JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

TUMKUMBUKE MWANAMUZIKI PEPE KALLE

Mnamo Novemba 30, 1951 katika Jiji la LeopordVille kwa sasa{KINSHASA} huko Kongo ya Mbelgiji kwa sasa {Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo} alizaliwa mtoto aliyepewa jina la Kabasele Yampanya.

Alikuwa mtunzi, mwimbaji wa muziki wa soukous na kiongozi wa bendi ya Empire Bakuba. Pepe Kale aka Tembo Jitu la Miraba Minne alikuwa bingwa wa miondoko ya soukous na kiongozi wa bendi ya Empire Bakuba, ambayo ilikuwa maarufu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Watanzania wengi tutaendelea kumkumbuka mwanamuziki huyu hasa wakati alipokuja nchini mwetu na kutikisa majiji ya Arusha, Dar es Salam na Mbeya.
Wakati wa ujio wake hapa Tanzania, Pepe Kalle ambaye sauti yake ilikuwa nyembemba na nyororo, alifuatana na wanamuziki akiwemo mipiga wa gita la besi Lofombo na waimbaji akina Papy Tax, Dilu Dilumona na Djo Djo Ikomo.
Pepe Kalle aliyefariki Novemba 28, 1998 kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 47.View attachment 2743695

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mwamba alikuwa na zaidi ya 200KG
 
Mchezaji wa timu ya kakakuona Sekilojo Chambua akiwa na Marehemu Abbas Gulamali kushoto na aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha Soka Tanzania FAT Marehemu Gerace Lubega
Ilikuwa mwaka 1992 wakati timu ya kakakuona ilipocheza fainali ya kombe la challenge na Uganda
FB_IMG_1694914169601.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
The legend Yvonne Chaka Chaka from South Africa.

Alizaliwa March 18, 1965. Meimbaji mashuhiri wa muziki mashuhuri wa Afrika Kusini, "kwaito." Moja kati ya nyimbo zake zimazopendwa zaidi ni wimbo wa UMQOMBOTHI wenye maneno ya kusindikiza "Be Proud to be African."

Wimbo huo wa Umqombothi (African beer) ni maalumu kwa ajili ya kujali vitu au mambo ya asili yako. Umqombothi ni kinywaji cha asili Afrika Kusini kinachotengenezwa na wenyeji.

Baada ya kufika wakoloni walipobaini ufundi wa Waafrika wa kutengeneza kinywani hicho, waliamua kupiga marufuku kwa mtu yeyote kujishuhulisha na biashara ya Umqombothi, kuanzia kutengeneza mpaka kuuza. Na kisha kufanya msako.

Kwenye ardhi ya Washona (sasa Zimbabwe) kiongozi mashuhuri, bwana Lobengula, alikuwa mnywaji mkubwa wa kinywaji cha asili kilichotengenezwa kwa mtama, halafu anasimdikizia na nyama choma. Wakoloni wakapiga marufuku pia. Sasa hivi uende baa utakuta mtu anakunywa bia na nyama choma pembeni. Hilo siyo geni, babu zetu Afrika walifanya hivyo kwa vinywaji vya asili.

Kinywaji cha Umqombothi kilisababisha mwimbaji Miriam Makeba aende gerezani akiwa na umri wa miezi michache ty tangu kuzaliwa kwake. Mama yake alikutwa mtaani akiuza kinywaji hicho ili kupata hela ya kujikimu na kichanga chake. Akatandikwa rungu na polisi na kukamatwa kwa kosa la kujihusisha na biashara ya Umqombothi. Alienda gerezani na kichanga chake.

Miriam Makeba alikuja kuwa mwanamuziki mashuhuri Afrika Kusini kama ilivyo kwa Yvonne Chaka Chaka.

Wema dlamini
Uph'mqombothi........
FB_IMG_1694914515225.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ilikuwa Timu ya Yanga ikicherekea ubingwa wa afrika mashariki na Kati waliochukua katika nchi ya Uganda 1999
Yanga ilichukua ubingwa huu tarehe 16-1-1999 baada ya kuifunga timu ya Villa ya Uganda kwa penalty
Yanga na villa walifungana mabao 1-1 katika dakika 90
Mabao yalifungwa na Hassan Mubiru wa villa dakika ya 7
Na Yanga alifunga Edibily Lunyamila dakika 42
Ikaja sehemu ya penalty Yanga ikashinda penalty 4 kwa penalty 2
Penalty za Yanga zilifungwa na Shaban Ramadhani
Edibily Lunyamila
Sekilojo Chambua
Ally Mayai
List ya Yanga kwenye mechi hiyo ilikuwa hivi Peter Manyika
Eustace Bajwala
Anwar Awadh /&Mzee ABDALLAH
Bakari Malima
ALLY Mayayi Tembele
Shaban Ramadhani
Sekilojo Chambua
Salvatory Edward/& Iddi Moshi
Mohamedi Hussein mmachinga /& Akida Makunda
Kalimangonga Ongala
Edibily Lunyamila
FB_IMG_1694914748860.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi hizo, hapo ni mkoa wa Mbeya. Kuna gari limepata ajali katikati ya barabara na juhudi za kulitoa zikiwa zinafanyika kwa kutumia break down hiyo nyekundu. Huku nyuma kuna basi likiwa linasubiri zoezi hilo liishe liweze kupita na nyuma kwa mbaali naiona FORD ANGLIA nayo ikisubiri kupata upenyo iweze kuendelea na safari yake. Kipindi hiki watu waliishi kama ndugu, ilikuwa hata kama gari lako limeharibika, basi wanakijiji wanakuhudumia kwa kila kitu mpaka gari lako litakapo tengemaa, wanakuchinjia na Jogoo Mkubwa.
FB_IMG_1694914841499.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ilikuwa mwaka 1993 kipindi hicho kikundi hiki cha Bima taarabu kipo kwenye ubora wake
Unawakumbuka wasanii waliopitia kikundi hiki
Marehemu Ally Tajiruna
Marehemu Mbwana Tajiri
Ally Hemed ukipenda Ally Star
Marehemu Mariam Nailon
Chausiku Salum ukipenda Bi chau
Marehemu Seba Juma
Maigizo alikuwa Marehemu kashata
Mkude
Bi zainabu
Bandubandu
Nyonganyonga
Marehemu minyugu
Marehemu Small
Branco wa chitosa
Kama mhenga unakumbuka endelea
Na nyimbo zao mzuri sana
Je nyimbo zipi unazikumbuka toka Bima taarabu
FB_IMG_1694915009480.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom