Rhz4567
JF-Expert Member
- Mar 16, 2018
- 4,893
- 6,599
Walio simama ndiyo wanaendelea kushika remote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walio simama ndiyo wanaendelea kushika remote
TBT: Diamond Platnumz akiwa form oneView attachment 2627472
Huu ni ukweli kwamba maisha hayana formula!Mjini njoo na akili. Mtumishi Mwamposa (kushoto) alipofika mjini akiwa mzee sasa kijana tu. View attachment 2612374
.wanziloshi wa kili music awardMtoto wa DanduView attachment 2591455
Alimaliza form four?TBT: Diamond Platnumz akiwa form oneView attachment 2627472
Kusema sema,hodi hodi na marafiki ni mipini ninayoendelea kuburudika kwayo mpaka sasa.CHUCHU SOUND NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.
Kado Cool
Jiji la Dar es salaam lilipata kukumbwa na Joto kali la muziki wenye mahadhi ya 'Mduara' mwanzoni mwa miaka ya 2000 pale bendi kali ya Chuchu Sound ilipokuwa ikitoa burudani ya muziki kupitia kumbi mbalimbali za burudani.
Chuchu Sound maarufu kama wazee wa 'Kuzima Moto ndani ya Jiji', watakumbukwa na wadau wengi wa muziki wa dansi kutokana na namna walivyochochea burudani ya muziki wa 'Mduara', muziki ulioonekana kupendwa na vijana wengi wa Jiji la Dar.
Bendi hii iliyoanzishwa na Mfanyabiashara, Yusuph Alley Chuchu (RIP), ilileta ushindani kubwa kwa bendi nyingi za muziki wa dansi nchini zikizokuwa zimeshika kasi jijini Dar es salaam mwanzoni mwa miaka hiyo ya 2000.
Pamoja na kuwepo bendi kadhaa zilizokuwa zikipiga vibao vya miondoko ya 'Mduara' kama The Kilimanjaro Band (Njenje), InAfrika Band (Mgema), Beta Musica (Bana Beta), Chuchu Sound walikuwa ndiyo wakali zaidi katika miondoko hiyo.
Chuchu ambayo maskani yake ilikuwa maeneo ya Mwananyamala Komakoma, inakumbukwa na wengi kutokana na kujaza kumbi nyingi za burudani pale inapotumbuiza, hali iliyopelekea kuwa gumzo kubwa jijini Dar.
Ukumbi wa Vatican City uliopo Sinza jijini Dar, ilikuwa ndiyo 'Ngome Kuu' ya bendi hiyo, pale ilipokuwa ikitoa burudani kila mwishoni mwa wiki na kufanya wapenzi wengi "kuduarika" kwa raha na burudani kiasi ambacho ni vigumu kupimika.
Sauti tamu za waimbaji Omari Mkali, marehemu Waziri Sonyo, Joniko 'Flower' Maua, marehemu Ladislaus Manyama, na Rapa asiyepimika na kusahaulika kirahisi, marehemu Mao Santiago ziliifanya Chuchu kuwa Chuchu Sound kweli.
Albamu zao tatu, ya kwanza ikiitwa "Kusema sema", ya pili ikipewa jina la "Hodi Hodi" na ya Tatu ikiitwa "Mkataa Pema" zinakumbukwa na wengi kutokana na namna vilivyoipa bendi hiyo mafanikio makubwa.
Vibao kadhaa kama 'Kusema sema', 'Sitishiki', 'Usione vyaelea', 'Marafiki', na vinginevyo vingi, vilitosha kabisa kuifanya bendi hiyo kuzima moto wa burudani uliokuwa ukiwaka kupitia bendi nyingine za muziki wa dansi.
Hapa ndipo bendi ya Chuchu ilipobatizwa jina la "The Fire Brigadiers" (Wazee wa Zimamoto) na kupelekea bendi nyingi kulazimika kufanya 'Mduara' japo kidogo, ili kukidhi kiu za mashabiki wao walioanza kuielewa mizuka ya Chuchu.
Wengi tunakumbuka gitaa mahiri la Solo la King Giovanni (RIP), Rhythm gitaa ikipigwa na George Choka sambamba na Bass gitaa likipigwa na Mbwana Mponda, hivyo kukamilisha safu nzima ya wapiga 'Mipini' wa kikosi hicho.
Kwa upande wa Kinanda, Ababuu Mwana Zanzibar alikuwa mahiri mno kupapasa keyboard, Tumba zilijuta kumfahamu Mohamed Kachumbari huku marehemu Gabby Katanga 'Yero Masai' na Mohamed 'Muddy' Terminator (RIP) wakizicharaza kwa ufundi mkubwa drums.
Kama Waswahili wasemavyo kuwa "Ivumayo Haidumu", msemo huu ukajitokeza kwenye bendi ya Chuchu Sound baada ya wanamuziki wake kuanza kuchomoka mmoja hadi mwingine kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kimaslahi.
Ndoano ya Kapteni John Komba, Mkurugenzi wa TOT ikawanasa wanamuziki Waziri Sonyo, na Gabby Katanga kuwafanya kuwa sehemu ya kikosi cha TOT na hivyo jinamizi la mikosi kuanza kuiandama Chuchu Sound.
Wakati Chuchu wakiendelea kujiuliza, mwimbaji Omari Mkali naye akajiondoa Chuchu na kwenda kuanzisha bendi ya Pamo Sound kitendo kilichoonekana dhairi kuifanya bendi hiyo kuchungulia kaburi.
Msumari wa mwisho ukapigiliwa na bendi ya Bambino Sound iliyokuwa ikiongozwa Banza Stone, baada ya kumnyakua 'keyboardist' Ababuu Mwana Zanzibar na Muddy Terminator na hivyo Chuchu Sound ikawa si Chuchu ile tena.
Tuna mengi ya kuzungumza yasiyokwisha pale tutakapoamua kuizungumzia Bendi ya Chuchu Sound tusimalize, lakini kwa leo itoshe tu kusema bendi hii ni moja kati ya bendi zitakazokumbukwa na mashabiki wengi.
Pamoja na maisha yake mafupi kwenye ulimwengu wa muziki wa dansi nchini, Chuchu Sound ilifanikiwa kuleta mapinduzi makubwa kupitia muziki wa 'Mduara'.
Hii imejionesha dhahiri baada ya bendi hiyo kufa kwa mtindo huo kushindwa kumpata mwingine aliyoumudu ikilinganishwa na enzi za Chuchu wazee wa "Zimamoto ndani ya Jiji".View attachment 2628661