
FB_IMG_1683788549218.jpg
FB_IMG_1683788551915.jpg
 
Back
Top Bottom