Kufanya mazoezi huimarisha mwili na ogani zake kama moyo. Mazoezi humuepusha kuwa na uzito kupita kiasi, huzuia maradhi ya moyo na kupanda kwa shinikizo la damu na kuboresha kumbukumbu na utendaji mzuri wa ubongo/akili
Kutembea na kuendesha baiskeli hukupa fursa ya kufanya mazoezi bila kuhitaji muda maalumu wa kufanya mazoezi. Kuendesha baiskeli kwa saa 1 kila siku kwa siku 7, hukusaidia kuchoma nusu kilo ya mafuta kutoka katika mwili wako
Kuendesha baiskeli kwa saa 1 kila siku kwa siku 7, hukusaidia kuchoma nusu kilo ya mafuta kutoka katika mwili wako. Mwendesha baiskeli ana moyo imara unaofanya kazi kwa ufanisi, kuliko mtumiaji wa gari au pikipiki
Kula mlo kamili na kufanya mazoezi husaidia mwili kutonenepa kupita kiasi. Unene kupita kiasi huhusishwa na hatari ya kupata maradhi kama Kisukari, Kupanda kwa Shinikizo la Damu, Magonjwa ya Moyo, Saratani n.k.
Mambo matano rahisi yanayoweza kukufanya uwe na furaha:
1~ Kutafakari (Meditation),
2~ Kutabasamu,
3~ Kufanya Mazoezi,
4~ Kusaidia Wengine
5~ Kuwa na Malengo!