JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

HUKO LUSHOTO KASKAZINI MWA TANZANIA LEO KATIKA HISTORIA

Mwaka 1896 Kampuni ya kikoloni ya serikali ya ujerumani ya Germany East Africa Plantation (Deutsche-Ostafrikanische Plantagenge Schellshaft) walianzisha shamba la majaribio ya kilimo cha kahawa kwenye eneo ambalo kwa sasa linajulikana kwa jina la Irente.

Mashamba mengine ambayo yalianzishwa kipindi hicho ni Gare, Maweni, Sakharani na Mazumbai. Kusudi lilikuwa ni kufanya jaribio la zao hili lakini kutokana na ukosefu wa usimamizi mzuri zao la kahawa lilitelekezwa mwaka 1914.

Baada ya Ujerumani kupoteza koloni lake kwa Mwingereza mwaka 1918 shamba hili lilimikiwa na raia kutoka Ugiriki, Bwana W.J Tamé. Na baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 shamba hili liliuzwa kwa Kanisa la Kilutheri Tanzania (Tanzania Lutheran Church).

Inasemekana neno Irente Farm lilitokana na kirai (phrase) "I rented a Farm" na hivyo jina Irente likatokana na jina "I rented". Kutokana na mazungumzo ya lugha ya kingereza wakati huo baadhi ya Waswahili walibadilisha "I rented" kuwa ‘Irente’.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ZAY B

Miaka ya 2000 kulikua na mwanadada machachali sana katika Bongo Fleva anaitwa Zay to tha B mwanadada GaiDI.

Mwanadada alikua anajitahidi sana kwa nyakati zake kwenye game na walikua mahasimu sana ma mwenzake Sista P.

Alitoa nyimbo maarufu Nipo Gado akishirikisha Kibra, na alikua na Album Mama Africa ambayo kwa nyakati zake pia ilihit sana.

Kipindi yeye yupo hot kwa upande wa kina dada ni Sista P tu ndio alikua wanasumbuana. So tunaweza sema ni moja ya waasisi wa ili game Tanzania.

Siku zimepita kimya, sijamsikia kwenye vyombo vya habari, social media wala story za vijiwe.

Last time alitoa wimbo wa Penzi la Teja ila naona haukupokelewa kiviile.so akala bati.
FB_IMG_1693963027022.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ndiyo kile kipindi Mabasi yanapaki Mnazi mmoja na Kisutu. Ilikuwa kwamba kama umechelewa ukakuta basi limeondoka, basi wewe ndugu yangu tafuta teksii (teksii nzima siyo mbovumbovu) uanze kulifukuzia hilo basi na ukifanya mchezo utakwenda kulipata pale Kibaha maili moja. Enzi za Isuzu na Nissan Diesel.
FB_IMG_1693965216873.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wangapi wanakumbuka shindano la ' Tusker project fame,lililovuma Sana kati kati mwa miaka ya 2000 chini ya udhamini wa Kampuni ya East African Breweries Limited?Wangapi wanamkumbuka mshiriki Mmoja maarufu Sana Kwa jina Hemed kutoka Dar Tanzania? View attachment 2669197

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Hemed ana uhusiano gani na hii picha ya mwamba na fisi wake 😆😆
 
Historia ya maisha ya Dk. Remmy Ongala yaelezwa kwamba mara alipozaliwa, wazazi wake walimuita Ramadhani Mtoro Ongala. Majina yake kamili alikuwa akiitwa Ramadhan Mtoro Ongala. Alizaliwa mwaka 1947 katika mkoa wa Kivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Familia yake iliishi katika eneo lililoitwa Kindu eneo ambalo halikuwa mbali sana kutoka mpakani na Tanzania.
Umaarufu wake ulizidi kung’ara mwaka 1990 alipotoa wimbo wa ‘Mambo kwa Soksi’ ingawa baadhi ya watu waliupinga kwa kusema kwamba haukuwa na maadili mema kwa jamii, ingawa kimsingi alikuwa anawaasa watu hususani vijana kutumia kondomu ili kuepukana na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Akiwa Super Matimila Dk. Remmy alitoka na nyimbo nyingi zikiwemo za ‘Bibi wa Mwenziyo’, ‘Kipenda Roho’, ‘Asili ya Muziki’ na ‘Ngalula’. Zingine ni pamoja na ‘Mwanza’, ‘Mama Nalia’, ‘Harusi’, ‘Hamisa’, ‘Mnyonge Hana Haki’, ‘Ndumilakuwili’ na ‘Mataka Yote’ ambazo zilimuongezea sifa kubwa Dk. Remmy kufuatia maudhui yaliyokuwa yakikidhi jamii.
Baadaye Dk. Remmy Ongala akaanza kusumbuliwa na maradhi ya kisukari iliyompelekea kuamua kuachana na muziki wa dansi kwa madai ya kwamba umejaa mambo mengi ya kishetani. Remmy akaokoka, akatubudu dhambi zake na akaanza kupiga muziki akimuimbia bwana.
Kabla ya kifo chake Dk. Remmy alitoa albamu yake ya Injili aliyooiita ‘Kwa Yesu Kuna Furaha’. Remmy alikuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha albamu yake ya pili, lakini mungu akampenda sana usiku wa kuamkia Jumatatu ya Desemba 13, 2010 nyumbani kwake Sinza. Eneo hilo alilokuwa akiishi lilipewa jina la ‘Sinza kwa Remmy’ kufuatia umaarufu wake alipokuwa hai.
FB_IMG_1693992998162.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom