JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Nani anakumbuka hizi chuma (mbaula)
FB_IMG_1697121038932.jpg
FB_IMG_1697121035813.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaitwa Michel Qissi ni Mbeligiji mwenye asili ya Morocco,huyu jamaa alizaliwa 12'Septemba'1962 huko Oujda, Morocco
Na ana uraia wa Nchi mbili yaani Belgium and Morocco
Alizaliwa kwa jina la Mohammed Qissi
Alitoka Morocco na kuelekea Blussels Ubeligiji pamoja na wazazi wake akiwa na umri wa miaka 2
Akiwa na miaka 7 alianza mafunzo ya boxing na baada ya muda akaongeza ujuzi wa Shotokan Karate na Muay Thai pamoja na Kickboxing baada ya hapo akawa rafiki mkubwa wa Jean Claude Van Damme na pia katika makuzi walikuwa pamoja na waliishi kwa kupendana sana na walitamani kwa mapenzi yote siku moja waje kuwa nyota katika filamu za mapigano
Na ndipo wakaanza mafunzo ya Martial arts wakiwa pamoja
Na ulipofika mwaka 1982 Qissi na Damme wakiwa na matumaini ya kutokata tamaa wakafunga safari mpaka United States of America.
Na mwaka 1984 wote kwa pamoja walishiriki kwenye filamu iliyoitwa Breaking wakiwa washiriki wa nyongeza
Baada ya hapo wakapata kwa mkataba kwenye kampuni ya Cannon Films Group ambazo ni tatu wakianza na Bloodsport huku Qissi alishiriki kama muigizaji mdogo katika mapambano na kwenye Bloodsport alitumia jina la Suan Paredes
Ulipofika mwaka 1989 Qissi na Damme wakarudi tena na kitu ikiitwa Kickboxer Van Damme (Kurt Sloan) akicheza kama staringi na Qissi (Tong Poo) akicheza kama adui
Na ilipofika mwaka 1990 wakarudi na kitu ya kuitwa Lionheart (A.W.O.L) filamu ambayo Qissi aliigiza na kaka yake ambaye alicheza kama adui yule jamaa anayepigana na Van Damme mwishoni jina lake ni Abdel Qissi na humo kwenye hiyo filamu alitumia jina la Attila
Ila tambua hiyo Lionheart ndio ilikuwa move ya mwisho kwa Qissi na Damme kushiriki kwa pamoja,ila Qissi aliendelea kushirki kwenye muendelezo wa Kickboxer 2,3,4 zitafute umuone humo.
Qissi na Damme wameshiriki filamu nne nazo ni
Breaking (1984)
Blood sport(----)
Kickboxer (1989)
Lionheart (1990)... MOHAMMED QISSI MICHEL QISSI
TONG POO.
FB_IMG_1698284466558.jpg
FB_IMG_1698284463150.jpg
FB_IMG_1698284459699.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiwanja cha ndege Dar es salaam Terminal 1 mnamo miaka ya 1950. Wakati huo Tanzania bado ikiitwa Tanganyika. Kiwanja hiki kilijengwa na Muingereza ambaye hakutaka kabisa kuendelea kutumia kile kiwanja cha ndege kilichojengwa na Mjerumani kule maeneo ya Kurasini, yaani lile eneo zima la JKT Mgulani, Jeshi la Wokovu, Temeke Wailesi, Uwanja wa Taifa mpaka pale mtoni kwa Azizi Ally. Na hii kweli ilikuwa zamani hasa, sababu hapo sioni Peugeot 403 wala 404, yaani ukifika hapo kiwanjani unajiona wewe tu.
FB_IMG_1698638741992.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha mbili tofauti (zamani na sasa) za Leleti Khumalo mwigizaji toka Afrika Kusini, alizaliwa tarehe 30 Machi 1970 kwa sasa ana umri wa miaka 53. Wengi tunamfahamu kwa jina la Sarafina kutokana na movie maarufu aliyoshiriki ya enzi za ubaguzi wa rangi iliyoitwa SARAFINA!
Unakumbuka nini kuhusiana na movie ya Sarafina? Mimi kuna baadhi ya matukio yalinitoa machozi na kunifanya niwachukie sana wabaguzi wote wa rangi
FB_IMG_1698641325007.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom