JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

JF Photo Library: Mada maalum ya Picha za Zamani

Hawa ndiyo wanzilishi kwa kundi la Mambo hayo
Philip Njaidi ukipenda Sumbi
Paschal ukipenda unamwita bocha
Wakiwa na msichana kipindi hicho Aisha baadaye akaja waridi
Walifurahisha na michezo yao kwenye TV
Wenyewe tuliwaita Sumbi na Bocha
Wale wahenga wanakumbuka michezo yao
Sumbi kwa Mara ya mwisho nilisikia yupo Sweden
Bocha sijui yupo wapi?
FB_IMG_1698641423964.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika wasanii wenye kipaji cha kuigiza vizuri sana huyu naye yumo
Anaitwa Julieth Samson jina la usanii anajulikana kama KEMMYenzi ya kaole Sanaa group

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka 105 iliyopita mnamo Novemba 21 mwaka 1916 meli kubwa inayoitwa BRITANNIC ambayo inasadikiwa kuwa ni mdogo wake na meli ya TITANIC pomoja na meli ya OLYMPIC kwasababu zote zilitengenezwa kwenye kizimba kimoja cha BELFAST. meli ya BRITANNIC ilipata ajali ya kutikiswa na mlipuko wa bomu la aina ya torpedo lililolushwa kutoka kwenye manuali ya kijeshi kwenye vita vya kwanza vya dunia) utofauti pekee kuwa meli ya TITANIC ilizama katika bahari ya Atlantic mwaka 1912 na meli ya BRITANNIC ilizama katika bahari ya pacific Novemba 21 mwaka 1916))
FB_IMG_1698642576000.jpg
FB_IMG_1698642582293.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
SCANIA 93F "SPECIAL SLEEPING COACH" katika ubora wake ikiwa na bonge la ngao mbele na jamaa kakaa juu yake. Hata hivyo serikali ilikuja kuzuia hizo ngao baada ya kugundua kwamba kuna madereva wengine kama mimi walikuwa wanayagonga na kuyatisha magari mengine ambayo hayakuwa na ngao kubwa mbele kama hiyo, hasa magari madogo madogo. Huyu Muhenga alifanya kazi nzuri sana Dar Njombe Songea na pia mikoa ya kusini Lindi, Nachingwea, Mtwara. Scania 93F kwa kipindi hiki ndiyo ilikuwa homa ya jiji ukiondoa Scania 113K injini nyuma ambayo ilikuwa haikamatiki ama haina mpinzani. Ogopa sana mabasi yaliyosajiliwa kipindi hicho yakiwa na namba TZE, TZK, TZL & TZM na hicho ndiyo kipindi yule dereva Giriki alikuwa hakamatiki. Karibu sana.
FB_IMG_1698643429720.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka 46 iliyopita, yaani mwaka 1978, tarehe kama ya Leo 26, Oktoba, majeshi ya Iddi Amin Dada yalirusha risasi ya kwanza katika ardhi ya Tanzania, kule Kagera katika shambulizi la ghafla. Vita ya Kagera ikaanza rasmi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matema Beach SCANIA 113K HP310, A.K.A BUSTAR, Injini Nyuma, ifuate upotee, Ilikuwa haikamatiki enzi zake hasa kwenye milima, ikitangulia imetangulia, ni hatari tupu. Ni kampuni chache sana ndizo zilipata kumiliki Toleo hili la Scania, baadhi ni MATEMA BEACH, ABOOD, KISWELE NA AIR MSAE. Karibu sana.
FB_IMG_1698643664757.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
BUHAYA OKASHEMELA!

MHARIRI NA MZALENDO EDWARD R. MUNSERI
Mwandishi na mwanaharakati na muasisi wa umoja wa kitaifa dhidi ya ukabila na mwandishi nguli wa magazeti ya,
"BUKYA NA GANDI", "BAHAYA TWEMANYE."
Mnamo mwaka 1952, mjini bukoba kulianza kuchapichwa gazeti la kizalendo la Bukya na Agandi, ambandi mhariri wake alikuwa ni Mhaya wa bukoba Edward R, Munseri ndani ya Lake province.

Gazeti hilo lilichapichwa kwa kila wiki Mara moja( kwa wiki lilitoka Mara moja), lilichapichwa kwa kihaya, kiswahili na kingereza( gazeti hilo moja,lilichapichwa kwa kutenga sehemu ya kihaya,sehemu ya kiswahili na sehemu ya kingereza), Hivyo yeyeto angeliweza kulisoma gazeti hilo kwa lugha ambayo angeliipenda yeye.
Kwa kipindi hicho,Edward Munseri ndiye aliyekuwa mwana habari (mhariri wa habari msomi kwa kipindi hicho) katika Tanganyika, alisomea Uganda na kuajiliwa katika ofisi ya taarifa ya selikali ya kikoloni ya Waingereza mjini Kampala nchini Uganda.Baada ya miaka kadhaa aliamua kurudi Tanganyika na kuajiriwa kama mhariri msaidizi wa gazeti la Habari za Leo na gazeti la Mambo Leo kabla ya kuamua kuacha kazi na kurudi Bukoba kuanzisha gazeti lake la Bukya na gandi.

MADHUMUNI YA KUANZISHA GAZETI LA BUKYA NA GANDI:

Aliwahi kusema kuwa, nia ya kuanzisha gazeti huru hilo la BUKYA NA GANDI ilikuwa ni kupambana na UKABILA ndani ya Buhaya.Alihitaji Abahaya wote kuugana na kuwa wamoja ili kuondoa ukabila wa Abaziba,Abanyambo, Abayoza, Abaamba, Abahiyangilo na makabila mengine ndani ya Buhaya ili kujiandaa kuutaduta Uhuru wao wote kama Wahaya dhidi ya Ukoloni wa Mwingereza. Ajenda hii ya Umoja ilionekana kwa Wahaya na baadae kukua na kusambaa na kuwa ajenda kubwa katika viongozi wa TANU ambapo waliiona kuwa ajenda ya kuliunganisha Taifa zima la Tanganyika na kuondoa ukabila na kuleta uzalendo wa umoja kama Utanganyika.

Sera ya umoja ilianzia buhaya na baadae taifa likawa bila ukabila na kupambania Uhuru dhidi ya utawala wa kikoloni. Gazeti hilo la BUKYA NA GANDI liliwa maarufu na lilipendwa sana na watu,na uchapishwaji wake uliongezeka Kutoka nakala 1,000 mnamo mwaka 1952 na kufikia nakala 3,000 mnamo mwaka 1955.

Umaarufu wa BUKYA NA GANDI ulimfanya kuamua kuanzisha kuchapa gazeti lingine ambalo lilichapishwa Mara moja kwa mwezi ambalo alilipa jina la ABAHAYA TWEMANYE ambalo lilichapishwa kwa kihaya tuu likihimiza juu ya Maendeleo ya Abahaya,mila na desturi zao.
FB_IMG_1698643733970.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ni kikosi Cha Yanga kilichokua ubingwa wa Afrika mashariki na Kati kule Zanzibar mwaka 1975
Kikosi kiliongozwa na kocha Marehemu Tambwe Leya aliyesimama upande wa kushoto
Anayefata ni Leodgar Tenga
Patrick Nyaga
Juma Shaban
Marehemu Selemani Sanga
Marehemu Gibson Sembuli
Waliokaa kuanzia kushoto Marehemu Omari Kapera
Marehemu Muhaji Mukhi
Sunday Manara
Ahmed Omari
Juma Matokeo
Jella Mtagwa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki ni kikosi Cha Yanga kilichokua ubingwa wa Afrika mashariki na Kati kule Zanzibar mwaka 1975
Kikosi kiliongozwa na kocha Marehemu Tambwe Leya aliyesimama upande wa kushoto
Anayefata ni Leodgar Tenga
Patrick Nyaga
Juma Shaban
Marehemu Selemani Sanga
Marehemu Gibson Sembuli
Waliokaa kuanzia kushoto Marehemu Omari Kapera
Marehemu Muhaji Mukhi
Sunday Manara
Ahmed Omari
Juma Matokeo
Jella Mtagwa
FB_IMG_1698643926616.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zamani wakati tunakua ukienda sokoni ukiangalia kwenye majalala utakuta kuku waliokufa wametupwa jalalani

siku hizi ukienda sokoni kuku hawaonekani! je siku hizi kuku awafi?
Je Kama wanakufa wanaenda kutupwa wapi?
FB_IMG_1698644265750.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom