BUHAYA OKASHEMELA!
MHARIRI NA MZALENDO EDWARD R. MUNSERI
Mwandishi na mwanaharakati na muasisi wa umoja wa kitaifa dhidi ya ukabila na mwandishi nguli wa magazeti ya,
"BUKYA NA GANDI", "BAHAYA TWEMANYE."
Mnamo mwaka 1952, mjini bukoba kulianza kuchapichwa gazeti la kizalendo la Bukya na Agandi, ambandi mhariri wake alikuwa ni Mhaya wa bukoba Edward R, Munseri ndani ya Lake province.
Gazeti hilo lilichapichwa kwa kila wiki Mara moja( kwa wiki lilitoka Mara moja), lilichapichwa kwa kihaya, kiswahili na kingereza( gazeti hilo moja,lilichapichwa kwa kutenga sehemu ya kihaya,sehemu ya kiswahili na sehemu ya kingereza), Hivyo yeyeto angeliweza kulisoma gazeti hilo kwa lugha ambayo angeliipenda yeye.
Kwa kipindi hicho,Edward Munseri ndiye aliyekuwa mwana habari (mhariri wa habari msomi kwa kipindi hicho) katika Tanganyika, alisomea Uganda na kuajiliwa katika ofisi ya taarifa ya selikali ya kikoloni ya Waingereza mjini Kampala nchini Uganda.Baada ya miaka kadhaa aliamua kurudi Tanganyika na kuajiriwa kama mhariri msaidizi wa gazeti la Habari za Leo na gazeti la Mambo Leo kabla ya kuamua kuacha kazi na kurudi Bukoba kuanzisha gazeti lake la Bukya na gandi.
MADHUMUNI YA KUANZISHA GAZETI LA BUKYA NA GANDI:
Aliwahi kusema kuwa, nia ya kuanzisha gazeti huru hilo la BUKYA NA GANDI ilikuwa ni kupambana na UKABILA ndani ya Buhaya.Alihitaji Abahaya wote kuugana na kuwa wamoja ili kuondoa ukabila wa Abaziba,Abanyambo, Abayoza, Abaamba, Abahiyangilo na makabila mengine ndani ya Buhaya ili kujiandaa kuutaduta Uhuru wao wote kama Wahaya dhidi ya Ukoloni wa Mwingereza. Ajenda hii ya Umoja ilionekana kwa Wahaya na baadae kukua na kusambaa na kuwa ajenda kubwa katika viongozi wa TANU ambapo waliiona kuwa ajenda ya kuliunganisha Taifa zima la Tanganyika na kuondoa ukabila na kuleta uzalendo wa umoja kama Utanganyika.
Sera ya umoja ilianzia buhaya na baadae taifa likawa bila ukabila na kupambania Uhuru dhidi ya utawala wa kikoloni. Gazeti hilo la BUKYA NA GANDI liliwa maarufu na lilipendwa sana na watu,na uchapishwaji wake uliongezeka Kutoka nakala 1,000 mnamo mwaka 1952 na kufikia nakala 3,000 mnamo mwaka 1955.
Umaarufu wa BUKYA NA GANDI ulimfanya kuamua kuanzisha kuchapa gazeti lingine ambalo lilichapishwa Mara moja kwa mwezi ambalo alilipa jina la ABAHAYA TWEMANYE ambalo lilichapishwa kwa kihaya tuu likihimiza juu ya Maendeleo ya Abahaya,mila na desturi zao.
Sent using
Jamii Forums mobile app